Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 14.05.2019: Hazard, Man City, Loftus-Cheek, Griezmann, Sessegnon, Koulibaly, Tielemans, Werner

Eden Hazard mwenye umri wa miaka 28- amekamilisha mkatataba wake wa pauni £86m na Real Madrid Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard mwenye umri wa miaka 28- amekamilisha mkatataba wake wa pauni £86m na Real Madrid

Mshambuliaji wa safu ya kati wa Chelsea Mbelgiji Eden Hazard mwenye umri wa miaka 28- atakamilisha mkataba wake wa pauni £86m na Real Madrid baada ya fainali ya ligi ya Europa. (L'Equipe - in French)

Wapelelezi wa Uefa watapendekeza Manchester City iwekewe marufuku ya Championi Ligi kwa walau mwaka mmoja kutokana na tuhuma kuwa klabu hiyo iliwapotosha maafisa wa masuala ya fedha wa soka ya Ulaya . (New York Times)

Haki miliki ya picha Getty Images

Na washindi wa Ligi ya Primia City wanapanga kutumia £200m msimu unaoanza kutokana na hofu kuwekewa marufuku ya kuwahamisha wachezaji. (Mail)

Kiungo wa kati wa England Ruben Loftus-Cheek, mwenye umri wa miaka 23, atasaini mkataba mpya katika klabu ya Chelsea ikiwa tu atapewa hakikisho la nafasi katika kikosi cha kwanza. (sun)

Atletico Madrid watafanya mkutano na mshambuliaji wa ufaransa Antoine Griezmann wiki hii, huku klabu hiyo ikiwa na wasi wasi kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28tayari amekubali kujiunga na Barcelona. (Cadena Ser - in Spanish)

Tottenham wanakamilisha mkataba wa thamani ya £25m kwa ajili ya mchezaji wa safu ya nyuma- kushoto wa timu ya England ya Fulham Ryan Sessegnon mwenye umri wa miaka . (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester United wanamlenga mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, mwenye umri wa miaka 27, msimu huu. (Mirror)

Na United pia wanapanga kutumia £45m kwa mshambuliaji wa Ivory Coast anayechezea kikozi cha Lille r Nicolas Pepe, mwenye umri wa miaka 23. (Mirror)

Meneja wa Leicester Brendan Rodgers ameiambia klabu hiyo iharakishe kusaini mkataba na wa kudumu na kiungo wa kati Mbelgiji Youri Tielemans mwenye umri wa miaka 22, anayechezea kikosi cha Monaco kwa sasa ambaye thamani yake ni £40m . (Star)

Wachezaji wa Foxes wamekuwa wakimuambia Tielemans jinsi wanavyomtaka aendelee ku bakia kikosini kwa matumaini ya kuongeza matumaini ya klabu hiyo kusaoini mkataba nae. (Leicester Mercury)

Manchester City wanadau ambalo limekataliwa kwa ajili ya mchezaji wa Ufaransa anayecheza safu ya kati Tanguy Ndombele Lyon mwenye umri wa miaka 22 . (Le 10 Sport, via Manchester Evening News)

Mkurugenzi mkuu wa RB Leipzig' anasema Liverpool bado inaweza kusaini mkataba mshambuliaji mjerumani Timo Werner mwenye umri wa miaka 23 huku klabu ikiwa bado haijafanya mazungumzo na Bayern Munich. (Bulinews, via Liverpool Echo)

Barcelona inatarajia kupokea dau kutoka kwa Chelsea kwa ajili ya kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 26, kama marufuku iliyowekewa Klabu hiyo ya Ligi ya Primia itacheleweshwa. (Goal)

Mjerumani anayechezea klabu ya Arsenal safu ya kati Mesut Ozil, mwenye umri wa miaka 30,anasema hana nia ya kuihama klabu hiyo. (Dazn Dach, via Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images

Everton wamepewa fursa ya kusaini mkataba na kiungo wa kati Mreno Joao Mario kutoka Inter Milan kwa £15m mwenye umri wa miaka 26 (Mail)

Meneja wa Toffees Marco Silva ameiambia klabu kuwa ni muhimu wafanye mikataba ya mikopo na wachezaji wa safu ya ulinzi ya Chelsea Kurt Zouma, 24, na kiungo wa kati wa Barcelona Andre Gomes, mwenye umri wa miaka 25,mkataba wa kudumu.(Liverpool Echo)

Real Madrid imemuambia mlindalango kutoka Costa Rica Keylor Navas, mwenye umri wa miaka 32, kwamba hayuko katika mipango yao ya msimu ujao (Marca)

Mcroasia Filip Benkovic, mwenye umri wa miaka 21 anayechezea klabu ya England ya Leicester, yuko tayari kucheza msimu mwingine katika klabu hiyokwa mkopo. (Leicester Mercury)

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 28, anasema kuwa amaifahamisha klabu hiyo kuhusu amuzi wake wa kuhamia Real Madrid. (Daily Mail)

Blues pia wanataka kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 26, ikiwa rufaa waliowasilisha kwa shirikisho la FIFA dhidi kupinga marufuku ya usajili wa wachezaji itapita msimu huu. (Cadena Ser via Daily Mail)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Eden Hazard

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amefutilia mbali mkutano wa mwisho wa msimu kwasababu alikuwa amekasirika baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0 na Cardiff siku ya Jumapili. (The Sun)

Kiungo wa kati United Paul Pogba, 26, alirushiana maneno na mashabiki baada ya wao kusema kuwa anastahili kuuzwa baada ya kushindwa na Cardiff. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 27, anasema kuwa alishangazwa na tetesi zinazodai kuwa atahamia Barcelona. (Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexandre Lacazette

Meneja wa Everton Marco Silva anasema kuwa hana uhakika ikiwa klabu hiyo itashinda kinyan'ganyiro cha kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes, 25, msimu ujao. (Liverpool Echo)

Kocha wa klabu ya Newcastle Rafael Benitez, 59, atafanya mkutano wa dharura na mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley wiki ijayo ili kujadili hatma yake ya baadae. (Daily Mail)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii