Champions League na Europa League: Ni klabu gani ya Uingereza itakayofuzu kushiriki makombe ya Ulaya msimu ujao?

Son Heung-min, Mohamed Salah, Eden Hazard na Pierri-Emerick Aubameyang Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tottenham, Liverpool, Chelsea na Arsenal zitawakilisha Uingereza na Ulaya katika fainali ya msimu huu

Mataji ya Champions League na Europa League yatawaniwa na vilabu vinne vya Uingereza kwa mara ya kwanza katka historia.

Liverpool na Tottenham zinakutana katika fainali ya mjini Madrid mnamo tarehe mosi , huku Chelsea na Arsenal zikishiriki katika fainali nyengine ya Europa League mjini Baku siku ya Jumatano tarehe 29 mwezi Mei.

Huku washindi wa michuano yote miwili wakiingia katika ligi ya mabingwa je hatua hiyo inamaanisha nini kwa nafasi ambazo zinawaniwaili timu kufuzu. BBC Sport inaangazia.

Ni klabu gani zinazofuzu Ulaya kama kawaida?

Timu nne bora katika ligi ya Uingereza hufuzu kwa ligi ya mabingwa , huku washindi wa FA , Carabao Cup na namba tano katika jedwali la ligi ya Uingereza hufuzu kushiriki katika Europa Leage.

Iwapo washindi wa mataji hayo mawili wanamaliza katika nne bora , nafasi zao zinawaendea wale waliopo katika nafasi ya sita na saba katika ligi.

Lakini washindi wa ligi ya mabingwa na wale wa Europa league-wote wanatoka Uingereza- na wote wanafuzu. Hivyobasi kutatokea nini?

Je Uingereza itapata nafasi moja ya ziada kwa ligi ya mabingwa?

Uingereza itapewa nafasi ya timu ya tano katika ligi ya mabingwa iwapo klabu moja ambayo imemaliza nje ya nne bora itashinda mojawapo ya michuano hiyo.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itamaliza ya tano ama sita iwapo Man United itawapiku siku ya mwisho ya michuano ya ligi ya Uingereza.

Arsenal iko pointi tatu na magoli manane nyuma ya Tottenham huku ikiwa imesalia mechi moja.

Hiyo itamaanisha kwamba wanahitaji kushinda kombe la Europa league ili kuweza kufuzu katika ligi ya mabingwa .

Iwapo Tottenham itamaliza ya tano, basi kikosi hicho cha Mauricio Pochettino kitahitaji kushinda kombe la ligi ya mabingwa .

La sivyo nafasi ya tano inamaanisha kwamba nafasi ya kushiriki katika kombe la Europa msimu ujao.

Je itakuwaje iwapo timu moja itashinda mataji yote mawili na kumaliza ndani ya nne bora?

Haki miliki ya picha .

Liverpool na Chelsea zina hakika ya kuwa ndani ya nne bora huku Tottenham ikitarajiwa kupata nafasi yake siku ya Jumapili.

Iwapo timu yoyote kati ya hizo zitashinda michuano yao , nafasi zao katika ligi ya mabingwa hazitaisaidia timu nyengine iliopo nje ya nne bora.

Hivyobasi Arsenal haiwezi kumaliza katika nafasi ya tano , ishindwe katika kombe la Europa na kufuzu katika ligi ya mabingwa.

Kitakachofanyika katika nafasi yake kitakushangaza.

Iwapo Chelsea itashinda kombe la Europa , inamaanisha kwamba mabingwa wa Australia Red Bull Salzburg wataelekea moja kwa moja katika awamu ya kimakundi badala ya kufuzu.

Hii ni kwa sababu ligi ya Bundesliga nchini Austria ikiwa katika nafasi ya 11 ni ligi kuu isio na klabu isioweza kufuzu moja kwa moja katika ligi ya mabingwa.

Tuseme Spurs itafanikiwa kusalia katika nne bora , basi iwapo watashinda kombe la mabingwa timu iliopo katika nafasi ya tatu nchini Ufaransa ambayo ni Lyon ama Saint-Ettiene itaingia katika awamu ya kimakundi badala ya kufuzu moja kwa moja.

Ligi ya Ufaransa ndio ligi inayoorodheshwa juu , ikiwa katika nafasi ya tano kuwa timu ambayo itafuzu.

JeChelsea inaweza kuinyima Arsenal nafasi?

Ni kweli Chelsea inaweza kuinyima Arsenal nafasi ya kufuzu kwa ligi ya mabingwa mara mbili kupitia ligi ya uingereza na Europa League iwapo Arsenal haitamailaza ndani ya timu nne bora.

Kikosi cha Maurizio Sarri kimejiwekea nafasi yao ya ligi kitu kinachomaanisha kwamba wanacheza ligi ya Yuropa kwa lengo la kushinda taji pekee.

Iwapo watashinda , bado watasalia katika ligi ya mabingwa na Arsenal kukosa kushiriki.

Iwapo Arsenal itashinda wote watashiriki katika kombe la mabingwa msimu uajo.

Lakini je Arsenal nao wana fursa ya kushiriki katika kombe la Europa, kweli?

Hapana.

Timu zitakazo maliza katika nafasi ya tano iwapo zitashinda mojawapo wa mashindamno hayo na nafasi ya sita watafuzu kushiriki ligi ya Europa pamoja na washindi wa kombe la FA.

Timu hizo zinaweza kuwa Arsenal au Manchester United .

Iwapo Manchester City itashinda kombe la FA, halafu baadaye timu iliopo katika nafasi ya 7 -Wolves -itashiriki katika ligi ya ya Europa katika raundi ya pili ya muondoano mnamo tarehe 25 mwezi Julai.

Lakini iwapo Watford itashinda FA , timu hiyo itaenda moja kwa moja katika awamu ya kimakundi huku timu iliopo katika nafasi ya sita katika ligi ikifuzu.

Hiyo inamaanisha kwamba Arsenal ama United , mkondo wao wa kwanza utahitilifiana na mipango yao ya maandalizi ughaibuni.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii