Tanzania 0-1 Uganda: Serengeti Boys yalazwa mechi mbili mfululizo Afcon U-17

Serengeti Boys

Chanzo cha picha, Getty Images

Matumaini ya timu ya taifa ya Tanzania ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Serengeti Boys kusonga mbele kwenye mashindano ya kombe la mataifa ya Africa Afcon2019 yameyoyoma baada ya kupokea kipigo cha pili mfululizo.

Serengeti Boys leo ilishuka dimbani jijini Dar es Salaam kupambana na Uganda lakini mchezo huo umeisha kwa wageni kuondoka na ushindi wa goli 3-0.

Mechi ya awali Serengeti Boys walikubali kichapo cha goli 5-4 dhidi ya Nigeria. Uganda walifungwa 1-0 dhidi ya Namibia.

Timu hizo mbili zilishuka dimbani hii leo kila moja ikiwa na hamu ya kufufua matumaini, lakini Uganda waliomudu ipasavyo mchezo huo na kutumia vizuri madhaifu ya safu ya ulinzi wa Tanzania kuondoka na ushindi mnono.

Katika matokeo mengine ya kundi hilo, Nigeria imeifunga Namibia goli 1-0 na kujihakikishia nafasi katika raundi ifuatayo.

Kwa matokeo hayo, ili Tanzania ifuzu hatua inayofuatia, itaomba dua zote Nigeria iifunge Uganda, na wao wawafunge Angola goli nyingi ili wafuzu kwa tofauti ya magoli.

Tofauti na mchezo na Nigeria ambapo safu ya ushambuliaji ya Tanzania ilionekana kwenye makali, hii leo safu ya ulinzi ya Uganda iliwadhibiti vilivyo washambulizi wa Tanzania.

Uganda waliandika bao la kwanza kupitia Kawooya Andrew katika dakika ya 15 ya mchezo.

Dakika 14 baadae, Ivan Asaba aliiandikia Uganda bao la pili katika dakika ya 29 ya mchezo.

Wachezaji wa Serengeti Boys walijaribu kufurukuta na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Uganda lakini bahati haikuwa yao.

Najib Yiga alipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Serengeti Boys katika dakika ya 77 kwa kuunganisha krosi kwa kichwa cha kuparaza huku bila kubughudhiwa na mabeki wa Tanzania.

Kocha wa Serengeti Boys Oscar Mirambo amewapa moyo Watanzania kuwa bado kuna matumaini kwa timu yao kufuzu: "hesabu ya mwisho itafanyika siku ya mwisho. Tukiwafunga Angola, tutakuwa nao sawa kwa alama tatu. Nigeria akimfunga Uganda, itamaanisha kuwa Uganda watasalia na alama tatu pia, hivyo wote watatu tutakuwa sawa kialama. Tunatakiwa kushinda goli nyingi mchezo wa mwisho."

Hakuna kisichowezekana, alisema Morocco. Tumefanikiwa kufuzu katiika fainali na tunahitaji kunyesha kwamba tulihitaji kushinda.