Everton 4-0 Manchester United: Manchester United yachakazwa na Everton

Gylfi Sigurdsson

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Gylfi Sigurdsson akiifungia Everton bao la pili kupitia mkwaju hatari

Everton huenda imezima matumaini ya Manchester United kumaliza katika nafasi ya nne bora katika michuano ya Ligi ya Premia ligi baada ya kuilaza mabao 4-0.

Ushindi huo wa Everton katika uwanja wa Goodison Park huenda pia umeweka bayana changamoto inayomkabili meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer..

Awali kipa wa United David de Gea alifanikiwa kuokoa bao la Richarlison kabla ya Mbrazili huyo kuingiza kimyani bao la kwanza katika dakika ya 13 iliyofuatiwa na mchezo wa hali ya juu ulioneshwa na timu hiyo chini ya ukufunzi wa Marco Silva.

De Gea alishindwa kuzuia kombora lililopigwa Gylfi Sigurdsson hatua 25 kutoka kwa lango la United, huku Everton ikitwaa udhibiti wa mchezo huo wa kusisimua.

Chanzo cha picha, EPA

Everton haikukomea hapo kwani iliendeleza mashambulizi ambapo Lucas Digne alifunga baada ya De Gea kutema mpira wa kona, nae Theo Walcott akatia wavuni pasi ya Sigurdsson na kuwa bao la nne.

United wapepiteza mara sita katika mechi nane walizocheza, huku ushindi huu wa Everton ukiandikisha historia ya klabu hiyo kushindwa mara tano mtawalio katika mechi za ugenini kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1981 - Hali ambayo inawaeka katika uwezekano wa kushiriki Ligi ya Europamsimu ujao.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mfumo wa mchezo wa upande wa Silva uliifanya United kikimbizwa bila huruma kwa dakika 90 minutes, lakini wadadisi wa soka wanasema - Everton ilionesha ujuzi na mchezo wa hali ya juu dhidi ya United.

Idrissa Gueye alidhibiti safu ya kati huku Sigurdsson na Mbrazili Bernard wakichonga mabao yote yaliyofungwa kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo.

Kumekuwa na hofu kuhusu hatma ya meneja Marco Silva katika klabu hiyo lakini ushindi huu wa leo bila shaka huenda ukabdaili dhana hiyo kwani umemfanya kupata uungwaji mkono mkubwa wa mashabiki wa Everton