Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 22.04.2019: Pogba, Coutinho, Hazard, Phelan, Carrick, Perez

Paul Pogba

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Real Madrid kufikia kiwango cha mshahara akitakacho Pogba?

Kiwango cha mshahara anachokitaka kiungo wa Manchester United Paul Pogba, 26, kinaweza kikawa kikwazo kwa Real Madrid kumsajili nyota huyo raia wa Ufaransa. (AS)

Chelsea wannapiga hesabu za kumnyakua kiungo wa Brazil na klabu ya Barcelona Philippe Coutinho, 26, kama mbadala wa mshambuliaji wao raia wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, ambaye mwisho wa msimu anatarajiwa kuhamia Real Madrid.(Calciomercato)

Klabu ya Manchester United ipo tayari kumpandisha Mike Phelan mpaka kuwa mkurugenzi wa ufundi, na nafasi yake ya meneja msaidizi kupewa kiongo wa zamani wa klabu hiyo Michael Carrick. (Mail)

Mchezaji nyota wa zamani wa Arsenal ambaye pia alitimuliwa kwenye kazi ya ukufunzi na klabu ya Monaco, Thierry Henry, 41, yumo kwenye mazungumzo na klabu ya New York Red Bulls ya ligi ya soka Marekani ili kujiunga nao kama mkufunzi. (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Kylian Mbappe amewahakikishia maswabiki wake kuwa habanduki PSG

Mshambuliaji nyota wa Ufaransa na klabu ya PSG Kylian Mbappe, 20, amekanusha uvumi ulioenea kuwa ana mpago wa kuhamia Real Madrid. Mbappe ametoa kauli hiyo baada ya kuifunga goli tatu timu yake ya zamani Monaco. (Goal.com)

Beki raia wa Brazil Marcelo, amesisitiza kuwa hana mpango wa kuihama klabu yake ya Real Madrid mwishoni mwa msimu - licha ya uvumi kuenea kuwa mchezaji huyo alikuwa akitammani kuungana tena na Cristiano Ronaldo, katika klabu ya Juventus. (Bein Sports, via Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Marcelo (kulia) ameamua kuuzima uvumi kuwa anajipanga kuhamia Juventus mwishon mwa msimu.

Kocha wa muda mrefu wa wachezaji chipukizi wa Aston Villa Sean Kimberley ameikacha klabu hiyo. (Birmingham Mail)

Bosi wa Newcastle Rafa Benitez amedai kuwa mfumo wa mishahara wa klabu hiyo unaifanya timu isiwe na matokeo mazuri kwenye Ligi ya Premia. (Newcastle Chronicle)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rafa Benitez amekuwa akihusishwa na mipango ya kuihama Newcastle

Mshambuliaji wa Newcastle raia wa Uhispania Ayoze Perez, 25, ameashiria kuwa anataka kuihama klabu hiyo mwushoni mwa msimu. (Mirror)

Rais wa klabu ya Nice ya Ufaransa Gauthier Ganaye amesema klabu yake huenda ikamsajili mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud, 32. (Goal.com)

Tetesi bora Jumapili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Marcus Rashford

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 21, huenda asihame klabu hiyo kama ilivyodaiwa baada ya Barcelona kukiri kuwa na hofu ya kugharamika zaidi kumshawishi nyota huyo kuondoka Old Trafford. (Express)

Tottenham ina matumaini makubwa ya kuwa kiungo wao wa kati Christian Eriksen, 27, ambaye amehusishwa na tetesi za kuhamia Real Madrid, atasaini mkataba mpya wa mda mrefu. (Goal.com)

Paris St-Germain haipo tayari kutoa ofa ya takribani pauni milioni 65 kumnunua mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 26, ambaye anajiandaa kuhama klabu hiyo msimu ujao. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wilfried Zaha

Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, anasemekana kutofurahishwa na hatua ya klabu hiyo kuhusu ombi lake la mda mrefu la kutaka kuongezewa mshahara. (Times)

Manchester City inapania kumnunua kiungo wa kati Muargentina Thiago Almada, 17 - ambaye anasifiwa kuwa Lionel Messi mpya anayechezea moja ya vilabu tano kuu nchini mwake, Velez Sarsfield - kwa kimmkataba wa pauni milioni 20. (Sun)

Kiungo wa kati wa Ajax Hakim Ziyech, 26, anaweza kupatikana kwa pauni milioni 25 tu, bei ambayo tayari imezivutia vilabu vya City, Manchester United, Arsenal na Liverpool. (Mirror)