Je itakuwaje Vincent Kompany wa Anderlecht atakapokutana na Mbwana Samatta wa Genk?

Vincent Kompany Haki miliki ya picha Getty Images

Hatua ya nahodha wa klabu ya Manchester City Vincent Kompany kutangaza kuwa anaihama klabu hiyo na badala yake kujiunga na Klabu ya Anderlecht nchni Ubeligiji imewashangaza mashabiki wengi wa klabu hiyo ambao walitarajia kwamba kandarasi ya mchezaji huyo itaongezwa kwa angalau mwaka mmoja.

Hatahivyo cha kufurahisha ni kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye aliichezea Manchester City kwa kipindi cha takriban miaka 11 -minane kati ya hiyo akiwa nahodha wa mabingwa hao atajiunga na klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji sio tu kama mfukunzi wao mpya bali pia mchezaji.

Katika ligi hiyo Kompany anatarajiwa kukutana ana kwa ana na nyota wa Taifa Stars Mtanzania Mbawana Samatta aliyeibuka mshindi wa tuzo la kiatu cha Ebony kwa msimu mzuri akichezea timu yake ya Genk.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ni mfungaji bora mwenza akiwa na magoli 23.

Hatua hiyo inamaanisha kwamba iwapo Genk na Anderlecht zitakutana msimu ujao Waswahili wanasema ni nyasi zitakazoumia kwa kuwa mafahali wawili watakuwa wamekutana.

Huku Samatta akishinda tuzo ya mchezaji mwenye magoli mengi katika ligi hiyo ya Ubelgiji huenda umaarufu huo ukapungua kutokana na kuwasili kwa Vincent Kompany ambaye mbali na kwamba huenda akamzuia mchezaji huyo wa Tanzania kutofunga magoli, pia atakuwa akiifunza timu yake akiwa ndani na nje ya uwanja.

Katika mechi za hivi karibuni kati ya Anderlecht inayopokea huduma za mchezaji wa zamani wa Crystal Palace Yannick Bolasie na Genk, timu hizo zimeonekana kucheza sare ya 1-1.

Haki miliki ya picha Getty Images

Akijulikana kama beki 'kisiki',Kompany alisema kuwa uamuzi wake wa kujiunga na Anderlecht kama mkufunzi mchezaji ulikuwa ''mzuri na mgumu'' baada ya kutangaza kwamba anaondoka Man City.

Wakati huohuo nahodha wa taifa Stars Mbwana Samatta alishinda tuzo hilo la kiatu cha Ebony nchini Ubelgiji kwa kuonyesha mchezo mzuri katika timu yake ya Genk.

Mchezaji huyo alifunga magoli 23.

Cha kushangaza ni kwamba Vincent Kompany pia aliwahi kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora mwenye asili ya bara Afrika nchini Ubelgiji .

Kompany aliifungia Anderlecht magoli 5 katika mechi 73 katika kipindi cha mwaka 2003 na 2006 wakati alipokuwa akiichezea klabu hiyo.

Klabu hiyo ina historia nzuri zaidi katika ligi ya Ubelgiji lakini kwa sasa iko katika nafasi ya sita katika ligi hiyo ya daraja la kwanza.

Anderlecht imeshinda mataji 34, ya hivi karibuni ikiwa msimu wa 2016-17.

Mbwana Samatta mfungaji bora wa magoli Ubelgiji

Haki miliki ya picha Getty Images

'Niliitembelea Anderlecht'

Kompany anasema kuwa mwaka uliopita alienda katika klabu hiyo wakati alipokuwa akishiriki katika timu ya taifa la Ubelgiji ili kuwasalimia.

''Marc Coucke ambaye ni mwenyekiti wa Klabu hiyo pamoja na mkurugenzi wa michezo Michael Verschueren waliomba ushauri wangu kuhusu hali ngumu ambayo klabu hiyo ilikuwa''.

''Niliwapatia wazo lango na kusikiliza maono yao: Wakiwa na maono, ujasiri na lengo la kurudi katika kilele cha ligi hiyo.

Kompany aliwapatia usaidizi wake bila ushirikiano wowote na kwamba hakutarajia wakati walipompatia wadhfa wa mchezaji mkufunzi, siku chache zilizopita.

"Nilijawa sio tu na hisia, lakini pia nilivutiwa na ishara ya imani waliokuwa nayo kwangu," alisema.

Haki miliki ya picha Getty Images

Wakati huohuo Samatta ambaye alijiunga na klabu ya Genk kutoka TP Mazembe mnamo mwezi Januari 2016, alikua akioogoza katika ufungaji wa magoli katika ligi hiyo ya Ubelgiji.

Alikuwa ameongezea magoli matatu katika ligi hiyo akiwa sawa kwa idadi ya mabao na mshambuliaji wa klabu ya Zulte Waregems , raia wa Tunisia Hamdi Harbaoui.

Vilevile mchezaji huyo wa Tanzania aliifungia timu yake mabao matatu katika michuano ya Yuropa ikiwemo mawili dhidi ya klabu ya uturuki ya Besikitas katika ushindi wa 4-2 nchini Uturuki.

Mbali na kuichezea Ubelgiji pia ameongoza timu yake ya taifa katika kufuzu katika kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 39.

Je itakuwaje Vincent Kompany wa Anderlecht atakapokutana na Mbwana Samatta wa Genk?

Mada zinazohusiana