Mwenyekiti wa City Khaldoon Al Mubarak adai baadhi ya wapinzani wao wanawaonea wivu

Manchester City chairman Khaldoon Al Mubarak with manager Pep Guardiola Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwenyekiti wa Manchester City Khaldoon Al Mubarak (kushoto) na kocha wake manager Pep Guardiola

Mwanyekiti wa Klabu ya Manchester City Bw Khaldoon Al Mubarak amesema baadhi ya wapinzania wao wana wivu juu ya mafanikio ya klabu hiyo.

City imekuwa klabu ya kwanza kushinda makombe matatu ya ligi za ndan ya Uingereza baada ya kuifunga Watford 6-0 kwenye fainali ya kombe la FA.

Mafanikio hayo lakini yanakosolewa na baadhi ya wachambuzi wakisema kocha wa City Pep Guardiola ametumia kitita kikubwa cha fedha kwenye usajili.

Hata hivyo, kwenye tathmini yake ya mwisho wa msimu, Mubarak ameviambia vyombo vya habari vya klabu hiyo kuwa hatakubali klabu yake "kutumika katika njama za kuhalalisha maamuzi ya kutowekeza vyema kwenye mpira."

Mabingwa hao wa Ligi ya Primia hawana hata mchezaji mmoja kwenye orodha ya wachezaji ghali 10 wa ligi hiyo. Wapinzania wao wakuu wana wachezaji wawili Paul Pogba (aliyesainiwa kwa pauni milioni 89) na Romelo Lukaku (aliyesainiwa kwa dau la awali la pauni milioni 75), Liverpool ina mchezaji mmoja kwenye orodha hiyo, Virgil van Dijik, aliyesainiwa kwa pauni milioni 75.

Mchezaji ghali zaidi kusainiwa na City ni Riyad Mahrez, waliyemng'oa Leicester City kwa pauni milioni 60 Julai in July 2018.

Wachezaji wengine ghali wa City ni Aymeric Laporte (pauni milioni 57), Kevin de Bruyne (pauni milioni 55) na Benjamin Mendy (pauni milioni 52).

"Mafanikio huambatana na kuonewa wivu, husda na kijicho, pamoja na mengine mengi. Hiyo ni sehemu ya mchezo," amesema Mubarak.

"Najua mambo ni magumu kwa wapinzani wetu, tunalifahamu hilo fika. Lakini uhalisia ni kuwa, hatujasaini mchezaji ghali zaidi kwenye ligi [Pogba], hatujamnunua kipa ghali zaidi [Kepa Arrizabalaga], hatujanunua kiungo ghali zaid, na pia hatujamsaini mshambuliaji ghali zaidi [Lukaku].

"Watu hufanya maamuzi, inabidi waishi nayo. Hii ni klabu inayoendeshwa vizuri."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Riyad Mahrez ndiye mchezaji ghali zaidi kuwahi kusainiwa na City kwa kitita cha pauni milioni 60.

Kukosolewa kwa City kunakuja wakati huu ambapo inachunguzwa na chombo cha fedha cha Uefa kwa tuhuma za kufanya matumizi mabaya kwenye usajili. City inakanusha vikali tuhuma hizo.

Mubarak amekasirishwa zaidi na matamshi ya rais wa ligi ya Uhispania, La Liga Bw Javeir Tebas ambaye hivi karibuni ammeziita klabu za City na PSG kama 'wanasesere' wa nchi fulani na kuzitaka zitimuliwe kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kutokana na namna wanavyomwaga fedha kwenye usajili.

City, backed inamilikiwa na kampuni ya Abu Dhabi United Group kutoka Falme za Kiarabu, huku PSG ikimilikiwa na kampuni ya Qatar Sports Investments.

"Naamini hili ni jambo baya sana kuziunganisha timu na kuzikosoa kulingana na rangi na asili ya wamiliki wake," amesema Mubarak.

City wanaamini matamshi ya Tebas hayajazingatia kipindi ambacho Real Madrid walitumia mamilioni ya pauni kuwaasajili nyota katika zama zao maarufu kama 'galactico'.

Wachezaji waliosajiliwa kipindi hicho na Madrid kwa madau ya kushtusha ni pamoja na Luis Figo, Zinedine Zidane, Ronaldo na David Beckham kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2000.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiwango cha Man United kinaendelea kusuasua licha ya kuwa na mchezaji ghali zaidi wa EPL, Paul Pogba.

"Sidhani kama shambulio hili linaishia kwetu Man City tu. Shambulio linalenga ligi nzima ya EPL. Naamini watu wameanza kuliona hilo. Najua kuwa watu hawataki kuitetea Man City - Lakini inawapasa waanze kuitetea ligi hii.

"Kuna klabu nne za Primia kwenye fainali mbili za makombe ya Ulaya. Hii ndio ligi bora duniani, ligi yenye mafanikio zaidi ya kibiashara na mabayo inaoneakana sehemu nyingi za dunia. Hilo linawaumiza watu wengi kutoka maeneo tofauti."

Mei 14, City walisema kuwa wanasikitishwa na habari iliyochapishwa na gazeti la New York Times na kudai kuwa maafisa wa Uefa wanataka klabu hiyo ifungiwe kushiriki mashindano yanayoandaliwa na chombo hicho.

City inadai kuwa na hofu juu ya uwepo wa watu ambao kwa maslahi yao ya kibiashara wanataka timu hiyo ifungiwe na Uefa.

Mubarak amesema kuwa Man City itasafishwa punde tu uchunguzi huo utakapokamilika kwa hoja zilizo wazi.

"Endapo suala hilo halitafanyika kwa misingi ya ya hoja, basi kwa hakika tutakuwa na maongezi ya namna nyengine kabisa."

Mada zinazohusiana