Afcon2019: Serengeti Boys yalazwa na Nigeria

Serengeti Boys Haki miliki ya picha Getty Images

Timu ya taifa ya Tanzania ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 The Serengeti Boys ilianza kwa mguu mbaya kampeni yake kushiriki katika kombe la mataifa ya Africa Afcon2019 baada ya kupoteza 5-4 kwa Nigeria katika uwanja wa kitaifa wa Dar-es salaam.

Serengeti ndio waliofungwa wa kwanza katika mechi hiyo ya magoli tisa katika robo ya kwanza ya mechi hiyo lakini wakasawazisha mara moja na kuleta usawa katika kipute hicho.

Lakini Nigeria waliendeleza mashambulizi makali na kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza Nigeria ilikuwa mbele kwa magoli 3-1.

Lakini katika kipindi cha pili vijana wa Serengeti waliingia na nguvu mpya wakitafuta kusawazisha na juhudi zao zilizaa matunda baada ya shambulizi la Kelvin John kumfunga kipa wa Nigeria.

Hatahivyo mambo yalibadilika baada ya Nigeria kupata mkwaju wa adhabu nje ya eneo hatari ambao walifunga.

Dakika nne baadaye Nigeria iliongeza bao lao la tano.

Vijana wa Serengeti sasa watakabiliana na Angola na Uganda katika mechi nyengine.

Wakati huohuo naibu mkufunzi wa klabu ya Taifa Stars hemed Morocco amesema kuwa wachezaji wake wako tayari kukabiliana na timu yoyote katika kombe la Africa zinazotarajiwa kuchezwa nchini Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19.

Timu ya Taifa Stars iko kundi Cha pamoja na majirani zao Kenya na Senegal na Algeria.

''Nina hakika tutaweka historia. Kila tunachohitaji kuandaa timu yetu mapema na kucheza mechi nyingi za kirafiki'', alisema katika mahojiano na gazeti la The Citizen nchini Tanzania kufuatia droo ya kombe la Africa siku ya Ijumaa usiku.

Morocco amesema kuwa Taifa Stars inashirikisha wachezaji wenye vipaji ambao wako tayari kuonyesha umahiri wao katikja mashindano hayo ya timu 24.

Hakuna kisichowezekana, alisema Morocco. Tumefanikiwa kufuzu katiika fainali na tunahitaji kunyesha kwamba tulihitaji kushinda.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii