Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 18.04.2019: Salah, Giroud, De Ligt, Sancho, Pogba, Rashford

Mohamed Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 26, anataka kuondoka katika klabu hiyo na anapanga kuwasilisha ombi la uhamisho. (As.com)

Hatahivyo, ajenti wa Salah Ramy Abbas Issa amekanusha taarifa hizo katika mitandao ya kijamii. (Twitter)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 32, anatarajiwa kukataa maongezi ya mkataba kwa miezi 12 kuondoka Stamford Bridge katika msimu wa joto (Mirror)

Mlinzi wa Ajax Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 19, analengwa na Tottenham, huku Spurs ikiwa radhi kulipa kitita kilichomfunga mchezaji huyo raia wa Uholanzi cha thamani ya £69. (Star)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atakabidhiwa £250m kutumia katika dirisha la uhamisho msimu wa joto, akiwemo mchezaji wa kiungo cha mbele wa Borrussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Ufaransa na Manchester United Paul Pogba, anatarajiwa kujiunga na mchezaji wa Chelsea Eden Hazard katika kuhamia Real Madrid. (Sun)

Na mshambuliaji wa Reds Marcus Rashford, aliye na miaka 21, anasita kusaini kuongezwa kwa mkataba wake Old Trafford, huku mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa England akiitisha kitita cha £200,000 kwa wiki. (Mail)

Barcelona inataka kumkabidhi winga wa Brazil Malcom, aliye na miaka 22, katika makubaliano ya kubadilishana na Rashford. (Mundo)

Waangalizi wa Arsenal wamekuwa wakimwinda mchezaji wa Ajax David Neres, mwenye umri wa miaka 22, wakati timu hiyo ikijiunga na Juventus katika kuonyesha hamu ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Brazil. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Zenit St Petersburg inamtaka mchezaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 24 Mateo Kovacic, ambaye yuko Stamford Bridge kwa mkopo kutoka Real Madrid. (Sun)

Winga wa Newcastle Matt Ritchie, mwenye umri wa miaka 29, huenda akaondoka St James' Park, huku Bournemouth ikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uskotchi. (Chronicle)

Everton na Arsenal zinamtaka mshambuliaji wa Fortuna Dusseldorf na timu ya taifa ya Ubelgiji Benito Raman, kwa kitita cha £15m (Sport Bild -kupitia Sport Witness)

Mshambuliaji wa Chelsea aliyechukuliwa kwa mkopo Tammy Abraham, huenda akarudi katika kalbu yake badala ya kusalia Aston Villa msimu ujao. (Football.London)

ZILIZO BORA KUTOKA JUMATANO:

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea iko tayari kumpoteza nyota wao na mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, na sasa inataka kumbadilisha na winga wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe, 23. (Mirror)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane ameitaka klabu hiyo kumuuza winga wa taifa la Wales Gareth Bale hata iwapo watapoteza pesa.. (Independent)

Tottenham inaongoza katika harakati za kumsaini winga wa Fulham ,18, Ryan Sessegnon kufuatia kazi nzuri inayofanywa na mkufunzi Mauricio Pochettino kuwajumuisha wachezaji kinda wa Uingereza. (Sun)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anataka kumsaini mshambuliaji wa Burnley ,19, Dwight McNeil, pamoja na kiungo wa kati wa Bournemouth Ryan Fraser, 25, na David Brooks, 21. (star)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amemtaka mshambuliaji wa Brazil,18, Vinicius Junior kwenda Real Madrid badala ya Sadio Mane wakati mibabe hiyo ya Uhispania ilipomtaka mshambuliaji huyo wa Senegal msimu uliopita. (El Chiringuito, via Metro)

Mkopo wa Denis Suarez katika klabu ya Arsenal haujapendeza na kiungo huyo wa Barcelona huenda akaelekea katika klabu ya Napoli kulingana na ajenti wake (Radio Kiss Kiss, via Mirror)

Arsenal ndio wanaopigiwa upatu kumsaini beki wa Barcelona Samuel Umtiti, lakini Manchester United pia wanamsaka mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25. (TuttoMercato, via Star)

Liverpool ina hamu ya winga wa Bayer Leverkusen raia wa Ujerumani Julian Brandt. (Bild, via Calciomercato)

Rais wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness anasema kuwa atamnunua mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappe mara moja iwapo mabingwa hao wa Ujerumani wana uwezo wa kumnunua mchezaji huyo wa PSG . (Deutschen Presse-Agentur, via Goal)

Klabu ya Uingereza Wolves wanafikiria kumsaini winga wa Liverpool mwenye umri wa miaka 18 raia wa Ureno Rafael Camacho. (O Jogo, via Mirror)

Klabu ya Ufaransa ya AS Monaco huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Ureno Adrien Silva kwa mkataba wa kudumu kutoka kwa Leicester. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amekuwa katika mkopo katika klabu hiyo tangu mwanzo wa mwaka huu. (France Football via Leicester Mercury)

Mtoto wa kiume wa Cristiano Ronaldo alifunga magoli saba katika kipindi cha kwanza cha mechi ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 10 na kuilaza Maritimo. (AS)