Pigo kwa Arsenal baada ya Henrikh Mkhitaryan kujiondoa katika fainali ya ligi ya Europa

Henrikh Mkhitaryan Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Henrikh Mkhitaryan ameichezea Arsenal mechi 11 katika Ligi ya Europa msimu huu

Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan hatacheza mechi ya fainali ya Ligi ya Europa dhidi Chelsea Mei 29.

Inasemekana kuwa Muarmenia, huyo wa miaka 30, amehofia usalama wake uwanjani Baku, Azerbaijan.

"Baada ya kutathmini njia zote,ilibidi tufanye uamuzi huo mgumu wa mimi kutosafairi na kikosi kitakachoshiriki fainali ya Ligi ya Europa," alisema Mkhitaryan.

"Ni aina ya mchezo ambao ni nadra sana, kwa kweli nasikitika sana kuwa sitacheza."

Kutokana na mzozo wa kisiasa kati ya Azerbaijan na Armenia, Mkhitaryan amekosa mechi kadha za klabu zilizochezwa Azerbaijan aiku zilizopita.

"Tumeandikia Uefa kuelezea hofu yetu kuhusu hali hiyo," alisema taarifa ya Arsenal.

"Tumejaribu mbinu zote ili Micki ajumuishwe kwenye kikosi hicho lakini baada ya kujadiliana na Micki na familia yake tulikubaliana kwa pomoja kuwa ajiondoe kwenye msafara huo.

Haki miliki ya picha Getty Images

"Micki amekuwa kiungo muhimu kuelekea fainali hii kwa kweli ni pigo kubwa kwa timu nzima.

"Pia tunasikitika kuwa atakosa mechi kubwa kama hiyo barani Ulaya kutokana na hali kama hii, ikizingatiwa kuwa ni furasa adimu katika mchezo wa kandanda."

Uefa iliijibu Arsenal kupitia taarifa ya maandishi iliyosema: "Tukishirikiana na Arsenal FC, Uefa imepata hakikisho kutoka kwa mamlaka ya juu ya nchi kuwa usalama wa mchezaji nchini Azerbaijan utaimarishwa.

"Kutokana na hakikisho hilo, mpango madhubuti wa usalama ulifanywa na kupewa klabu hiyo.

"Japo Klabu imeridhishwa na juhudi za Uefa na serikali ya Azerbaijan, tunaheshimu uamuzi wa kibinafsi wa mchezaji kutosafiri."

Shirikisho la soka la Azerbaijan FA limeelezea "masikitiko" yake kuwa Mkhitaryan hatujiunga na klabu yake kishiriki mechi hiyo muhimu ya fainali.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Henrikh Mkhitaryan ni nahodha wa Armenia na ameifungia timu hiyo mabao 27 katika mechi 82

Katika taarifa yake shirikisho la AFFA lilisema: "Tunasikitika sana na uamuzi uliyochukuliwa. Japo tunaheshimu uamuzi wa kibinafasi kuhusu suala hili, tunasisitiza kuwa Azerbaijan kama mwenyeji wa fainali hizo imeweka mikakati yote ya kiusalama inayohitajika na Uefa kuhakikisha usalama wa kibinafsi wa Bw. Mkhitaryan unalindwa.

"Hakuna haja ya kutilia shaka hakikisho lililotolewa na Azerbaijan."

Arsenal, amabo walimaliza ligi ya Primia katika nafasi ya tano, watafuzu kwa Champions League msimu ujao wakiishinda Chelsea.

Itakuwa kombe lao la kwanza la ulaya tangu mwaka 1994.

Meneja wa Arsenal Unai Emery amesema: "Alitaka kucheza, alakini alipozungumza na familia yake akaamua kubadili msimamo huo..

"Ni uamuzi wa kibinafsi sana na tunahitaji kuheshimu uamuzi wake. Sina ufahamu kuhusu tatizo la kisiasa lakini lazima niheshimu uamuzi wake."

Siku ya Jumatatu Balozi wa Azerbaijan nchini Uingereza, Tahir Taghizadeh, alisema hakuna haja ya kuwa na hofu kuhusu usalama wa nyota huyo raia wa Armenia.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii