Tetesi za soka Ulaya Jumanne 16.04.2019: Coutinho, Rashford, Pogba, Mane, Hazard, Benitez, Vieira

Haki miliki ya picha Getty Images

Real Madrid ina mipango miwili ya uhamisho-mmoja ukishirikisha kumsaini mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard mwenye umri wa miaka 28 mbali na kuwachukua kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba na mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane mwenye umri wa miaka 27. (El Confidencial - in Spanish)

Manchester United wamemwambia ajenti wa Pogba Mino Raiola kwamba Real Madrid italazimika kulipa Yuro milioni 150 ili kumsaini mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa 26. (Marca)

Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, 26, huenda akalengwa na Chelsea iwapo marufuku ya uhamisho ya Chelsea itaondolewa mwisho wa msimu lakini mchezaji huyo amekataa uhamisho wa kuelekea Manchester United. (Sport)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alikataa kuzungumzia hatma ya Coutinho wakati wa mkutano na vyombo vya habari wakati wa maandalizi ya kikosi chake katika mechi ya awamu ya pili ya robo fainali dhidi ya Barcelona. (Manchester Evening News)

Barcelona itajaribu kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford kwa dau la £100m. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ana mwaka mmoja katika mkataba wake na bado hajaongeza. (Mirror)

Manchester United imejiandaa kulipa £31m kumsaini beki wa Roma na Ugiriki Kostas Manolas, 27. (Leggo, via Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images

Newcastle United inatumai kuafikia makubaliano na mkufunzi Rafael Benitez kuhusu nyongeza ya kandarasi yake katika kipindi cha wiki mbili zijazo. (Newcastle Chronicle)

Mchezaji wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Patrick Vieira ni mmojawapo wa wawaniaji wa kazi ya ukufunzi katika klabu ya Lyon. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 42 kwa sasa anafunza klabu ya Nice. (Le Parisien, via Sun)

Image caption Inter Milan ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 28. (Tuttosport, via Calciomercato)

Nahodha wa klabu ya Manchester City Vincent Kompany anasema kuwa atakuwa katika klabu hiyo msimu ujao. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 anakamilisha kandarasi yake mwisho wa msimu huu . (Talksport)

Inter Milan ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 28. (Tuttosport, via Calciomercato)

Manchester United, Juventus na Paris St-Germain zinafikiria kumsaini kiungo wa kati wa klabu ya Sporting Lisbon na Ureno ,24, Bruno Fernandes. (A Bola, via Mail)

Haki miliki ya picha AFP

Hatma ya kiungo wa kati wa Southampton Jody Clasie katika klabu hiyo haijulikani. Raia huyo wa Uhalonzi ,27, yuko kwa mkopo katika klabu ya Feyenoord na alitarajiwa kujiunga nao kwa mkataba wa kudumu lakini haelewani na mkufunzi Giovanni van Bronckhorst. (Independent)

Maafisa wa Juventus watakutana na Benfica siku ya Jumanne ili kuzungumzia uhamisho wa mshambuliaji Joao Felix ambaye anataka kucheza na nyota mwenza wa Ureno Cristiano Ronaldo. (AS)

Mshambuliaji wa Newcastle United Dwight Gayle, 29, anasema kuwa huenda akaichezea West Brom msimu ujao ambapo mchezaji huyo wa Uingereza yupo kwa mkopo. (Shields Gazette)

Arsenal huenda ikamzuia mchezaji wa Algeria mwenye umri wa miaka 21 kutonunuliwa huku akidaiwa kuvutia klabu kama vile Empoli. (Le10 Sport, via Mirror)

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU

Arsenal wanataka kumsaini beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30. (Talksport)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa klabu hiyo huenda ikawauza wacheza muhimu mwisho wa msimu huu.

Raia huyo wa Ufaransa anataka kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake baada ya msururu wa matokeo mabaya msimu huu.. (Sky Sports)

mshambuliaji wa zamani wa Lyon Moussa Dembele.

Manchester United hawana hamu na mshambuliaji wa zamani wa Lyon Moussa Dembele.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amefunga magoli 18 katika mashindano yote msimu huu. (Mirror)

Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi anatarajiwa kuondoka Inter Milan msimu huu.

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa klabu hiyo huenda ikawauza wacheza muhimu mwisho wa msimu huu. Haki miliki ya picha Getty Images

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 huenda akahamia Real Madrid kwa dau la £52m. (AS)

Mchezaji anayelengwa na Liverpool na Bayern Munich Timo Werner hatotia saini kandarasi mpya na klabu ya RB Leipzig.

Kandarasi ya mshambuliaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23 katika klabu hiyo ya Bundesliga inakamilika mwisho wa msimu huu. (Sky Germany)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund 19 na Sweden Alexander Isak Haki miliki ya picha AFP

Chelsea itashindana na Real Madrid katika mbio za kumnunua ,mshambuliaji wa Borussia Dortmund 19 na Sweden Alexander Isak. (Sun)

Hatahivyo Zidane mwenye umri wa miaka 46 amepinga madai kwamba atamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema, 31. (Marca)

Na timu hiyo itamuuza beki wa Ufaransa Raphael Varane, 25, kwa dau la £437m kutokana na sheria inayomzuia katika kandarasi yake . (RAI Sport via Calciomercato)

Beki wa Ufaransa Raphael Varane, 25

Bayern Munich wanamtaka kiungo wa kati wa Roma na Itali Nicolo Zaniolo mwenye umri wa miaka 19. (Bild - in German)

Rais wa klabu ya Lille Gerard Lopez anasema kuwa winga wa Ivory Coast ,23, Nicolas Pepe, ambaye ananyatiwa na Manchester United, ataondoka katika klabu hiyo ya Ufransa mwisho wa msimu huu . (Manchester Evening News)

Leicester imewachukua vijana watatu ili kusaidia kuendeleza timu hiyo katika siku za usoni.

Bruno Fernandes Haki miliki ya picha AFP

Kiungo wa kati wa Guiseley Dylan Barkers, Beki wa Hasting United Jamie Fielding na kiungo wa kati wa Hasting Adam Lovatt wamejiunga na klabu hiyo. (Leicester Mercury)

Wawakilishi kutoka Manchester United, Juventus na Paris St-Germain walizuru klabu ya Aves ili kumtazama kiungo wa kati wa Sporting Lisbon ,24, Bruno Fernandes. (A Bola)

Kundi moja la wafanyibiashara linaloungwa mkono na European Money liko tayari kuinunua klabu ya Huddersfiedl Town kwa kitita cha £50m. (star)

TETESI ZA SOKA JUMAPILI

Ole Gunnar Solksjaer
Image caption Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solksjaer

Klabu ya Manchester United kumpatia kocha wao Ole Gunnar Solksjaer pauni milioni 200 za usajili. Hiko ndiyo kiwango kikubwa zaidi United kuwahi kutoa. (Sunday Express)

Kiungo Paul Pogba, 26, anatarajiwa kupewa unahodha katika klabu yake ya Manchester United ili kuzima mipango ya kuhamia Real Madrid. (Sunday Mirror)

Manchester United watachuana na mahasimu wao Manchester City katika mbio za kumsajili beki kinda wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England Aaron Wan-Bissaka, 21, mwenye thamani ya pauni milioni 40. (Mail on Sunday)

Miamba hiyo ya Old Trafford club pia ipo tayari kumlipa mshahara mara tatu ya anaopokea sasa kiungo Christian Eriksen, 27, wa Tottenham endapo atakubali kujiunga nao mwishoni mwa msimu.

Image caption Christian Eriksen

Man united pia wanaendelea kumnyemelea beki wa Napoli Kalidou Koulibaly. Beki huyo raia wa Senegal mwenye miaka 27 ana thamani ya pauni milioni 110. (Sunday Express)

Solskjaer: Tutaifunga Barcelona nyumbani kwao

Je Manchester United wataweza kuwazuia Suarez na Messi?

Kiungo wa Arsenal na Uswizi Granit Xhaka, 26, ananyemelewa na miamba ya soka nchini Italia klabu ya Inter Milan.(Sunday Express)

Barcelona wanatazamiwa kujaribu kumsajili tena winga wa Chelsea Willian, 30. Barca waliwahi kupeleka dau la pauni milioni 55 ili kimsajili Mbrazili huyo lakini wakakataliwa. (Sunday Telegraph)

Tottenham wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez. Gomez 22- mkataba wake una thamani ya pauni milioni 43. (Mail on Sunday)

Image caption Paulo Dybala wa Juventus

Juventus watalazimika kumuuza mshambuliaji wao Paulo Dybala, 25, ili kuwezesha kupata pauni milioni 86.4 ili wamsajili mshambuliaji wa Benfica Joao Felix, 19. (Tuttosport via Football Italia)

Rais wa Benfica Luis Filipe Vieira wiki iliyopita alikataa dau la pauni milioni 65 kutoka kwa miamba hao wa Italia. (O Jogo - in Portuguese)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii