Berahino apatikana na hatia ya kuendesha gari akiwa mlevi

Saido Berahino akiwa mahakamani katika mahakama ya hakimu mkazi ya Highbury Corner Haki miliki ya picha PA
Image caption kesi ya Saido Berahino inaendeshwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Highbury Corner

Mchezaji soka Saido Berahino amepatikana na hatia ya kuendesha gari huku akiwa amekunywa pombe.

Mshambuliaji wa Stoke City alikuwa amezidisha takriban mara tatu ya kiwango cha kileo wakati wakati gari lake aina ya Range Rover liliposimamishwa katika eneo la West End jijini London majira ya saa tisa usiku tarehe 18 Februari.

Mahakama ya Highbury Corner ilisikiliza kesi ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 25-ambaye alikamatwa dakika chache baada ya kuibiwa.

Mahakimu walisema''hakuwa na uoga wa kifo wala wa kujeruhiwa vibaya " kabla ya kumpiga faini ya £75,000 na kumzuwia kuendesha gari kwa kipindi cha miezi 30.

mahakama iliambiwa kuwa "hapakuwa na mzozo " juu ya wizi , ulionaswa na kamera za CCTV, lakini wakili wa Berahino Garry Green alidai kuwa muhimu katika kesi ilikuwa ni "ikiwa mteja ilikuwa ni muhimu kwa mteja kuendesha gari lake au la ".

Jaji mkuu Mark Oxenham alisema kuwa rafiki wa kike wa Berahino alikuwa meendesha gari hilo kabla na "angeweza kuendelea na safari kutoka kwenye eneo la tukio ".

Mahakama iliambiwa kuwa mchezaji huyo wa kimataoifa wa Burundi awali alipatikana na hatia ya kuendesha akiwa amelewa mnamo mwaka 2015 na ya kuwa mmiliki wa gari lililoendeshwa na mlevi being mwaka 2012.

Katika usiku alipokamatwa, polisi waliitwa kutokana na ripoti ya uwezekano wa tukio la kudungwa kisu kwa watu saba nje ya mgahawa wa VQ Cafe, katika mtaa wa Great Russell.

Berahino,ambaye ni mkaazi wa Old Penkridge Road, Staffordshire alikuwa anaendesha gari ya Range Rover wakati polisi walipolisimamisha katika eneo la Bedford Square.

Aliulizwa kuhusu mapigano, lakini hakuwa ameona chochote, alisema mwendesha mashtaka Katie Weiss.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Berahino ambaye ni mzaliwa wa Burundiatashiriki katika kombe la mataifa ya Afrika - Africa Cup of Nations

Kamishna wa polisi Stephen Luu alisema kuwa dereva alionekana "muoga" na alikuwa " alikuwa anapumua hewa yenye harufu ya pombe.

Berahino alipatikana amekunywa mililita103 za pombe mililita 100 za hewa, iliambiwa mahakama . Kiwango kinachokubalika kisheria ni miligramu 35.

Aliwaambia polisi kuwa aliibiwa, huku rafiki yake wa kike akisema anaamini rafiki yake wa zamani wa kiume alikuwa amepanga Berahino asha,mbuliwe, iliambiwa mahakama.

Saa yake pamoja mikufu miwili ya almasi iliibiwa.

'Inamgarimu kipaji chake'

Mahakama iliambiwa kiuwa Berahino kwa sasa hana kipato, kwasababu amesimamishwa kucheza na Stoke bila malipo na ana gharama za malipo ya £20,000 kila mwezi.

Mzaliwa huyo wa Burundi aloiyejiunga na Stoke kutoka West Brom kwa mkataba wa awali wa £12m mwezi Januari January 2017, anatarajiwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika linaloanza mwezi Juni.

"Nilikuwa naogopa . nilikuwa tu ndio nimeshambuliwa na mpwa wangu alikuwepo pale na nilipaswa kuchukua hatua. ilinibidi niendeshe haraka kutoka eneo la tukio ,"alisema.

"Walikuwa na kisu na bunduki pia ."

Alisema hakuwaarifu polisi mara moja juu ya wizi baada ya kuitwa .

"Siku za nyuma nimekuwa katika vyombo vya habari na sikutaka lolote litangazwe kunihusu ," alisema.

"Ineharibu taaluma yangu nilikuwa naogopa hilo.

"Hicho hi kitu ambacho sikukitaka kabisa."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii