Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 12.05.2019: Guardiola, Gueye, Hudson-Odoi, Ozil, Bale, Fernandes, Richarlison

Josep Guardiola applauds Haki miliki ya picha Getty Images

Pep Guadiola amewahakikishia Manchester City kuwa hana mpango wa wa kuacha kazi katika klabu hiyo kwa miaka miwili licha ya tetesi kuwa huenda akajiunga na Juventus msimu huu wa joto.(Express)

Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Everton Idrissa Gueye,29. Everton inata karibu paunimilioni 40 kumuuza kiungo huyo wa kimataifa wa Senegal. (Mail)

Buyern Munich bado wanamtaka winga wa Chelsea na kiungo wa kimataifa wa England Callum Hudson-Odoi,18 (Build- kwa Kijerumani)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Callum Hudson-Odoi

Mesut Ozil, 30, hataondoka Arsenal msimu huu wa joto. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani atasalia Gunners hadi mkataba wake utakapokamilika.(Mirror)

Tottenham wanatahmini uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa kimataifa wa Ureno na Benfica Gedson Fenandes,20. (Mirror)

Klabu ya Nice inayoshiriki League 1 inapania kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Olivier Girroud,32, msimu ujao, kwa mujibu wamkurugenzi wa kiufundi wa Gilles Grimandi.(Canal Footbal Club via Bleacher Report)

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Antoine Griezmann na Olivier Giroud

Tottenham wanatahmini uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa kimataifa wa Ureno na Benfica Gedson Fenandes,20. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Leister City mbelgiji YouriTielemans,22, anatarajiwa kurejea Monaaco baada ya uhamisho wake wa Foxes utakapomalizika (VTM Nieuws-kwa kidachi)

Vilabu vya Paris st-Germain na Atletico Madrid vinataka kumnunua msambuliaji wa Everton na kiungo wa Kimataifa wa Brazil Richarlison,22, ambaye bei yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 70. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Richarlison

Everton wameanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu uhamisho wa kudumu wa wa kungo wa kati wa Ureno Andre Gomes,25, anayechezea klabu hiyo kwa mkopo(LiverpoolEcho)

Southhampton wanapanga uhamisho wa pauni milioni 30 wa mshambuliaji wa Fulham na SerbiaAlesandar Mitrovic, 24.(Express)

Kumekua na mvutano mkubwa kati ya mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale na meneja Zinadine Zidane, kumaanisha kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Wales hana maisha katika klabu hiyo.(AS-in Spanish)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Bale

Everton na Tottenham wanatafakari uwezekano wa uhamisho wa kubadilishana wachezaji utakaohusisha mabeki wa kushoto Lucas Digne na Danny Rose.

Hatahivyo Spurs wanasemekana kuwa wakotayari kujadili mkataba huo iki a Rose atakyepo.(Star)

Inter Milan wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Barcelona Mcroatia Ivan Ractic,31, kwa kima cha euro milioni 50. ( Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ivan Rakitic (Kushoto)

Barcelona wanakaribia kufikia mkataba wa kumsajili mlinzi wa Ajax Mdachi Matthis de Ligt,19, na pia wanataka kumsainiDonny van Beek,22. (Mundo Deportivo- kwa kihispania)

Tetesi Bora Jumamosi

Mshambuliaji wa Chelsea Ubelgiji Eden Hazard, 28, yuko katika harakati ya kukubali masharti mapya na Real Madrid kuhusiana na uhamisho mwisho wa msimu huu . (Independent)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden hazard

Manchester United ilikosa fursa muhimu ya kumsaini nahodha wa klabu ya Ajax na uholanzi Matthijs de Ligt, 19, kwa kuwa iliambiwa kwamba mchezaji huyo atakjuwa mnene kupitia kiasi. (Mirror)

Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 19, atasalia katika klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund mwisho wa msimu huu na kupinga kurudi katika ligi ya Uingereza. (Sun)

Uhamisho wa kiungo wa kati wa Man Utd na Ufaransa Paul Pogba kuelekea Real Madrid huenda usifanyike , baada ya ajneti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 Mino Raiola kupigwa marafuku ya miezi mitatu kutowakilisha wachezaji. (Talksport)

Beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire huenda akaichezea klabu yake mechi yake ya mwisho siku ya Jumapili. Tottenham, Arsenal, Chelsea na Manchester United wote wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 , lakini Leicester hawatamuuza kwa dau la chini ya £60m. (Sun)

Manchester United ilikosa fursa muhimu ya kumsaini nahodha wa klabu ya Ajax na uholanzi Matthijs de Ligt, 19, kwa kuwa iliambiwa kwamba mchezaji huyo atakjuwa mnene kupitia kiasi. (Mirror)

Tetesi Bora Ijumaa

Kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard anataka kuhamia Real Madrid haraka iwezekanavyo , lakini Chelsea haiko tayari kumuuza mchezaji huyoi wa ubelgiji mwenye umri wa miaka 28 chini ya dau la £100m. (ESPN)

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Eden Hazard (wa kati)

Manchester United italazimika kulipa Yuro100m iwapo wanataka kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho. Mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 ni miongoni mwa mwachezaji 10 ambao wanatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu . (AS - in Spanish)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii