Tetesi za soka Ulaya Jumapili 26.05.2019: Pogba, Dybala, Sandro, Hazard, Silva, De Ligt, Fekir

Eden Hazard

Chelsea itataka kulipwa £130m na Real Madrid ili kumuuza mshambuliaji wake Eden Hazard, 28, ijapokuwa mabingwa hao wa Uhispania wanathamini mchezaji huyo wa Ubelgiji kuwa na thamani ya £88m. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri amekubali mkataba wa kuifunza Juventus baada ya mkufunzi wa Man City Pep Guardiola kukataa wito wa klabu hiyo ya Itali (Italian journalist Tancredi Palmeri, via Sunday Mirror)

Juventus iko tayari kumuuza mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, na beki wa Brazil mwenye umri wa miaka 28 Alex Sandro ili kubadilishana na kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba, 26. (Sunday Express)

Haki miliki ya picha Getty Images

Wakati huohuo, United inakaribia kumsaini beki wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, licha ya Barcelona kuwa katika nafasi nzuri ya kumsaini beki huyo wa Uholanzi . (RAC1, via Metro)

Manchester City itampatia winga wa Ujerumani Leroy Sane £150,000 kwa wiki ili kujaribu kuanzisha mazungumzo ya kandarsi mpya , lakini pia watamuuaza mchezaji huyo kwa zaidi ya £100m ambaye analengwa na klabu ya Bayern Munich, iwapo mnakubaliano hayataafikiwa . (Sunday Mirror)

Kiungo wa kati wa Uhispania David Silva amepewa kandarasi nzuri ya miaka miwili na klabu ya Qatar na huenda ameichezea Man City mechi yake ya mwisho. (Sun on Sunday)

West Ham wameipatia Barcelona takriban £18m ili kumnunua kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ureno Andre Gomes, ambaye alihudumu msimu uliopo kwa mkopo katika klabu ya Everton. (Sunday Times - subscription required)

Mkufunzi wa zamani wa Asenal Arsene Wenger amepata ofa ya kurudi katika ukufunzi na klabu ya Japan ya Vissel Kobe. (Goal.com)

Lazio imejiunga na Everton, Newcastle na West Ham katika kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Uingereza ambaye hana kandarasi Danny Welbeck, 28. (Sun on Sunday)

Ombi la United kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21, litategemea iwapo Rafael atasalia kuwa mkufunzi wa klabu hiyo. (Newcastle Chronicle)

Haki miliki ya picha Getty Images

Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya AC Milan Ivan Gazidis amewasiliana na Massimiliano Allegri kuona iwapo anataka kurudi kuifunza klabu hiyo wakati atakapoondoka katika klabu ya Juventus mwisho wa msimu huu . (Tuttomercatoweb - in Italian)

Manchester United italazimika kulipa zaidi ya £105m ili kumsaini mshambulaji wa Benfica 19 Joao Felix, kulingana na meneja wa klabu hiyo Domingos Soares de Oliveira. (Sunday Express)

Liverpool inataka kutumia fursa ya mwanya uliopo katika kandarasi ili kumsaijili kinda wa Brazil na klabu ya Fluminense mwenye umri wa miaka 17 , licha ya kwamba raia huyo wa Brazil amekubali kujiunga na Watford. (Globoesporte - in Portuguese)

Mchezaji anayelengwa na Manchester United Kalidou Koulibaly huenda akajiunga na Real Madrid baada ya klabu hiyo la La Liga kuwasilisha dau la £79m kwa klabu hiyo ya Napoli kumnunua beki huyo wa kati wa Senegal , 27. (Corriere dello Sport - in Italian)

Rais wa aklabu ya Lyon Jean-Michel Aulas amekubali kumwachilia kiungo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 Nabil Fekir, ambaye karibu ajiunge na Liverpool mwaka uliopita kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu. (L'Equipe - in French)

Winga wa Chelsea Victor Moses atapunguza kwa ufupi mkopo wake katika klabu ya Fenerbahce.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 wa Nigeria anatumai kujiunga tena na Antonio Conte wakati mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea atakapopewa ukufunzi wa klabu hiyo ya Itali. (Football London)

Haki miliki ya picha Getty Images

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Edin Dzeko anatarajiwa kuondoka Roma huku raia huyo wa Bosnia , 33, akitarajiwa kujiunga na Inter Milan. (Sky Italia, via Football Italia)

Blackburn Inafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua straika wa Everton mwenye umri wa miaka 21 na raia wa Ujerumani Bassala Sambou, ambaye anamaliza kandarasi yake mwisho wa msimu huu (Lancashire Evening Telegraph)

Mshambuliaji mwengine huenda akaihama Everton , huku raia wa Nigeria Henry Onyekuru, 21, akiambia klabu hiyo anataka kuufanya uhamisho wake katika klabu ya Galatasaray kuwa wa kudumu ili kushiriki katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulayamsimu ujao. (Fanatik - in Turkish)

Haki miliki ya picha Getty Images

Mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay, 25, amezua uvumi kwamba huenda akaihama klabu ya Lyon kwa kuchapisha video katika mtandao wake wa instagram akiwa anapanda ndege ya kibinafsi na traki yenye maandiko "Merci Lyon". (Mail on Sunday)

Mshambuliajhi wa Tottenham Harry Kane, 25, analekea kuponya ili kushiriki katika fainali ya kombe la ligi ya mabingwa dhidi ya Liverpooli siku ya Jumamosi tarehe mosi mwezi Juni baada ya mshambuliaji huyo wa Uingereza kunaza kupona jeraha lake la kifundo cha mguu (Sunday Times - subscription required)

Mkufunzi wa zamani wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson ameshangazwa ni kwa nini klabu hiyo haitafuti ushauri wake na anaamini kwamba klabu hyo ingemsajili mkufunzi wa Tottenham manager Mauricio Pochettino badala ya Ole Gunnar Solskjaer. (Mail on Sunday)

Mada zinazohusiana