Wachezaji wa soka England kugomea mitandao ya kijamii kwa saa 24 kupinga ubaguzi

Danny Rose

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Danny Rose

Wachezaji wanaosakata soka ya kulipwa nchini England na Wales watagoma kutumia mitandao ya kijamii kwa saa 24 siku ya Ijumaa kulalamikia jinsi mitandao hiyo na wasimamizi wa kandanda wanavyoshughulikia suala la ubaguzi wa rangi.

Hii inafuatia visa kadhaa vya ubaguzi dhidi ya wachezaji wenzao katika mechi za nyumbani na za kimataifa.

Mapema wiki hii nahodha wa, Manchester United Ashley Young alishambuliwa katika mtandao wa Twitter hali ambayo ilimfanya nahodha wa Watford Troy Deeney kuingilia kati na kusema sasa'' mmezidi".

"Siku ya Ijuma tunatoa ujumbe kwa mtu yeyote anaewatukana wachezaji uwanjani au katika mitandao ya kijamii kwamba hatutakubali tena hilo katika ulimwengu wa soka," alisema Deeney, ambaye alifuta ujumbe katika mtandao wake wa Instagram baada ya kutusiwa mapema mwezi huu.

"Mgomu huo utatoa fursa kwa wachezaji kuzungumza kwa sauti moja dhidi ya ubaguzi wa rangi."

Chanzo cha picha, Getty Images

Danny Rose na wachezaji kadhaa wa England walizomewa wakati wa mechi za kufuzu kwa kombe la Euro 2020 nchini Montenegro mwezi uliopita.

Mlinzi huyo wa Spurs baadae alisema "hatakubali mtu mwingine yeyote kukabiliwa na visa vya kibaguzi uwanjani".

"Sitaki kuona mchezaji yeyote mpya akipitia yale niliyopitia katika taaluma hii," alisema Rose. "

Mlinzi wa Manchester United, Chris Smalling pia ameongeza kuwa: "Mda umewadia kwa mitandao ya kijamii ya Twitter, Instagram na Facebook kutafakari jinsi ya kukabiliana na suala la ubaguzu wa rangi.

Pia alisema ipo haja ya wamiliki wa mitandao hiyo kuzingatia umuhimu wa kulinda afya ya iakili ya watumiaji wa mitandao hiyo bila kujali umri wao, rangi ya ngozi yao, jinsia wala viwango vyao vya mapato.

Chama cha PFA kimesema kuwa mgomo huo ni mwanzo wa msururu wa kampeini ya kukabilina na ''ubaguzi wa rangi kaika mchezo wa kandanda".

Young alitukanwa baada ya United kuondolewa na Barcelona katika kinyang'anyiro cha kuwania kombe la klabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne. ''

Visa vya kibaguzi mwaka 2018-19

  • Desemba: Ganda la ndizi lilirushwa uwanjani wakati wa Derby ya London Kaskazini uwanjani Emirates, baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kufungia bao Arsenal.
  • Desemba: Raheem Sterling alidaiwa kushambuliwa kibaguzi wakati Manchester City iliposhindwa Chelsea. Sterling baadae alisema magazeti yanachochea "ubaguzi wa rangi"
  • Machi: Chelsea iliwasilisha malalamishi kwa Uefa baada ya mchezaji wake Callum Hudson-Odoi kubaguliwa wakati wa mechi ya marudiano ya Ligi ya Europa dhidi ya Dynamo Kiev.
  • March: England iliripoti visa vya wachezaji wake kubaguliwa waliposhinda Montenegro mabao 5-1 mjini Podgorica.
  • April: Mshambuliaji wa Juventus Mtaliano Moise Kean, 19, alitusiwa wakati wa mechi dhidi ya Cagliari.
  • April: Winga wa Derby Duane Holmes na mlinzi wa Wigan Nathan Byrne walitukanwa kwa misingi ya rangi ya ngozi yao katika mashindano hayo.
  • April: Deeney na wachezaji wenzake wa timu ya Watford Adrian Mariappa na Christian Kabasele walitukanwa katika mtandao wa kijamii.
  • April: Young alishambuliwa kwenye Twitter