Tetesi za soka Jumamosi tarehe 20.04.2019: Zaha, Lukaku, Pogba, De Gea, Sane, Jesus, Danilo, Tagliafico

Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26,amesema yuko tayari kuondoka Crystal Palace na anataka kucheza Championi Ligi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26,amesema yuko tayari kuondoka Crystal Palace na anataka kucheza Championi Ligi

Mchezaji wa safu ya mashambulizi Ivory ya Coast Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26,amesema yuko tayari kuondoka Crystal Palace na anataka kucheza Championi Ligi. (Mail)

Manchester United wanajiandaa kusikia ni nini Romelu Lukaku atakachotaka msimu huu, huku mshambuliaji huyo mwenye uraia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 25 akiwqa tayari kuondoka Old Trafford. (Telegraph)

Mshambuliaji wa safu ya kati Mfaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, na mlinda lango Muhispania David de Gea,mwenye umri wa miaka 28,wametumia hali ya sintofahamu juu ya ikiwa Manchester watafuzu kwa ajili ya Championi Ligi au la kudai ongezeko kubwa la mshahara ili wabaki Old Trafford. (Times - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

David de Gea na Pogba wanasemekana kutumia sintofahamu juu ya ikiwa Manchester United watafuzu kwa Chambpioni Ligi kw akudai malipo ya juu zaidi

Kiungo wa kati Mjerumani Leroy Sane,mwenye umri wa miaka 23, na mshambuliaji kutoka Brazil Gabriel Jesus, mwenye umri wa miaka 22, ni wachezaji wawili tu miongoni mwa wachezaji takribani wanane walioombwa kuondoka Manchester City ikatika msimu ujao. (El Chiringuito, via Sun)

Inter Milan wanafanya mashauriano na mchezaji wa kimataifa wa safu ya ulinzi ya Manchester City Mbrazilo Danilo, mwenye umri wa miaka 27. (Calciomercato)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Real Madrid bado ina matumaini ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Paris St-Germain Mbrazili Neymar

Mchezaji wa Arsenal Nicolas Tagliafico, mwenye umri wa miaka 26, amekataa ofa ya mkataba mpya na Ajax na muwakilishi wake, Ricardo Schlieper, amedokeza kuwa mlinzi huyo wa Argentina angependelea kuhamia Italia. (Football London)

Real Madrid bado ina matumaini ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Paris St-Germain Mbrazili Neymar,ambaye ana umri wa miaka 27 kwa sasa. (Marca)

Timu hiyo inayoongoza katika Ligi ya Uhispania pia wanakamilisha mkataba wa kumchukua mshambuliaji Mserbia Luka Jovic, mwenye umri wa miaka 21 kutoka Eintracht Frankfurt . (Star)

meneja wa Chelsea Maurizio Sarri ameonyesha dalilli kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Mfaransa Olivier Giroud mwenye umri wa miaka 32 hataondoka Chelsea msimu ujao (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Real Madrid wanakamilisha mkataba wa kumchukua mshambuliaji Mserbia Luka Jovic kutoka Eintracht Frankfurt

Napoli wanaangalia uwezekano wa kumchukua mchezaji wa safu ya nyuma wa Tottenham na England Kieran Trippier, mwenye umri wa miaka 28. (Football Italia)

Arsenal na Everton wanaangalia uwezekano kumuhamisha mshambuliaji Fortuna Dusseldorf ya Mbelgiji Benito Raman,mwenye umri wa miaka 24 kwa £13m . (Bild, via Sun)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez kulipwa £50m kila mwaka , kabla ya mauzo ya mchezaji , kama atakubali kusaini mkataba mpya

Meneja wa Burnley Sean Dyche hawezi kusema mengi juu ya yale anayoyafikiria kuhusu thamani ya Dwight McNeil baada ya winga huyo wa Uingereza kwenye umri wa miaka 19- kusemekana anatakiwa na Arsenal, Manchester City, Liverpool, Everton na Newcastle. (Burnley Express)

Newcastle imemuambia meneja Rafael Benitez atakuwa anapewa £50m kila mwaka , kabla ya mauzo ya mchezaji , kama atakubali kusaini mkataba mpya . (Independent)

Maelezo ya picha,

Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde amemuelezea Pep Guardiola kama mtu aliye bora zaidi katika biashara

Mchezaji wa safu ya kati wa Southampton kutoka Northern Irish Steven Davis, mwenye umri wa miaka 34, anayecheza kwa deni katika Rangers, ameanza mazungumzo na klabu ya Uskochi juu ya kuhama msimu huu. (Sky Sports)

Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde amemuelezea Pep Guardiola kama mtu aliye bora zaidi katika biashara, licha ya Manchester City kuendolewa katika Championi Ligina Tottenham. (Marca)

Mchezaji wa Aston Villa Ross McCormack, mwenye umri wa miaka 32, hatarudi katika Motherwell -timu anayoichezea mshambuliaji huyo wa Uskochi imethibitisha. (Daily Record)

Unai Emery anasema ana uwezo wa kudhibiti muda wake wa maombi ya muda wa mchezo miongoni mwa wachezaji wake wa kufuatia tetesi juu ya mshambuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette, mwenye umri wa miaka 27. (Football London)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na England Andy Cole, anataka kuongoza timu ya soka ya England kupambana na ubaguzi wa rangi

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na England Andy Cole, mwenye umri wa miaka 47, anataka kuongoza timu ya soka ya England kupambana na ubaguzi wa rangi na kumrithi Lord Herman Ouseley kama mwenyekiti wa taasisi ya kukabiliana na ubaguzi -Kick It Out. (Mirror)

Mashabiki wa Leeds wanaeneza tetesi juu ya uwezekano wa kurejea kwa mchezaji wao wa zamani James Milner baada ya mchezaji huyo wa safu ya kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 33 ambaye hana mkataba msimu ujao, kutokuwa miongoni mwa wachezaji walioorodhishwa na Liverpool katika kikosi chao cha 2019-20. (Express)