Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 19.04.2019: Hazard, Pepe, Benitez, Zidane, Demirbay, Koulibaly

Eden Hazard

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid inakaribia kumsaini mshambuliaji wa Ubelgiji na Chelsea Eden Hazard ,28, kwa karibia dau la Yuro milioni 100. (Marca - in Spanish)

Hatahivyo imeripotiwa kwamba The Blues wamepunguza fedha wanazomuuzia Hazard, huku wakimlenga mshambuliaji wa Ivory Coast na Lille Nicolas pepe,23, ili kuchukua mahala pake. (AS - in Spanish)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane atakabidhiwa £430m kutumia mwisho wa msimu ) huku akimlenga kiungo wa kati wa Man United na Ufaransa Paul Pogba, 26, na mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 27, . (Mirror)

Chanzo cha picha, Reuters

Newcastle itampatia mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez kitita cha £50m ili kumshawishi raia huyo wa Uhispania kusalia katika uwanja wa St James' Park. (Mail)

Benitez amekabidhiwa £100m kutumia katika ununuzi wa wachezaji ili kuimarisha klabu ya Newcastle.. (Mirror)

Arsenal ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Hoffenheim na Ujerumani Kerem Demirbay, 25, kwa dau la £22m, ili kuchukua mahala pake kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey. (Metro)

Beki wa Napoli na Senegal mwenye umri wa miaka 27 Kalidou Koulibaly amekana kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo ya Serie A kuelekea Man United. (Express)

Southampton inafikiria kumsaini kiungo wa kati wa Rangers na Canada Scott Arfield, 30. (mirror)

Mkurugenzi wa Newcastle Lee Charnley ameonya kwamba klabu hiyo itaendelea kuishi ndani ya uwezo wake baada ya kuripoti faida ya £18.6m baada ya kutozwa kodi. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Reuters

Naibu mkufunzi man United Mike Phelan anamshauri mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer kuhusu mipango yake ya uhamisho mwisho wa msimu huu. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Roma na Bosnian Edin Dzeko, 33, yuko tayari kujiunga na Inter Milan na hayuko tayari kurudi nchini Uingereza. (Calciomercato)

Chanzo cha picha, EPA

Mshambuliaji wa Uhispania Diego Costa, 30, amekataa kufanya mazoezi na Atletico Madrid baada ya kupigwa marufuku kutocheza mechi nane. (AS - in Spanish)

Liverpool huenda ikashiriki katika mechi ya kirafiki nyumbani huku uwanja wa klabu ya Tottenham ikitarajiwa kuandaa mechi hiyo. (Liverpool Echo)