Kylian Mbappe: PSG inasama nyota huyo wa Ufaransa atasalia klabu hiyo msimu ujao

Kylian Mbappe Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mbappe alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligue 1msimu

Kylian Mbappe''ataendeleza historia ya uhusiano wake'' na Paris St-Germain kwa kutuwakilisha msimu ujao, wanasema mabingwa hao wa Ufaransa.

Mbappe ambaye pia aliisaidia Ufaransa kushinda kombe la Dunia alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka katika Ligue 1 siku ya Jumapili.

Katika hotuba yake ya kupokea tuzo hiyo aligusia kuhusu "mradi wake mpya kwingine".

Alipoambiwa afafanue tamko hilo, nyota huyo wa miaka 20 alisema: "Nimesema kile nilichotaka kusema."

Katika taarifa kwa, PSG ilisema"Ushirikiano thabiti unaunganisha klabu hii na Mbappe", ambaye alijiunga nayo kutoka Monaco mwaka 2017.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kabla ya hapo aliichezea klabu hiyo kwa mkopo na baadae akapewa mkataba wa kudumu wa kima cha karibu euro milioni 166, kitita ambacho kilimfanya kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi baada ya Neymar.

Ameifungia PSG mabao 59 katika mechi 86, kushinda ligi mara mbili na kombe moja la Ufaransa, lakini waliondolewa katika kinyang'anyiro cha Champion League na Manchester United.

Mbappe ni mfungaji bora wa mabaolatilaLigue 1 msimu huu akiwa na mabao 32.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii