Asamoah Gyan achaguliwa "Kapteni Jenerali" wa timu ya taifa ya Ghana Black Stars

Asamoah Gyan appointed 'general captain' Haki miliki ya picha AFP

Nyota wa soka nchini Ghana Asamoah Gyan amepewa wadhifa mpya baada ya kuvuliwa ukapteni katika timu ya taifa.

Kocha wa timu ya Black Stars, Kwasi Appiah, amempa Gyan wadhifa wa "Kapteni jenerali", kutokana na kuba wake katika timu hiyo

Andre Ayew akitajwa kapteni mpya wa kudumu.

Uamuzi wa kocha Appiah unafuata mkutano na wasimamizi wakuu wa kamati ya shirikisho la soka Ghana.

Jumatatu wiki hii, Gyan alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa kupinga mipango ya kumuondoa katika nafasi hiyoya kapteni.

Alibatilisha uamuzi huo baada ya mawasiliano ya simu na rais wa Ghana Nana Akuffo-Addo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliyefanikiwa kufunga mabao 51 katika michauno 106 ya kimataifa, alisema kwamba amejiuzulu "kabisa" baada ya kuondoshwa katika wadhifa huo wa kapteni.

Rais Nana Akufo-Addo alizungumza na Gyan siku ya Jumanne, na kumshawishi mshambuliaji huyo wa Kayserispor abadili uamuzi wake

"Ombi la rais haliwezi kupuuzwa," amesema.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Nana Akufo-Addo

Kabla ya kupokonywa wadhifa huo, Gyan aliwahi kuhudumu katika wadhifa huo wa ukapteni kwa miaka saba.

Wadhifa huo umezusha mzozo mkubwa katika timu ya taifa ya Ghana kwa miaka mingi.

Gyan hajawahi kuichezea timu hiyo tangu mnamo 2017 kutokana na jeraha, na ameng'ang'ana kupata fursa ya kucheza katika timu ya Kayserispor.

Amesema anatamani kuisaidia Ghana ishinde katika mashindnao ya Afcon na anaendelea kuwajibika kuitumikia nchi yake na watu wa Ghana.

Gyan amefanikiwa kufunga katika fainali sita mtawalia za kitaifa pamoja na katika mashindnao ya kombe la dunia kati ya mwaka 2006 na 2014.

Timu ya Black Starsitacheza mechi yake ya kwanza katika kombe la matifa ya Afrika dhidi ya Benin Juni 25..

Haijawahi kushinda katika mashindano hayo tangu 1982.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii