Manchester City huenda ikapigwa marufuku kushiriki katika ligi ya mabingwa kwa msimu mmoja

Manchester City Haki miliki ya picha AFP
Image caption Manchester City ilishinda ligi ya Uingereza mara nne katika misimu minane siku ya Jumapili

Wachunguzi wa Uefa wanataka Manchester City kupigwa marufuku kushiriki katika kombe la ligi ya mabingwa kwa msimu mmoja iwapo watapatikana na hatia ya kuvunja sheria ya kifedha. hatahivyo kulingana na duru muhimu , uamuzi wa mwisho haujafanywa na mchunguzi mkuu Yves Leterme.

Waziri mkuu wa zamani nchini Ubelgiji, mwenyekiti wa jopo la wachunguzi wa shirikisho la soka la Uefa anatarajiwa kufanya mapendekezo wiki hii.

Huku kukiwa hakuna kura inayopigwa kutoa uamuzi katika kisa kama hicho , uamuzi wa mwisho unatoka kwake lakini wenzake wanaaaminika kutoa msimamo wao katika mkutano wa hivi karibuni kwamba marufuku ya msimu mmoja inatosha.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Manchester City ilishindwa na Tottenham katika kombe la ligi ya mabingwa msimu huu na hawajapita nusu fainali

Je Manchester City imefanya nini na je klabu hiyo imeadhibiwa?

Leterme na kundi lake wamekuwa wakiangazia ushahidi uliopatikana katika misururu ya siri zilizovuja na kuchapishwa katika gazeti la Ujerumani la Der Spiegel mwaka uliopita.

Ripoti hiyo inadai kwamba Manchester City ilikiuka sheria ya kifedha ya Fifa kwa kuongeza thamani ya ufadhili wa mamilioni wa pauni.

City ilipigwa faini ya £49m mwaka 2014 kwa kukiuka sheria hapo awali.

Mabingwa hao wa ligi ya Uingereza walikana kufanya makosa na Uefa imesema kuwa haiwezi kuzungumzia kuhusu uchunguzi unaondelea, lakini kulingana na gazeti la New York Times, wachunguzi sasa wanataka sheria hiyo kufuatwa na kupigwa marufuku.

Kitengo cha majaji cha Uefa kitalazimika kuamua iwapo kimekubaliana na mapendekezpo yoyote kutoka kwa Leterme -yanayotarajiwa katika kipindi cha saa 48 zijazo-ijapokuwa marufuku hiyo haitaathiri michuano ya msimu ujao kwa sababu City inaweza kukata rufaa ama hata kuipeleka kesi hiyo katika mahakama ya kutatua mizozo katika michezo.

Lakini pia itakuwa pigo kwa klabu ambayo inatumia kila njia kushinda shindano hilo la Ulaya kwa mara ya kwanza, na ambao wanaweza kukabiliwa na marufuku ya uhamisho, huku shirikisho la soka nchini Uingereza FA, Ligi ya Uingereza na Fifa zikichunguza City kuhusu kuwasajili wachezaji wenye umri mdogo.

Mapema msimu huu , taarifa kutoka kwa Manchester City ilisema: Tuhuma kuhusu ukiukaji wa sheria za kifedha ni za uongo.

Manchester City inaunga mkono kuanzishwa kwa uchunguzi wa Uefa kama fursa ya kumaliza uvumi unaotokana na udukuzi wa barua pepe za Manchester City.

Je sheria za uchezaji wa haki zinasemaje?

Uchezaji wa haki kwa kupitia matumizi ya kifedha ulianzishwa na Uefa ili kuzuia klabu katika mashindano kutotumia fedha kupitia kiasi chao ili kukabiliana na kile kinachoidaiwa na rais wa Uefa Michel Platini kuwa matumizi ya dawa za kusisimua misuli katika soka.

Chini ya sheria hizo, hasara za kifedha ni chache na klabu zinahitajika kuafikia mahitaji yote ya uhamisho mbali na malipo ya wachezaji kila mara.

Klabu zinahitajika kusawazisha matumizi ya ya soka -uhamisho na mishahara na runinga pamoja na mapato ya tiketi pamoja na mapato yanayotokana na idara ya kibiashara.

Fedha zinazotumika katika viwanja , vifaa vya mazoezi ,ukuzaji wa vipawa miongoni mwa vijana ama fedha zinazotumika katika miradi ya kijamii haziangaziwi.

Bodi inayodhibiti fedha katika klabu , ilioundwa na Uefa , ina uwezo wa kuzipiga marufuku klabu kutoshiriki katika mashindano ya Uefa ikiwemo adhabu nyengine kama vile onyo, faini, kutolipa fedha za zawadi , kupiga marufuku uhamisho, kupunguza alama, kupiga marufuku usajili wa wachezaji wapya na masharti kuhusu idadi ya wachezaji wapya ambao wanaweza kusajiliwa katika mashindano ya Uefa.

Je kuna klabu ambayo imeadhibiwa?

Mwaka 2014 klabu ya Paris St-Germain inayomilikiwa na Qatar ilipokea adhabu kama hiyo kama ile ambayo City ilipokea.

PSG ilidaiwa kukiuka sheria za FFP wakati bodi inayodhibiti fedha za klabu CFCB ilipoamua kurudisha nyuma kandarasi ya ufadhili ya £167m na mamlaka ya utalii nchini Qatar, ambayo ilifutilia mbali hasara yao iliokuwa na thamani isiokuwa ya sawa.

Hatua hiyo ilimaanisha kwamba timu hiyo ya Ufaransa ilipitisha kiwango cha matumizi ya fedha, wakati sheria za uchezaji wa haki za Uefa zilipokuwa haziruhusu hasara ya hadi £37m katika kipindi cha miaka miwili kilichopita.

Walipokea faini, na waliruhusiwa kusajili wachezaji 21 pekee katika kombe la mabingwa kwa msimu mmoja.

PSG imesalia katika uchunguzi mwaka wa kifedha wa 2017-18 wakati walipomsajili Neymar kutoka Barcelona kwa rekodi ya dau la £222m na Kylian Mbappe kutoka Monaco, aliyekua katika mkopo kwa £180m .

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii