Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 15.05.2019: Sane, Griezmann, Pogba, Hazard, Martial, Bale, Sanchez

Winga wa Manchester City, Leroy Sane Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Leroy Sane,Winga wa Manchester City

Bayern Munich wameanza mazungumzo na Manchester City kuhusu uhamisho wa winga wa miaka 23 wa Ujerumani Leroy Sane. (Daily Record)

Barcelona wameamua kumsajili mshambuliaji Antoine Griezmann ambaye ametangaza kuondoka kwake Atletico Madrid msimu huu wa joto.

Hii ni baada ya klabu hiyo ya Uhispania kuondolewa katika kinyang'anyiro cha ubingwa wa Ulaya na Liverpool(Marca)

Real Madrid wameonesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26, huku United ikiwa tayari kumuuza mchezaji huyo kwa pauni milioni 150. (Independent)

Licha ya tetesi kuwa Real Madrid wamekubali makataba wa pauni milioni £86 kumnunua Eden Hazard, 28, Chealsea bado wanashikilia kuwa hatamuachilia kiungo huyo hadi walipwe pauni milioni 100.(Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard

Hazard ameambia vyombo vya habari kuwa aliamua kuingilia kat i suala hilo na kwamba atajaribu kuishawishi Chelsea kuafikiana na Real kuhusu uhamisho. (Express)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ametishia kuuza nusu ya kikosi chake baada ya kushindwa na Cardiff. (Sun)

Mshambuliaji wa Wales, Gareth Bale, 29, huenda asirejea Tottenham kwasababu hana haraka ya kuondoka Real Madrid, kwasababu amesalia na miaka mitatu katika mkataba wake wa £600,000-kwa wiki. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Bale

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 23, hatauzwa na Manchester United msimu huu kwasababu amemvutia mmoja wa mwenyekiti mwenza Joel Glazer. (ESPN)

Everton wanatafakatri uwezekano wa kumtuma mlinzi wa England wa chini ya miaka 21 Jonjoe Kenny, 22, kwa mkopo msimu ujao, huku Seamus Coleman akitarajiwa kuwa beki wa kulia na safu ya nyuma. (Liverpool Echo)

Manchester United huenda wakatumia pauni £12m kumruhusu mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez ajiunge na Inter Milan kwa mkopo msomaji ujao. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexis Sanchez

Leicester wanajaribu mpango wa kumrudisha kiungo wa kati wa 22 Mbelgiji Youri Tielemans amabe yuko Monaco kwa mkopo, kwasababu Manchester United na Tottenham wameonesha nia ya kutaka kumnua. (Sky Sports)

Barcelona wanataka kumuuza kiungo mkabaji wa kati Philippe Coutinho, 26, msimu huu wa joto lakini hawatamuachilia aondoke kwa kitita cha euro milioni 100 sawa na (£86.8m). (Sport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kalidou Koulibably (kati kati)

Manchester United wamerudi nyuma katika mpango wao wa kumnunua Kalidou Koulibably, 27,baada ya kuitisha pauni £90.(Independent)

Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City wana mpango wa kuwanunua walau wachezaji watatu wapya msimu huu wa joto, huku wakilenga zaidi mlinzi wa safu ya kati na mashambuliaji. (ESPN)

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne

Mshambuliaji wa safu ya kati wa Chelsea Mbelgiji Eden Hazard mwenye umri wa miaka 28- atakamilisha mkataba wake wa pauni £86m na Real Madrid baada ya fainali ya ligi ya Europa. (L'Equipe - in French)

Blues pia wanataka kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 26, ikiwa rufaa waliowasilisha kwa shirikisho la FIFA dhidi kupinga marufuku ya usajili wa wachezaji itapita msimu huu. (Cadena Ser via Daily Mail)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Eden Hazard

Atletico Madrid watafanya mkutano na mshambuliaji wa ufaransa Antoine Griezmann wiki hii, huku klabu hiyo ikiwa na wasi wasi kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28tayari amekubali kujiunga na Barcelona. (Cadena Ser - in Spanish)

Tottenham wanakamilisha mkataba wa thamani ya £25m kwa ajili ya mchezaji wa safu ya nyuma- kushoto wa timu ya England ya Fulham Ryan Sessegnon mwenye umri wa miaka. (Mail)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii