Halima Aden: Mwanamitindo wa kwanza kuvaa burkini na kuonyeshwa katika jarida la Sports Illustrated

Halima Aden in a burkini Haki miliki ya picha Yu Tsai/Sports Illustrated Swimsuit

Mwanamitindo wa Kisomali raia wa Marekani amekuwa mwanamitindo wa kwanza Muislamu kuonyeshwa katika jarida la michezo Sports Illustrated akiwa amevaa burkini.

Halima Aden ameonyeshwa katika jarida la kila mwaka akiwa amevaa nguo hiyo ya kuogelea inayofunika mwili mzima isipokuwa uso viganja vya mikono na miguu.

"Wasichana wadogo wanaovaa hijab wanapaswa kuwa na wanawake wanaowatazamia katika kila sekta," ameiambia BBC.

Halima Aden alilelewa Kenya katika kambi ya wakimbizi , akahamia Marekani akiwa na umri wa miaka 7 na alianza kuvaa hijab muda mfupi baada ya hapo.

"Sasa tunawaona wanasiasa, wafanyabiashara wanawake, waandishi na watangazaji na wanawake wengine katika ufanisi wanaovaa hijab,na huo ndio ujumbe tunaohitaji kuutuma," amesema.

"Kumekuwa na muitikio mzuri na ni heshima kubwa kwangu kwamba Sports Illustrated limechukua fursa hii kuonyesha urembo walio nao wanawake wanaovaa kwa stara."

Haki miliki ya picha Yu Tsai/Sports Illustrated Swimsuit

Sports Illustrated, lililowaonyesha nyota kama Tyra Banks na Beyonce katika ukurasa wake wa juu, ni jarida la Marekani linalosomwa zaidi na wanaume, na kumekuwa na hisia mchanganyiko kufuatia taarifa hii.

Mmoja aliandika katika Twitter: "Iwapo utaendelea kuvaa hijab na uufunike mwili wako- iwapo ukidhani ni sheria ya dini yetu au kwasababau unataka kuvaa mavazi ya stara - inakwenda kinyume kwa kupiga pozi linaloamsha hisia katika jarida linalofahamika kuwachukulia wanawaka kama vitu.."

Mwingine aliandika:"Ningeelewa iwapo ingelikuwa ni maonyesho ya kununua mavazi ya kuogolea kwa wanawake. Lakini kwa jarida lililonuiliwa wanaume, inakwenda kinyume kabisa na malengo ya hijab."

Huenda ukavutiwa na hizi pia:

Katika Instagram maoni yalikuwa tofuati kidogo wakati Halima akionekana kutiwa moyo zaidi: "Nafurahia kuona namna jarida hili linavyojumuisha watu wa tabaka mbali mbali kila mwaka . Mwaka huu ni kiwango kipya."

Ujumbe mwingine: "Kuvuka mipaka baby!"

Haki miliki ya picha Allure
Image caption Mnamo 2017 Halima Aden alikuwa mwanamitindo wa kwanza anayevaa hijab kuonekana kwenye ukurasa wa kanza wa jarida kubwa nchini Marekani

Katika mahojiano na BBC mnamo 2017 mwanamitindo huyo ameeleza kwamba hijabu yake ni "taji" na akaeleza namna wabunifu mitindo walivyokuwa wakichukulia haki ya mwanamke kuchagua anachotaka: " Inashangaza kwamba hatujaona mwanamitindo anayevaa hijab, linapaswa kuwa jambo la kawaida, haipaswi kuwa ni tofauti na wanamitindo wengine wote."

Mwaka huo huo alikuwa alikuwa mwanamitindo wa kwanza anayevaa hijab kuonekana kwenye ukurasa wa kanza wa jarida kubwa nchini Marekani.

Vazi la burkini awali lilibuniwa na Aheda Zanetti, raia wa Australia muislamu. Bi Zanetti amesema dhamira ilikuwa ni kuwaruhusu wanawake wa kiislamu kuweza kwenda kujivinjari katika fukwe za bahari kama wanawake wengine.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption 'Burkini' zimevaliwa na waokoaji maisha baharini Australia

Lakini vazi hilo la burkini linasalia kuzusha mzozo hususan nchini Ufaransa ambako maafisa katika baadhi ya miji wamependekeza lipigwe marufuku, wakieleza kwamba linakiuka sheria zisizo za kidini.

Akijibu tuhuma hizo nchini Ufaransa, Bi Zanetti ameuliza: "Wanajaribu kudhibiti nini? kwanini hawajawapa haki ya kwenda kuishi maisha ya kawaida?" amesema.

"Ninapaswa kuwashukuru watu hao walio na maoni pasi kusikiliza wanachotaka wanawake, ambacho ni uhuru wa kuamua."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii