Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 21.04.2019: Rashford, Eriksen, Zaha, De Gea, Almada

Marcus Rashford

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Marcus Rashford

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 21, huenda asihame klabu hiyo kama ilivyodaiwa baada ya Barcelona kukiri kuwa na hofu ya kugharamika zaidi kumshawishi nyota huyo kuondoka Old Trafford. (Express)

Tottenham ina matumaini makubwa ya kuwa kiungo wao wa kati Christian Eriksen, 27, ambaye amehusishwa na tetesi za kuhamia Real Madrid, atasaini mkataba mpya wa mda mrefu. (Goal.com)

Paris St-Germain aiko tayari kutoa ofa ya takribani pauni milioni 65 kumnunua mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 26, ambaye anajiandaa kuhama klabu hiyo msimu ujao. (Express)

Crystal Palace inamtaka Zaha kwa pauni milioni 80 lakini haitaki kumuuza kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast na beki wakeb wa kulia Aaron Wan-Bissaka, 21, msimu wa ujao. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wilfried Zaha, Mshambuliaji wa Crystal Palace

Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, anasemekana kutofurahishwa na hatua ya klabu hiyo kuhusu ombi lake la mda mrefu la kutaka kuongezewa mshahara. (Times)

Manchester City inapania kumnunua kiungo wa kati Muargentina Thiago Almada, 17 - ambaye anasifiwa kuwa Lionel Messi mpya anayechezea moja ya vilabu tano kuu nchini mwake, Velez Sarsfield - kwa kimmkataba wa pauni milioni 20. (Sun)

Kiungo wa kati wa Ajax Hakim Ziyech, 26, anaweza kupatikana kwa pauni milioni 25 tu, bei ambayo tayari imezivutia vilabu vya City, Manchester United, Arsenal na Liverpool. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Gareth Bale

Mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale huenda akajiunga na ligi ya Uchina, Umoja wa milki za Kiarabu, MLS, ama moja ya vilabu tagika barani Ulaya - Lakini hilo linaweza kufanyika ikiwa mkataba wake wa sasa unaokadiriwa kuwa pauni 500,000 kwa wiki utasawazishwa na malipo ya Welshman ambaye mkataba wake unaendelea hadi mwaka 2022. (Mirror)

Manchester City ina mpanga wakumnunuia kiungo matata wa Benfica Joao Felix, 19, na wamekua wakifuatilia mchezo wa mshambulioaji wa Eintracht Frankfurt Luka Jovic, 21. (Goal.com)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Joao Felix(Kushoto)

Manchester City inajiandaa kumpatia John Stones mkataba mpya katika juhudi ya kumhakikishia mlinzi huyo wa England wa miaka 24 kuwa bado yuko katika mipango ya usoni ya kocha Pep Guardiola. (Mirror)

Paris St-Germain huenda akamrudisha uwanjani mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 27, ili ashiriki mchezo wao dhidi ya Monaco Jumapili usiku.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Neymar hajaonekana uwanjani tangu mwezi Januari baada ya kuumia mguu

Nyota huyo hajaonekana uwanjani tangu mwezi Januari baada ya kuumia mguu (L'Equipe - in French)

Beki wa kati wa Bayern Munich Niklas Sule, 23, ni mlinzi wa hivi punde kujumuishwa katika orodha ya uhamisho wa wachezaji wanaopigiwa upatu kujiunga na Manchester United msimu ujao. (Sport1, via Mirror)

Manchester United pia inapania kuwasaini kiungo wa kati wa West Ham, Declan Rice, 20, winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18, na winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19 - kwa mujibu wa mshambuliaji wa mshambuliaji wa zamani wa England Paul Merson. (Star)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Winga wa Chelsea, Callum Hudson-Odoi

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane, ambaye amehusishwa na tetesi za uhamisho wa mshambuliaji wa Paris St-Germain striker Kylian Mbappe, 20, amekiri kuwa atafanyia marekebisho mfumo wa mchezo wa klabu hiyo msimu ujao lakini amekataa kuzungumzia wachezaji anaowalenga katika mpango huo. (London Evening Standard)

Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Edu, 40, anajiandaa kujiunga na klabu hiyo tena kama mkurugenzi wa kiufundi, huku Mbrazil Gabriel Martinelli 17, akiorodheshwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na na klabu hiyo msimu wa joto. (Mail)