Caster Semenya ameshindwa kesi ya rufaa dhidi ya sheria mpya za IAAF juu ya viwango vya homoni

Caster Semenya Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Caster Semenya alishinda taji la mbio za Olyimpiki mita 800 mara mbili na la dunia mara tatu a

Caster Semenya ameshindwa katika kesi muhimu dhidi ya shirikisho la riadha duniani, hii ikimaanisha kuwa shirika hilo litaruhusiwa kudhibiti viwango vya homoni za wanariadha wa kike

Mahakama ya utatuzi wa migogoro michezoni Cas) imekataa kesi ya Afrika kusini ya kupinga sheria mpya za IAAF.

Lakini Cas ilisema kuwa ilikuwa na "hofu kubwa juu ya utekelezwaji wa baadaye'' wa sheria hizo mpya.

Semenya, mwenye umri wa miaka 28, alisema sheria hizo'' si za haki " na kwamba alitaka "kukimbia kama nilivyo , jinsi nilivyozaliwa ".

Awali wakati wa kesi yake ya riufaa Semenya aliytuma picha hii kwenye ukurasa wake wa Twitter akiwa pamoja na mawakili wake:

Sasa mshindi huyo wa Olympiki, dunia na mashindano ya jumuiya ya madola kwa mita 800 pamoja na wanariadha wengine wenye jinsia zaidi ya moja (DSD) - watalazimika kupata matibabu ili kkushiriki mashindano ya kuanzia mbio za mita 400 hadi maili, au wabadili mbio.

Cas ilibaini kuwa sheria zilizokuwepo za wanariadha wenye DSD zilikuwa ni za kibaguzi -lakini kwamba ubaguzi huo ulikuwa "muhimu, wa kueleweka na wa uwiano kwa ajili ya kulinda maadili ya wanariadha wanawake ".

Hata hivyo , Cas ilielezea hofu kubwa juu ya ya utekelezwaji wa sheria ikiwqemo mkiwemo:

  • Hofu kwamba wanariadha wanaweza kukiuka masharti ya viwango vya homoni za kike vilivyowekwa na IAAF;
  • Maswali kuhusu faida za viwango vya juu homoni za jinsia tofauti wanazozipata wakimbiaji wa mita 1500 na maili.
  • Utekelezaji wa wanariadha wa sheria hizo mpya

Cas imeitaka IAAF kuangalia uwezedkano wa kuchelewesha utekelezwaji wa sheria hizo kwa wanariadha wanaokimbia katika matukio ya mita 1500 na maili moja hadi pale ushahidi utakapopatikana.

Haki miliki ya picha Getty Images

Semenya hatatakiwa kupunguza viwango vyake vya homoni za (testosterone) kama alikamilisha hilokatika mbio za Diamond Ligi mjini Doha Ijumaa.

Katika ujumbe wake wa Twitter kufuatia uamjuzi wa Cas Semenya amesema kuwa ''Wakati mwingine ni bora kujibu kwakutojibu lolote''

Haki miliki ya picha Twitter/Caster Semenya
Image caption Caster Semenya posted this image on Twitter following the Cas decision

Caster Semenya ni nani?

Caster Semenya ni mojawapo wa nyota maarufu katika riadha.

Mshindi mara mbili wa dhahabru katika mahsindano ya olimpiki na bingwa wa mara tatu wa dunia katika mbio za mita 800, mwanariadha huyo raia wa Afrika ksuinimwenye miaka 28 ameshinda mbio 29 katika umbali huo.

Hatahivyo tangu kuchipuka kwake, kufuatia ushindi wa dunia mnamo 2009, jinsia yake, na manufaa ya utofauti wa bayolojia mwilini mwake umekuwa ukichunguzwa.

Matokeo ya utafiti wa jinsia uliofanywa miaka 10 iliopita bado hayajatangazwa hadharani, licha ya kwamba vyombo vya habari vimetuhumu kwamba ana sifa za kike na kiume ikiwemo kiwango kikubwa cha homoni za kiume testosterone.

Shirikisho la riadha duniani IAAF lilipendekeza sheria kuzuia viwango vya homoni hiyo ya testosterone inayoruhusiwa kwa wanariadha wanawake katika masindano ya 400m na maili. Semenya alipinga uamuzi huo mahakamani ya kutatua mizozo katika michezo.

Nini matatizo ya kijinsia (DSD)?

Wanariadha walio na DSD - hali inayowafanya kukuwa pasipo viwango vya kawaida vya homoni kwa jinisa zao.

Homoni, jeni, na sehemu zao za siri huenda vimechanganyika kwa sifa za kike na kiume.

Neno 'tatizo' linapingwa huku baadhi ya walioathirika wakipendelea kutumia "watu walio na jinsia mbili" na kuitaja kuwa hali ya "kuwana tofuati katika kukuwa kijinsia".

Nini hufanyika baada ya kutambuliwa?

Watu wengi walio na hali hii hushia kuwa na jinsia waliochaguliwa walipo zaliwa. hatahiyvo, wengine wanaohisi kwmaba jinsia waliochaguliwa haimbatani na namana wanavyojihisi , huamua kubadili jinisa zao.

Waathiriwa wa hali hii huenda wakapoteza uwezo wa kuzaa na wanahitaji matibabu ya homoni na ushauri nasaha kuwasaidia kukabiliana na hali walio nayo.

Ni kwanini kesi hii ni muhimu?

Haki miliki ya picha Getty Images

Kwa miaka mingi michezo imegawanyika katika kitengo cha wanaume na wanawake, lakini kesi ya Semenya na sayansi iliyojitokeza inaonyesha kwamba kuna tofauti inayoweza kuwepo.

Imependekezwa kwamba iwapo IAAF itashindwakatika kesi hiyo, huenda kukaidhinishwa kitengo cha 'wazi' ambapo kimsingi wanaume na wanawake wataweza kushindana pamoja na kitengo kitakacho ruhusiwa kutokana na vipimo vya homoni kwa mwanariadha na sio jinsia zao.

Semenya iwapo atapoteza kesi hii je ni nini kitakachofuatia?

Mwanasayansi mashuhuri wamichezo amependekeza atapungua kasi kwa kati ya sekundi tano mpaka saba hivi katika mashindano ya mbio za 800m akipunguza kiwango cha homoni ya testosterone kama ilivyopendekezwa.

Anaweza kuishia kukimbia mbio za masafa marefu. Amewai kukimbia mbio za 5,000m mara mbili msimu huu, na akashinda kila wakati.

Sheria inasemaje?

Wanariadha wanawake wanaotaka kushindana wanalazimika kupata dawa kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kuingia mashindanoni, na kuhakikisha kuwa kiwango cha homoni hizo kinashuka.

Ikiwa mwanariadha wa kike hatataka kutumia dawa, wanaweza kushindana kwenye:

  • Mashindano yeyote ya kimataifa isipokuwa mbio za mita 400 na maili moja
  • Michuano yeyote ambayo sio ya kimataifa
  • michuano ya wanaume katika ngazi yeyote
  • michuano inayohusisha watu wenye jinsia mbili
  • Wanaotaka kushiriki michuano hawatakiwi kufanyiwa upasuaji .
  • Taarifa ya IAAF imesema sheria hizo ''hazina lengo la kuwahukumu au kuhoji jinsia ya mwanariadha''.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii