Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 23.05.2019: Terry, Cancelo, Trippier, Rakitic, Wan-Bissaka

John Terry Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Terry

Nahodha wa zamani wa England na Chelsea John Terry, ambaye kwa sasa ni naibu meneja wa Aston Villa, anashauriana na Middlesbrough kuhusu uwezekano wa kuwa maneja wao mpya.(Talksport)

Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Ureno Joao Cancelo, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa na Juventus kuwa euro milioni 60. (Record - in Portuguese)

Atletico Madrid na Napoli wanapania kumsajili beki wa kulia wa Tottenham na mchezaji wa kimataifa wa England Kieran Tripper, 28. (Mirror)

Spurs wameweka dau la £10m kumnunua winga wa Leeds United wa miaka 18, Muingereza Jack Clarke. (Mail)

Manchester United wanashughulikia mpango wa kumsaini Ivan Rakitic, 31, lakini Barcelona wanataka kulipwa uero milioni 48 kumwachilia nyota huyo wa kimataifa wa Croatia. (Record)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ivan Rakitic

United wanatarajiwa kuwasilisha dau la kwanza la £25m kumunua beki wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka, 21, lakini Eagles wanataka £50m kumwachilia mchezaji huyo. (Evening Standard)

Muargentina Sergio Romero, 32, huenda akapandishwa cheo kuwa kipa wa Manchester United ikiwa David de Gea, 28, ataondoka Old Trafford msimu huu wa joto. (Mail)

United tayari wamewasilisha rasmi ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21. (ESPN)

Everton, West Ham na Manchester United wamepewa nafasi ya kumsaini kwa mkopo kiungo wa kati wa Uholanzi na Marseille Kevin Strootman, 29. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Romelu Lukaku

Antonio Conte anatarajiwa kusajili mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, kutoka Manchester United atakapoajiriwa kama meneja wa Inter Milan. (Times - subscription required)

Liverpool wanakaribia kukamilisha mpangowa £200,000 wa kumsajili kipa raia wa Poland Jakub Ojrzynski, 16, kutoka Legia Warsaw. (Liverpool Echo)

Wolves wanaongoza kinyang'anyiro cha kumsaini mshambuliaji Moussa Marega, 28 rai wa Mali ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £30m-kutoka Porto. (Mirror)

Haki miliki ya picha BBC Sport

Newcastle, Southampton na Brighton wote wanataka kusaini winga Harry Wilson, 22, lakini Liverpool wanataka kulipwa £25m kumwachilia nyota huyo wa kimataifa wa Wales. (Sky Sports)

Bournemouth wako tayari kupokea ofa ya kummuuza winga Jordon Ibe, 23 raia wa Uingereza. (Mirror)

Tetesi Bora Jumatano

Kiungo wa kati wa United Paul Pogba, 26, atapewa jukumu la unahodha wa klabu hiyo katika juhudi za kumshawishi Mfaransa huyo asiondoke Old Trafford. (ESPN)

Kipa wa Arsenal Petr Cech, 37, atarejea Chelsea msimu huu wa joto kuchukua wadhifa wa mkurugenzi wa michezo. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Petr Cech amecheza mara 10 katika Ligi ya Europa msimu huu

Gunners wanatafakari uwezekano wa kumsajili kwa uhamisho wa bila malipo kipa wa Dynamo Dresden na Ujerumani wa timu ya wachezaji wa chini ya miaka 21 Markus Schubert, 20, msimu ujao kuchukua nafasi ya Cech. (Bild - in German)

Kipa wa Uhispania na Manchester United David de Gea, 28,amekataa kutia saini mkataba mpya na klabu hiyo wakati mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu ujao. (Sun)

Meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri, 60, analengwa na Juventus wanapomtafuta nani atakaechukua nafasi ya Massimiliano Allegri huku Mtaliano huo pia akinyatiwa na klabu ya Roma. (Sky Sports)

The Blues hawatazuia Sarri kuondoka ikiwa Juventus itakuwa tayari kulipa hadi pauni milioni tano (£5m) kama fidia ya kumrudisha Italia. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maurizio Sarri

Manchester United wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsaini winga wa Swansea na Wales, Daniel James, 21 kwa pauni milioni kumi na tano.(Mail)

Tottenham wamekata tamaa ya kumsajili winga wa Crystal Palace Wilfied Zaha, 26, baada ya kushindwa kufikia bei ya pauni milioni mia moja (£100m) kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast. (Evening Standard)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii