Manchester City yakosolewa kwa kuwakejeli mashabiki wa Liverpool

Wimbo wa manchester City unaonyesha mashabiki wa Liverpool ''wakichapwa katika mitaa" na "kulia " Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wimbo wa manchester City unaonyesha mashabiki wa Liverpool ''wakichapwa katika mitaa" na "kulia "

Manchester City wamekosolewa juu ya video ya wimbo wao iliyoonyesha wachezaji na wahudumu wa timu hiyo wakiungana katika kuimba wimbo wa kejeli wa kusherehekea mashabiki wa Liverpool "wakichapwa mtaani ".

Video hiyo inadhaniwa kuwa ilichukuliwa kutoka kwenye ndege wakati timu hiyo ilipokuwa ikisafiri kutoka kwenye sherehe za ushindi wa Primia Ligi wa 4-1 katika Brighton.

Ushindi huo uliiwezesha the Blues kuichapo Liverpool kwa ushindi mwembaba wa pointi moja.

Manchester City bado haijatoa kauli yoyote juu ya video hiyo.

Haijabainika wazi ni wachezaji wala wahudumu gani wa klabu hiyo walishiriki katika wimbo huo, ambao unakumbusha kushindwa kwa Liverpool katika fainali ya Championi Ligi mjini Kiev.

Wimbo huo unaelezea jinsi mashabiki wa Liverpool ''walivyochapwa katika mitaa" na "kulia " na wimbo huo unaelezea pia kuwa mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah alijeruhiwa - lakini pia ikielezea kuwa aliumizwa na Vincent Kompany.

Hata hivyo, waliojiunga kuimba wimbo huo walisikika kwenye kibwagizo tu cha wimbo wakiimba "Allez, Allez, Allez"

" Kusema ukweli ni jambo la aibu kwamba baadhi ya mashabiki wa Man City wanafikiri ni SAWA kwa wachezaji wao kuimba juu ya kupigwa kwa mashabiki ," alisema kupitia ujumbe wa Tweeter mmoja wa mashabiki wa Liverpool, huku wengi zaidi wakijibu kuwa video ilikuwa "si ya thamani", "isiyokuwa ya kitaaluma " wala "busara".

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii