Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 24.05.2019: Rodriguez, Sane, Asensio, Trippier, Lukaku

James Rodriguez Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption James Rodriguez

Liverpool, Manchester United na Arsenal wanataka kumsaini mchezaji nyota wa Colombia James Rodriguez, 27, ambaye anatarajiwa kuondoka Bayern Munich mkataba wake wa mkopo utakapokamilika msimu huu. (Mirror)

Rais wa Bayern Munich Uli Hoeness amethibitisha kuwa mabingwa hao wa Bundesliga wanamtaka winga wa Manchester City Mjerumani Leroy Sane. (Suddeutsche Zeitung - in German)

City wanajiandaa kuweka dau la kumnunua nyota huyo wa miaka 23 kutoka kwa miamba hao wa ujerumani ambalo linatarajiwa kuvunja rekodi. (Mail)

Arsenal wanataka kumsaini winga Ryan Fraser, 25, baada ya fainali ya ligi ya Europa, lakini Bournemouth wanataka kulipwa £30m kumwachilia kiungo huyo wa kimataifa wa Uskochi. (Independent)

Tottenham wamewasiliana na Real Madrid ili kuanza mazungumzo ya kutaka kumnunua kiungo wa kati Marco Asensio, 23, lakini wameambiwa mchezaji huyo rai wa Uhispania hapatikani. (AS - in Spanish)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marco Asensio (Kulia)

Kocha wa Newcastle Rafael Benitez amewambia Marseille na Roma kuwa kipaumbele chake ni kukubali mkataba mpya St James Park baada ya wao ku kuonesha ari ya kutaka kumpatia kazi ya umeneja. (Chronicle)

Wachezaji Matteo Darmian, 29, Romelu Lukaku 26, Juan Mata, 31, na Marcos Rojo - huenda wakondoka Manchester United msimu huu(Mirror)

Inter Milan itatangaza ofa ya zaidi ya £30m winga wa Croatia winger Ivan Perisic, 30, ili kumnunua Lukaku. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ivan Perisic

Manchester City wanataka £15m kumuuza kiungo wa kati Fabian Delph, huku vilabu kadhaa vya ligi ya Premier vikimnyatia nyota huyo wa miaka 29. (Sun)

Mshambuliaji wa Crystal Palace Christian Benteke, 28, huenda akaondoka Selhurst Park msimu huu baada ya kukubali dau la £15m la kumnuuza nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kutoka klabu ya China ya Shandong Luneng Taishan. (Times - subscription required)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Christian Benteke(Kulia)

Napoli wanatarajiwa kumsaini beki wa kulia- kushoto wa Tottenham Kieran Trippier, 28, huku Mwingereza huyo akipewa idhini ya kukubali ofa nzuri. (Independent)

Manchester United wanatarajiwa kumsaini mshambuliaji Dillon Hoogewerf baada ya kucheza mechi ua vijana wa Ajax. (Metro)

Arsenal ni moja ya vilabu vinavyofuatilia mchezo wa mshambuliaji Danny Loader, 18 raia wa Ungereza. (Goal)

Haki miliki ya picha SNS
Image caption Kocha wa Leicester, Brendan Rodgers (Kulia)

Meneja wa Leicester Brendan Rodgers anatathmini uwezekano wa kuungana tena na winga Patrick Roberts, ambaye alicheza chini yake wakati alipokua Celtic. (Sun)

Tetesi Bora Alhamisi

Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Ureno Joao Cancelo, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa na Juventus kuwa euro milioni 60. (Record - in Portuguese)

Nahodha wa zamani wa England na Chelsea John Terry, ambaye kwa sasa ni naibu meneja wa Aston Villa, anashauriana na Middlesbrough kuhusu uwezekano wa kuwa maneja wao mpya.(Talksport)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Terry

Atletico Madrid na Napoli wanapania kumsajili beki wa kulia wa Tottenham na mchezaji wa kimataifa wa England Kieran Tripper, 28. (Mirror)

United tayari wamewasilisha rasmi ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21. (ESPN)

Everton, West Ham na Manchester United wamepewa nafasi ya kumsaini kwa mkopo kiungo wa kati wa Uholanzi na Marseille Kevin Strootman, 29. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Romelu Lukaku

Spurs wameweka dau la £10m kumnunua winga wa Leeds United wa miaka 18, Muingereza Jack Clarke. (Mail)

Manchester United wanashughulikia mpango wa kumsaini Ivan Rakitic, 31, lakini Barcelona wanataka kulipwa uero milioni 48 kumwachilia nyota huyo wa kimataifa wa Croatia. (Record)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii