Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 25.04.2019: Ronaldo, Guardiola, Oblak, Eriksen, Herrera, Pogba, Luis

Cristiano Ronaldo atakubali uteuzi wa meneja wa Manchester City Pep Guardiola kama kocha

Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 34, ataafiki uteuzi wa meneja wa Manchester City Pep Guardiola kama kocha . (Marca)

Manchester United wametenga pesa za dharura kwa ajili ya kuwalipa wachezaji wanaotaka kuowaondoa kikosini msimu ujao(Sun)

Mlindalango wa Atletico Madrid Mslovenia Jan Oblak, mwenye umri wa miaka 26, yuko juu katika orodha ya Manchester United ya watu wanaoweza kuchukua nafasi ya David De Gea iwapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka, 28, ataondoka Old Trafford. (Metro)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer itabidi awe mvumilivu katika nia yake ya kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati msimu ujao hadi pale atakapojua kama mchezaji kutoka Uhispania Ander Herrera, mwenye umri wa miaka 29, atabaki kwenye klabu hiyo au la . (Teamtalk)

Maelezo ya picha,

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer itabidi atulize kiu yake ya kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati kuchukua nafasi ya Ander Herrera

Tottenham inakabiliwa na hali ya sintofahamu juu ya ikiwa wamuuze mchezaji mahiri Christian Eriksen msimu ujao. Mzezaji huyo wa kimataifa wa Denmark ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 27, ametimiza zaidi ya mwaka mmoja tangu ajiondoe kwenye mkataba wa sasa wa £75,000- mkataba wa wiki moja na Real Madrid na Inter Milan wanamfuatilia kwa karibu. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa Liverpool Muholanzi Virgil van Dijk, anatarajiwa kutajwa kama mchezaji wa PFA wa mwaka huu

Mmiliki wa klabu ya Port Vale Norman Smurthwaite anakaribia kuiuza klabu hiyo na anaangalia uwezekano wa kununua klabu ambazo bado inang'ang'ana katika Ligi ya pili pili Notts County. (mirror)

Mkurugenzi mkuu wa Billy Hogan amesifu usajili wa kikosi cha ''bora '' cha Liverpool kwa kusaidia kuipeleka klabu hiyo katika mashindano ya kombe la Primia Ligi na Championi Ligi . (Liverpool Echo)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Roy Keane anasema kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, ni "tatizo kubwa " katika Manchester United

Mlinzi wa Liverpool Muholanzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kutajwa kama mchezaji wa PFA wa mwaka kabla ya mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 24. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Stoke na Scotland Darren Fletcher, mwenye umri wa miaka 35, ambaye mkataba wake utakamilika msimu huu , anaweza kurejea Manchester United katika nafasi ya usajili. (Telegraph)

Kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, ni "tatizo kubwa " katika Manchester United, anasema kiungo wa kati wa zamani Roy Keane. (Sky Sports)

Arsenal imepanga tarehe kwa ajili ya uwezekano wa kusiani mkataba na Gabriel Martinelli, mwenye umri wa miaka 17, kutengeneza dau lake baada ya kukubali mkataba na Ituano kumsajili mshambuliaji huyo kutoka taifa la Brazil. (Yahoo Brasil via Metro)

Manchester City wanaangalia uwezekano wa kumchukua kiungo wa kati wa Benfica Florentino Luis mwenye umri wa miaka 19- kutoka Ureno. (Guardian)