Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 27.05.19: De Ligt, Neymar, Mbappe, Berahino, Boateng,Rojo

N'Golo Kante Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption N'Golo Kante ameendelea kuwa kiungo muhimu katika safu ya ulinzi ya Chelsea kama ilivyo kwa timu ya taifa ya Ufaransa.

Kiungo mkabaji wa Chelsea N'Golo Kante, 28, anaweza kuukosa mchezo wa fanali wa Europa dhidi ya Arsenal baada ya kupata majeraha ya goti akiwa mazoezini. (Guardian)

Mchezaji anayewaniwa na Barcelona Matthijs de Ligt, 19, ataamua mustakabali wake baada ya kushiriki ligi ya kimataifa ya Ulaya na timu yake ya taifa ya Uholanzi - tayari beki huyo kisiki na nahodha wa Ajax amesema anaipenda ligi ya Primia. (ESPN)

Kocha wa Paris St-Germain Thomas Tuchel amesema hana hakika kama washmbuliaji wwake raia wa Brazil Neymar, 27, na Mfaransa Kylian Mbappe, 20, kama watasalia na klabu yake msimu ujao ingawa bado anawahitaji. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Benchi la ufundi la PSG lipo mashakani kuwakosa washambuliaji wake mahiri Mbappe na Neymar kwa mpigo.

Mmiliki wa Newcastle United Mike Ashley amekubali kuiuza klabu yake kwa binamu wa wa mmiliki wa Manchester City kwa kitita cha pauni milioni 305. (Sun)

Klabu ya Manchester City wameingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Monaco mwenye thamani ya pauni milioni 40, Youri Tielemans. Klabu ya Leicester pia wanataka kumsajili kiungo huyo raia wa Ubelgiji mwenye miaka 22 baada kuichezea klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sergio Ramos aliwaongoza Real Madrid kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara ya nne katika miaka mitano

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anataka kumbakiza beki Sergio Ramos, 33, klabuni hapo msimu ujao. Klabu kadhaa zinamuwinda beki huyo mkongwe zikiwemo Liverpool, Manchester United na timu kadhaa za ligi ya Uchina. (Marca - in Spanish)

Timu ya Stoke City imemtaarifu mshambuliaji wao raia wa Burundi Saido Berahino mwenye thamani ya pauni milioni 12 kuwa wamesitisha mkataba wake baada ya kukutwa na kosa la kuendesha gari huku akiwa amekunywa pombe. (Mail)

Image caption Stoke City imekatisha mkataba na Berahino kwa kile walichokiita utovu wa nidhamu

Klabu ya Tottenham wamearifiwa kuwa itawapasa kutoa kitita cha pauni milioni 20 ili kumsajili kiungo kinda wa England anayechezea Leeds United Jack Clarke, 18. (Mirror)

Beki raia wa Argentina Marcos Rojo, 29, amesema kuwa amehakikishiwa mustakabali wake na uongozi wa klabu ya Manchester United. (Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Majeraha yameandama kiwango cha Marcos Rojo

Raisi wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness amemwambia beki mkongwe wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ujerumani Jerome Boateng, 30, kuwa anaweza kuihama klabu hiyo ya Bundesliga. (Bild - in German)

Raia wa Algeria na mchezaji wa zamani wa Newcastle Mehdi Abeid, 26, anataka kurejea kwenye ligi ya Primia badala ya kusaini mkataba mpya na klabu ya Dijon kwenye Ligi ya Ufaransa. (L'Equipe - in French)

Image caption Jose Mourinho bado hajapata kibarua kipya

Kocha wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho bado hajafanya uamuzi wa klabu gani ya kwenda kuifundisha toka alipofukuzwa na United mwezi Disemba. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Spurs Harry Kane anatarajiwa kusafiri na wachezaji wenzake kulekea jijini Madrid pamoja na kikosi kizima cha klabu yake. Kane anajaribu kuthibitisha kuwa yupo 'fiti' kuchuana na Livepool kwenye fainali ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Liverpool. (Mail)

Mada zinazohusiana