Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 21.05.2019: Sane, Pogba, Conte, Batistuta, Giroud

Leroy Sane Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Leroy Sane

Bayern Munich wanaamini kuwa watamsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ujarumani Leroy Sane, 23, kutoka Manchester City msimu huu wa joto. (Mirror)

Manchester United wanatarajiwa kuitisha euro milioni 160 (£138m) kumuuza kiungo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, 26. (Star)

Mlinzi wa Leicester na nyota wa kimataifa wa England Harry Maguire, 26, ni mmoja wa walinzi wa kati wanaolengwa na Manchester City kuchukua nafasi ya Vincent Kompany. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paul Pogba

Meneja mpya wa Anderlecht, Kompany anamfuatilia kwa karibu kocha wa chuo mpira cha Manchester City, Simon Davies na mkuu wa sayansi ya michezo Sam Erith, kuungana nae mjini Brussels. (Telegraph)

Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ameafiki masharti ya kujiunga na Inter Milan kama kocha wao mpya msimu ujao. (Guardian)

Juventus wameachana na Conte na sasa wanamlenga meneja wa sasa wa Chelsea, Maurizio Sarri. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Antonio Conte

Arsenal wametoa ofa ya kumnunua kipa wa valencia Mbrazili Norberto Murara, baada ya kuzungumzana wawakilishi wa mchezaji huyo wa miaka 29. (Star)

Nyota wa zamani wa kimataifa wa Argentina Gabriel Batistuta, 50, bado hajafikia kiwango cha ukufunzi wa timu kubwa lakini sasa inaaminiwa kuwa ameonesha nia ya kuchukua nafasi ya usimamizi iliyoachwa wazi katika klabu ya Middlesbrough. (Hartlepool Mail)

Chelsea wanatarajiwa kuthibitisha kuwa mshambuliaji wa kimataifa Ufaransa Olivier Giroud, 32, amekubali kusalia katika klabu hiyo kwa mwaka mmoja mwingine. (London Evening Standard)

Meneja wa Ireland Kaskazini Michael O'Neill amaeibuka moja wa watu wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya umeneja iliyoachwa wazi West Brom. (Express and Star)

Haki miliki ya picha EPA

Meneja mkuu wa Hertha Berlin Michael Preetz amefanya mazungumzo na mwenzake wa Liverpool Jurgen Klopp katika juhudi za kutafuta huduma za kiungo wa kati wa kimataifa wa Serbia Marko Grujic, 23, kwa mkopo wa mwaka mwingine tena. (Liverpool Echo)

Mlinzi mahiri wa zamani wa Brighton Bruno, 38, anasomea kozi ya ukufunzi wa Uefa mjini Belfast. (Argus)

Tetesi bora Jumatatu

Streka wa PSG na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, amebainisha kuwa anaweza kuihama klabu yake katika kipindi hiki cha usajili. Kauli hiyo inatarajiwa kuziamsha klabu kongwe na tajiri kama Real Madrid, Barcelona na Manchester City kumgombea. (Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kylian Mbappe

Kiungo raia wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 28, anataka kurudi mezani na klabu yake ya Manchester City kwa malengo ya kusalia klabuni hapo zaidi ya mwezi Juni 2020 ambapo mkataba wake wa sasa unaishia. (Mail)

Kocha Pep Guardiola atapewa fursa ya kusalia klabuni Manchester City walau kwa miaka mitano ijayo huku kipato chake kikifikia pauni milioni 100, baada ya mshahara wake kwa mwaka kuchupa toka pauni milioni 15 mpaka milioni 20. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Manchester City Pep Guardiola

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amemwonesha dalili za wazi winga raia wa Wales Gareth Bale, 29, kuwa muda wake katika klabu hiyo umefikia tamati, baada ya kusema kuwa asingemuingiza mchezoni kutoka benchi walipofungwa Jumapili na Real Betis hata kama kungekuwa na fursa ya kuingiza wachezaji wanne. (Eurosport)

Bale hata hivyo amewaambia wachezaji wenzake kuwa anapanga kusalia klabuni hapo mpaka kwisha kwa mkataba wake na takuwa mwenye furaha kucheza gofu endapo hatapangwa kucheza. (Radioestadio, via Mail)

Kiungo wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 28, anapiga hessabu za kuikacha klabu yake na kujiunga na miamba ya Ligi ya Ufaransa PSG. (Talksport)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii