Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 29.05.2019: Lukaku, Solskjaer, Neymar, Hazard, Cavani, Costa, Jovic

Romelu Lukaku Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Romelu Lukaku

Mshambuliaji wa Manchester United Mbelgiji Romelo Lukaku, 26, yupo tayari kukatwa mshahara ili ahamie klabu ya Inter Milan hivi karibuni. (Gazzetta dello Sport)

Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer ameipa klabu yake mpaka mwakani kuuza wachezaji wote asiowataka ikiwa kama sehemu ya miango yake ya kuijenga upya klabu hiyo. (MEN)

Barcelona wameamua kuendelea na kocha Ernesto Valverde kwa msimu ujao japo kulikuwa na ripoti kuwa kocha huyo alikuwa afutwe kazi. (Marca)

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema ana matumaini ya kumsajili Eden Hazard, 28, katika majira haya ya joto. (Onda Cero, via Mirror)

Atletico Madrid wamemchagua mshambuliaji wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya Uruguay Edinson Cavani, 32, kama mbadala wa mshambuliaji wao Diego Costa, 30. (Cadena Ser - in French)

Newcastle United wamefanya mawasiliano na klabu ya Benfica wakiwa na nia ya kumsajili kipa wao raia wa Ugiriki Odysseas Vlachodimos, 25, na inaaminika Benfica wanataka kitita cha pauni milioni 13. (O Jogo - in Portuguese)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Je, PSG watakubali kubadilishana na Barcelona wachezaji?

Barcelona pia inasemekana wapo tayari kumtoa kiungo Philippe Coutinho, 26, ama mshambuliaji Ousmane Dembele, 22, kwenda Paris St-Germain kama sehemu ya makubaliano ya kumpata mshambuliaji Neymar, 27. (Record)

Kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte amesaini mkataba mpya wa kuinoa klabu ya Inter Milan mpaka mwaka 2022. (Tuttomercatoweb - in Italian)

Image caption Antonio Conte

Streka wa Eintracht Frankfurt Luka Jovic yaonekana hana nia ya kuendelea kusakata kabumbu kwenye klabu hiyo baada ya kuhamisha viurago vyake kwenye kabati lake la timu kabla ya michuano ya Ulaya ya wachezaji wa chini ya miaka 21. (Bild - subscription)

Kocha wa Arsenal Unai Emery anataka kumsajili beki wa pembeni wa Ubelgiji Thomas Meunier, 27, kutoka katika klabu ya Paris St-Germain. (France Football)

Barcelona wanataka kumsajilibeki wa kushoto wa klabu ya Wolfsburg Mfaransa Jerome Roussillon, 26, baada ya mchezaji huyo kuwakuna wachunguzi wa klabu hiyo waliokuwa wakimuangalia kipa wa timu hiyo Koen Casteels, 26. (Mundo Deportivo - in Spanish )

Timu iliyopanda daraja Ligi ya Primia Aston Villa itaanza maandalizi ya michuano hiyo kwa kutuma nia ya kumsajili mshambuliaji wa Nottingham Forest Joe Lolley, mwenye thamani ya pauni milioni 10. (Mail)

Beki wa kulia wa Tottenham na England Kieran Trippier, 28, hatasainiwa tena na klabu ya Napoli baada ya timu hiyo kuelekeza nguvu zake kwa wachezaji kinda. (Sun)

Tetesi bora Jumanne

Haki miliki ya picha Reuters

Mchezaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, Sergio Ramos mwenye umri wa miaka 33 amemwomba bosi wa Real Madrid Florentino Perez kumruhusu aikache klabu yake na kwenda China. (LaSexta - in Spanish)

Bosi wa Chelsea Maurizio Sarri ambaye amehusishwa kwenda kujiunga na klabu ya Juventus inasemekana kuwa amefikia makubaliano ya kupewa mshahara wa kiasi cha pauni milioni 1.2kila mwaka . (Mail)

Meneja wa timu ya taifa ya Uholanzi Ronald Koeman, Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri na Kocha wa Arsenal Unai Emery ni miongoni mwa watu ambao wanapewa nafasi ya kwenda kuchukua mikoba ya bosi wa sasa wa Barcelona Ernesto Valverde. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester United na Real Madrid zinaweza kumuwania mchezaji wa Argentina Giovani lo Celso, 23, msimu huu.

Mchezaji wa Ajax, Matthijs de Ligt, 19 amesema kwamba ripoti zinazomuhusisha kutaka kuhamia Manchester United zisizingatiwe.

Mada zinazohusiana