Premier League: Liverpool yaongoza mbele ya mabingwa Man City

Wachezaji wa Liverpool na Manchester City Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Liverpool ilikaribia kushinda ligi ya Uingereza tangu 1990

Liverpool ilijipatia zaidi ya takriban £152m kutoka kwa ligi ya Uingereza msimu huu ikiwa ni £1.44m zaidi ya mabingwa Manchester City, baada ya kushiriki katika mechi nyingi za moja kwa moja katika mechi zilizopeperushwaa na runinga Uingereza

The Reds, ambao walimaliza wa pili katika jedwali la Uingereza wakiwa na jumla ya pointi 97 walionyeshwa wakicheza moja kwa moja mara 29 katika Sky Sports ama BT Sport ikiwa ni mara tatau zaidi ya Man City.

Kikosi hicho cha Pep Guardiola kilipokea £38.4m kwa kumaliza juu ikiwa ni zaidi ya takriban £2m zilizopokewa na kikosi cha Jurgen Klopp.

Klabu ya Huddersfield ambayo ilishushwa daraja ilipokea £96.6m baada ya kumaliza wa mwisho.

Klabu zote ishirini zilipokea mapato sawa ya £34.4m, pamoja na £43.2m kutoka kwa runinga za kimataifa kila moja na £5m za mauzo

2018-19 Mapato ya ligi ya Premier
Mechi za moja kwa moja Malipo kwa jumla (£)
Manchester City 26 150,986,355
Liverpool 29 152,425,146
Chelsea 25 146,030,216
Tottenham 26 145,230,801
Arsenal 25 142,193,180
Manchester United 27 142,512,868
Wolves 15 127,165,114
Everton 18 128,603,905
Leicester 15 123,328,078
West Ham 16 122,528,663
Watford 10 113,895,527
Crystal Palace 12 114,215,215
Newcastle 19 120,130,418
Bournemouth 10 108,139,973
Burnley 11 107,340,558
Southampton 10 104,302,937
Brighton 13 105,741,728
Cardiff 12 102,704,107
Fulham 13 101,904,692
Huddersfield 10 96,628,865

Mada zinazohusiana