London Marathon 2019: Eliud Kipchoge ashinda London Marathon mara ya nne mfulululizo

Mkenya Eliud Kipchoge ashinda London Marathon 2019 Haki miliki ya picha PA
Image caption Mkenya Eliud Kipchoge

Mkenya Eliud Kipchoge ameshinda London Marathon kwa mara ya nne mfululizo.

Kipchoge, 34, ambaye alivunja rekodi ya dunia ya mbio hizo mjini Berlin mwaka jana, alikamilisha mbio za leo kwa muda wa saa mbili dakika mbili na sekunde thalathini na nane (2: 02: 38.)

Waethiopia Mosinet Geremew na Mule Wasihun walimaliza katika nafasi ya pili na ya tatu nyuma ya Kipchoge, ambaye alikosa kuvunja rekodi yake mwenyewe ya Dunia kwa sekunde 59 ambayo ilikua 2:01:39.

Muingereza Mo Farah alichukua nafasi ya tano baada ya kumaliza dakika 3 na sekunde moja nyuma ya Kipchoge, huku Muingereza Callum Hawkins akimaliza katika nafasi ya 10.

Mkenya mwingine Brigid Kosgei, 25, alishinda mbio hizo upande wa kinadada na kuwa mwanamke wa kwanza wa umri mdogo kushinda London marathon upande wa wanawake.

Kosgei alimshinda bingwa mtetezi Vivian Cheruiyot kwa kutumia mda wa saa 2:18:20 kushinda mbio hizo kwa mara ya kwanza.

Mkenya Vivian Cheruiyot alichukua nafasi ya pili huku Roza Dereje wa Ethiopia akimaliza wa tatu.

Muingereza Charlotte Purdue alimaliza nafasi ya 10.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakiambiaji wa kiuume mwanzo wa mbio hizo

Maelfu ya watu waMEshiriki makala ya 39 ya mbio za London Marathon 2019.

Mbio hizo zimechangisha £1bn tangu zilipoanzishwa mwaka 1981, kwa mujibu wa wadhamini Virgin Money.

Mshirikishi wa mbio hizo Hugh Brasher amesema : "Hakuna mbio zingine zinazokaribia London Marathon kwa uchangishaji wa fedha.''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakimbiaji wa kike wanaoshiriki mbio hizo
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zaidi ya rekodi 80 za Guinness World zinalengwa kuvunjwa, ikiwa ni pamoja na mtindo wa mavazi
Haki miliki ya picha PA
Image caption Tabasamu: Watu washangilia mwanzo wa mbio hizo

Kipchoge, Hajawahi kushindwa katika umbali wa zaidi ya maili 26.2 tangu mwaka 2013 katika mashindano ya Berlin Marathon.

Mshindi mara nane David Weir ameshiriki mbio hizo katika kitengo cha kutumia kiti cha magurudumu kwa mwaka wa 20 mfulululizo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sir Mo Farah alishinda Half marathon mjini London mwezi uliyopita
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakenya Vivian Cheruiyot ma Mary Keitany

Ukweli kuhusu mbio za London Marathon

  • Watu 444,168 wamejiandikisha kuchangia mbio za mwaka huu idadi ambayo ni zaidi 7.3% ikilinganishwa na mwaka jana.
  • 44% ya watu waliyotoa maombi ya kishiriki mbio hizo ni wanawake na nusu ya wakimbiaji hawajawahi kushiriki mbio za marathon.
  • Waandaaji wa mbio hizo mwaka huu wanalenga kukusanya jumla ya pauni milioni 3.5
  • Kundi la wanaume linalojiita ''Ever Presents'' limekua likishiriki mbio hizo tangu mwaka 1981

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii