Man City, Liverpool, Chelsea, Spurs, Arsenal, Man Utd: Wafahamu wachezaji nyota wanaolengwa na timu hizi

Jadon Sancho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho huenda akagharimu dau la zaidi ya £100m

Ligi ya Uingereza ya Premia ilifika kilele chake wiki moja iliopita -lakini klabu tayari zimeanza kuangazia msimu ujao wa 2019-20.

Dirisha la uhamisho lilifunguliwa siku ya Alhamisi , 16 mwezi Mei na litaendelea kuwa wazi hadi Agosti.

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekiri kwamba anahitaji wachezaji wapya baada ya kumaliza katika nafasi ya sita wakiwa pointi 32 nyuma ya mabingwa Manchester City.

Ni mapema mno na klabu nyingi zinatazama majina mengi, wachezaji mbadala na mipango bila kusahau kwamba kuna changamoto watakazokabiliana nazo.

Mambo yanaweza kubadilika.

Huu hapa mwelekezo wa jinsi klabu sita bora za EPL zinaweza kufanya mabadiliko.

Manchester City inamsaka mchezaji Rodri

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rodri (kushoto) aliichezea klabu yake ya Atletico Madrid mechi 46 katika mashindano yote msimu huu akifunga magoli mawili.

Malengo yake ni mchezaji atakayecheza namba sita na beki wa kushoto.

Kiungo huyo wa kati wa Uhispania Rodri mwenye umri wa miaka 22, ni miongoni mwa wachezaji anayepigiwa upatu kuchezea safu ya kati ya klabu hiyo.

Lengo la usajili huo ni kumtafuta mrithi wa Fernandinho mwenye umri wa miaka 34. City haitamsajili mchezaji wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes.

Huku hatma ya nahodha Vincent Kompany ikiwa haijulikani , pia wanamtafuta beki wa kati anayecheza kwa mguu wa kushoto.

Mchezaji ambaye City wanamlenga sana ni beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan Bisaka mwenye umri wa miaka 21.

Duru zinaarifu kuwa katika kumsaini mchezaji huyo City huenda ikakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa man United na huku akitaka kusalia mjini London hawezi kukataa wito wa kuelekea kaskazini mwa mji huo.

City pia wameonyesha hamu ya kutaka kumsaini beki wa kushoto wa Leicester Ben Chillwel, 22, na winga wa Fulham mwenye umri wa miaka 18 Ryan Sessegnon.

Kulikuwa na mazungumzo ya kuongeza mkataba wa kiungo wa kati wa Ujerumani IIkay Gundogan, lakini hakuna makubaliano yalioafikiwa.

Na baada ya City kumfuata tena mnamo mwezi January, alitaka kusitisha mazungumzo hadi mwisho wa msimu .

Inaeleweka kwamba anataka kusalia hata iwapo atakamilisha mwaka wake wa mwisho wa kandarasi.

Liverpool inamlenga kinda Rhian Brewster

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jurgen Klopp anampenda sana kinda mshambuliaji Rhian Brewster

Liverpool ndio timu ambayo imejistawisha kati ya timu zote sita baada ya kufanya usajili wa wachezaji wa kutosha hivyobasi hawahitaji wachezaji wengi.

Wanahisi kwamba kuimarisha klabu hiyo italazimika matumizi ya kiwango cha juu cha fedha licha ya kwamba kuna wachezaji mahiri wanaoweza kuingia na kuwa katika kikosi cha kwanza.

Wamiliki wa klabu hiyo Fenway Sports hawataki kutumia fedha vibaya- wanataka kufanya hivyo kwa mipango na ujasiri.

lengo lao ni kufikia kiwango ambacho wanaweza kufanya mabadiliko makubwa wakati wanapohitaji na iwapo fursa hiyo itapatikana.

Kwa sasa uwezo wa kifedha wa kufanya mabadiliko kama hayo haupo.

Wanahisi kwamba wako katika kilele chao kama ilivyokuwa kwa mfano walipomuuza Phillipe Coutinho na kumnunua Virgil van Dijk na Alisson.

Huku Alberto Moreno akidaiwa kutaka kuondoka na Nathaniel Clyne pia akitarajiwa kuondoka, watahitaji mchezaji atakayechukua mahala pao hususan katika safu kushoto.

Mchezaji ambaye anaweza kujiimarisha katika safu hiyo ama hata kucheza katika safu tofauti.

Katika safu ya mshambulizi Daniel Sturridge anatarajiwa kuondoka.

Jurgen Klopp anampenda sana kinda Rhian Brewster hivyobasi hana mpango wa kusajili mshambuliaji nambari tisa mgongoni.

Badala yake Liverpool inaweza kumsajili mshambuliaji anayeweza kucheza mbinu tofauti -mchezaji atakayemwezesha Klopp kuwabadilisha washambuliaji anavyotaka.

Divock Origi anatarajiwa kusalia licha ya kwamba haijulikani iwapo atatia saini mkataba mpya au la. Timu hiyo pia imehusishwa na mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Julian Brandt,

Lakini inadaiwa kwamba uhamisho wa mchezaji huyo wa Ujerumani huenda usifue dafu.

Marufuku ya kuwanunua wachezaji Chelsea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chelsea inaweza kukataa kumuuza nyota wao Eden Hazard

Chelsea Itategemea uamuzi wa marufuku yao ya uhamisho , na kwa sababu ya hilo , hakuna klabu kati ya sita bora inayokabiliwa na chamngomoto kubwa za usajili.

Kuna uwezekano kwamba mahakama ya kutatua mizozo ya michezo huenda isitoe uamuzi wake hadi mwezi Julai - ambapo kitakuwa ni kipindi cha katikati cha dirisha la uhamisho.

Kufuzu kwa Chelsea katika ligi ya mabingwa kumeipatia wakati mgumu . Kuna uwezekano kwamba walikubali marufuku hiyo wakijua kwamba wangecheza katika kombe la Yuropa na kutumia wachezaji ilio nao kwa sasa ili kumaliza msimu.

Lakini kwa sababu sasa wako katika ligi ya klabu bingwa-watahitaji wachezaji wa ziada ili kuwawezesha kushindana katika kiwango hicho ,hivyobasi wamelazimika kukabiliana na mafuruku hiyo kwa hali na mali. Kwa sasa wanahitaji mshambuliaji na winga.

Iwapo marufuku hiyo itaendelea watalazimika kuongeza mkataba wa mshambuliaji Oliver Giroud mbali na kuongeza mkopo wa Gonzalo Higuain.

Michy Batshuayi na Tammy Abraham pia huenda wakarudi katika klabu hiyo.

Tayari mshambualiji nyota Eden hazard analengwa na klabu ya Real Madrid na anataka uhamisho huo kukamilishwa mara moja.

Iwapo marufuku hiyo itafaulu , baadhi wanahisi kwamba huenda Chelsea ikamzuia kuondoka-Hivyobasi watalazimika kukosa dau kubwa la uhamisho la sivyo aondoke bure mwaka mmoja baadaye kwa lengo kwamba iwapo watamzuia huenda akaisaidia pakubwa timu hiyo.

Huku Pedro, Willian na Callum Huson Odoi wakikabiliwa na majeraha, huenda Hazard asiuzwe.

Iwapo marufuku hiyo haitatekelezwa , Blues italazimika kumuuza Hazard na kumnunua Coutinho.

Huku Antoine Griezman akijiunga na Barcelona , lazima mchezaji mmoja atalazimika kuondoka na kuna uwezekano mkubwa kwamba mchezaji huyo atakuwa Coutinho.

Wachezaji wengine wanaolengwa na klabu hiyo ni pamoja na Wilfried Zaha wa Crystal palace.

Mchezaji huyo anataka kuondoka katika klabu hiyo ya Selhurst mwisho wa msimu huu. Tusimsahau mchezaji aliyesajiliwa mapema Christian Pulisic kutoka Borussia Dortmund.

Katika safu ya mashambulizi Edison Cavani na Marco Asensio ni majina ambayo yametajwa .

PSG ina mpango wa kumuuza Cavani , ambaye uhusiano wake na Neymar ni mbaya, huku Asensio huenda akatumiwa na Real Madrid kumnunua Hazard.

Tottenham inataka kumsajili Sessegnon

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tottenham, Manchester United, Paris St-Germain, Juventus, Borussia Dortmund na RB Leipzig zinamwania mchezaji wa Fulham Ryan Sessegnon

Huenda kukafanyika mabadiliko makubwa katika klabu ya Tottenham mwisho wa msimu huu , bila kujali kile kitakachotokea katika fainali ya ligi ya mabingwa.

Wanatafuta wachezaji ambao hawajatia fora katika klabu yoyote-kumbuka Lucas Moura wakati alipokuwa hachezeshwi katika klabu ya PSG, na Malcolm katika klabu ya Barcelona.

Spurs inamtaka Ryan Sessegnon na mhezaji huyo pia anataka kuhamia katika klabu hiyo.

Angesalia katika klabu ya Fulham iwapo wangesalia katika EPL lakini sasa wamekubali uhamisho wake. Hawawezi kumkosa mchezaji huyo msimu ujao.

Tottenham bado haijawasilisha ombi la kutaka kumsajili mchezaji huyo lakini duru zinasema kwamba klabu hiyo inapanga kuwasilisha ombi na sababu itakayozifanya klabu hizo mbili kuketi chini na kukubaliana kuhusu dau la uhamisho.

Wanalenga kumchezesha kiungo huyo katika wingi ya kushoto kabla ya kumrudisha safu ya nyuma ya kushoto kwa muda mrefu.

Klabu ambazo zimekuwa zikimuandama mchezaji huyo ni pamoja na Man United, PSG, Juventus, Borussia Dortmund na RB Leipzig, Chelsea-Lakini kutokana na marufuku inayotarajiwa na swala la ujirani wa London linaleta uhasama mkubwa.

Wakati huohuo kuna uwezekano mkubwa kwamba Mchezaji Christian Eriksen atauzwa mwisho wa msimu huu.

Huku mchezaji huyo wa Denmark akiwa hataki kuongeza kandarasi yake, Spurs haitakubali kumpoteza kupitia uhamisho wa bila malipo mwaka ujao.

Hatahivyo kuna uwezekano kwamba huenda akaanzisha mazungumzo ya kandarasi mpya. Hatahivyo Totteham imekuwa ikiwalenga wachezaji kama vile Jack Grealish wa Aston Villa na Zaha.

Katika safu ya nyuma Spurs ingependa kuwaondoa wachezaji Victor Wanyama pamoja na Eric Dier.

Arsenal inamtafuta mrithi wa Aaron Ramsey

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aaron Ramsey atamaliza ushirikiano wake na Gunners mwisho wa msimu huu baada ya miaka 11

Halitakuwa dirisha zuri la uhamisho kwa upande wa Arsenal . Swala nyeti ni kiwango cha fedha alizopewa mkufunzi Unai Emery Kutumia.

Iwapo klabu hyo itashiriki katika kombe la Yuropa msimu ujao basi fedha watakazopewa ni £40m pekee.

Lakini wapo watashiriki katika ligi ya mabingwa , kitita hicho huenda kikaongezeka na inaaminika kwamba huenda kikafikia dau la £100m.

Huenda pia Adidas ikachangia pakubwa wakati itakapochukua rasmi ufadhili wa timu hiyo.

Malengo ya Arsenal ni kununua mchezaji katika safu ya ulinzi na kiungo wa kati atakayechukua mahala pake Aaron Ramsey anayeeleka Juventus.

Mchezaji wa Getafe Djene Dakonam ambaye yuko katika kandarasi hadi 2021 huenda akawa jibu la tatizo la safu ya kati.

Arsenal ilikaribia kumsajili kiungo wa kati wa PSG Christopher Nkunku mwezi Januari , huku Adrien Rabiot akiwa mchezaji mwengine ambaye wamekuwa wakimlenga katika siku za nyuma.

Lakini huenda Arsenal imetupilia mbali hamu yao ya kuwanunua wachezaji hao.

Danny Welbeck anaondoka na kuna mpango wa kumuuza kwa mkopo mshambuliaji Eddie Nketiah.

Manchester United wnamtaka Koulibaly na Sancho

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kalidou Koulibaly aliichezea napoli mara 47 msimu huu

United inalenga kuwanunua wachezaji tofauti ikiwemo vijana na nyota walio na uzoefu.

Na wanataka kujaza safu za ulinzi , ya kati na wingi. beki wa kwanza anayesakwa ni Kalidou Koulibaly wa Napoli.

Hatahivyo dau la juu la mchezaji huyo huenda likaivunja hamu United.

Koulibali ana umri wa miaka 27 akiwa katika kandarasi hadi 2023 huku klabu yake ikiwa haitaki kumuuza.

Vile vile United pia itashindana na Man City katika kutaka kumsajili beki wa Crystal palace Aaron Wan Bissaka.

Huku katika safu ya kati wakitaka kumsajili Rabiot. Lakini mengi yatategemea kitakachotokea na Paul Pogba. Mchezaji nyota waliyetaka kumsajili ni Jadon Sancho.

Lakini hatua ya United kumaliza katika nafasi ya sita katika ligi ya EPL imebadilisha kila kitu.

Sancho hayuko tayari kukosa soka ya ligi ya mabingwa na iwapo ataondoka anataka kuichezea klabu ambayo ina uthabiti ,maendeleo huku uwezo wa kushinda mataji ukiwepo.

Klabu za PSG, Barcelona na Real Madrid wanamtaka Sancho. United pia iimevutiwa na mchezaji wa Swansea Daniel James.

Mada zinazohusiana

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea