Tetesi za soka Ulaya Jumatano 24.04.2019: Felix, Zaha, Sane, Trippier, Gattuso, Mahrez, Hudson-Odoi, Coutinho, Richarlison

Joao Felix miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa na Juventus
Maelezo ya picha,

Joao Felix miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa na Juventus

Mchezaji wa safu ya kati wa Benfica Mreno Joao Felix ambaye sasa ana umri wa miaka 19 yuko juu kwenye orodha ya uhamisho iliyotolewa na mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 34, kwa klabu yake. Washambuliaji wawili wa Ureno waliokuwa zamani katika Real Madrid - Muhispania anayecheza safu ya kati Isco, 27, na mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, mwenye umri wa miaka 25 - pia walikuwa kwenye orodha hiyo. (Corriere dello Sport, via Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa upande mwingine , Ronaldo ameidhinisha dau la £100m la mabingwa wa championi Serie A kwa Mreno mwenzake Felix, ambaye ana mkataba wa euro 120m. (A Bola, via Metro)

Crystal Palace watatakiwa kushusha bei yao ya £75m wanayotaka kumtoa Wilfried Zaha mwenye umri wa miaka 26 ikiwa mshambuliaji huyo wa Ivory Coast anataka kuhamia katika klabu ya Championi Ligi. Tottenham, Arsenal na Manchester United wogte wanamtaka lakini wanataka mkataba mzuri. (Star)

Manchester City wanahofu kuwa winga wao Mjerumani Leroy Sane, mwenye umri wa miaka 23, anaagalia uwezekano wa kuondoka kwenye klabu hiyo kutokana na kwamba mazungumzo ya mkataba wake yamekwama (Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester City wanahofu kuwa winga wao Mjerumani Leroy Sane ataondoka kwenye klabu hiyo baada ya mazunguzo ya mkataba wake kukwama

Manchester United wamemchagua mchezaji wa safu ya kulia nyuma wa timu ya Uingereza ya Tottenham Kieran Trippier, mwenye umri wa miaka 28, kama mchezaji mbadala wanaelenga kumchukua ikiwa watashindwa kusainimkataba na Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 21,kutoka Crystal Palace. (Mirror)

Kwa upande mwingine , United wanaamini Mbeljgiji Thomas Meunier mwenye umri wa miaka 27 anayechezea Paris St-Germain safu ya nyuma kulia ni mchezaji ambaye anayeweza kupatikana kwa bei nafuu na kwa urahisi zaidi anayeweza kukaba nafasi ya Trippier au Wan-Bissaka. (Independent)

Liverpool watadai 40m euros kwa Mserbia Marko Grujic mwenye umri wa miaka 23 -kiungo wa kati huku klabu ya Uhispani ya Atletico Madrid ikionyesha nia ya kumtaka. (ESPN)

Maelezo ya picha,

Liverpool watataka malipo ya 40m euros kwa Mserbia Marko Grujic

Newcastle wanaangalia uwezekano wa kumchukua meneja wa AC Milan Mtaliano Gennaro Gattuso, mwenye umri wa miaka 41, kuchukua nafasi ya kocha wao Muhispania Rafael Benitez ambaye zaza ana umri wa miaka 59 ikiwa ataamua kuondoka mwishoni mwa msimu huu. (Gazzetta - in Italian)

Mshambuliaji wa Manchester City Riyad Mahrez anatishia kuondoka kwenye klabu hiyo na winga huyo Mualgeria mwqenye umri wa miaka 28, amekwisha lalamika wazi juu ya kunyimwa muda wa kucheza chini ya meneja Pep Guardiola. (Mail)

Hali ya baadae ya mchezaji wa safu ya kati wa Barcelona Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 26, itategemea ikiwa Fifa itaamua kuchelewesha marufuku ya kuhama dhidi ya Chelsea, huku Manchester United pia wakiwafuatilia kwa karibu wachezaji huyo maarufu wa Brazil . (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Hali ya baadae ya mchezaji wa safu ya kati wa Barcelona Philippe Coutinho itategemea ikiwa Fifa itaamua kuchelewesha marufuku ya kuhama dhidi ya Chelsea

Mlindalango wa Atletico- Madrid Jan Oblak mwenye umri wa miaka 29- raia wa Slovenia ni goli kipa namba moja katika orodha ya Manchester United ya walinda lango wanaoweza kukaba nafasi ya David de Gea wakati hatma ya Muhispania huyo mwenye umri wa miaka 28 katika Old Trafford ikiwa haieleweki. (Metro)

AC Milan wanataka kusaini mkataba na mshambuliaji wa Everton Mbrazili Richarlison,mwenye umri wa miaka 21, hata hivyo klabu hiyo ya mabingwa wa Ligi ya Utaliano watatakiwa kuingia Championi Ligi na kulipa 75m euro kwa mujibu wa tathmini ya Ligi ya Primia. (Calciomercato)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Meneja wa Arsenal Unai Emery anakabiliwa na kipindi kigumu cha kipindi cha uhamisho kutokana na hofu inayozingira klabu hiyo juu ya muswada wa malipo ya mshahara

Arsenal wanahusishwa na uhamisho wa Mbrazili Gabriel Martinelli mwenye umri wa miaka 17. Winga huyo ambae kwa sasa anachezea timu ya Ituano, anaaminiwa kuwa anakamilisha mchakato wa kupata Paspoti ya Ulaya . (UOL Esporte, via Evening Standard)

Hata hivyo, meneja wa Arsenal Unai Emery anakabiliwa na kipindi kigumu cha kipindi cha uhamisho kutokana na hofu inayozingira klabu hiyo juu ya muswada wa malipo ya mshahara. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Stoke City wanadai £30m kwa ajili ya mlindalango Jack Butland anayelengwa na klabu za Primia Ligi Bournemouth na Crystal Palace

Mshambuliaji wa Roma, raia wa Bosnia Edin Dzeko, mwenye umri wa miaka 33, ataiangusha West Ham msimu huu kwa nia yake ya kutaka kujiunga na Inter Milan. (Calciomercato)

Stoke City wanadai £30m kwa ajili ya mlindalango Jack Butland mwenye umri wa miaka 26 kutoka Uingereza , anayelengwa na klabu za Primia Ligi Bournemouth na Crystal Palace. (Mail)

Ajax wako tayari kutoa mkataba mzuri wa muda mrefu kwa meneja Muholanzi Erik ten Hag mwenye umri wa miaka 49 ili kuzuwia klabu za Primia Ligi kumchukua. (Telegraph)

Norwich City watakuwa na ukomo wa bajeti ya £20m kwa ajili ya uhamisho kwani wanajiandaa kwa ajili ya Primia Ligi msimu ujao . (Mail)