Europa League: Chelsea yaikamua Arsenal na kushinda kombe la ligi ya Europa

Wachezaji wa Chelsea wakisherehekea ushindi wao Haki miliki ya picha Reuters

Eden Hazard alifunga magoli mawili huku Chelsea ikiicharaza Arsenal katika fainali ya kombe la Europa

Eden Hazard alifunga magoli mawili huku Chelsea ikiicharaza Arsenal katika fainali ya kombe la Europa na kumpatia kocha Maurizio Sarri kombe lake la kwanza tangu achukue ukufunzi wa timu hiyo.

Olivier Giroud aliifungia Chelsea goli la kwanza dhidi ya klabu yake ya zamani kupitia kichwa kizuri huku Pedro akifunga goli la pili kupitia krosi ya Hazard.

Baada ya kutoa pasi ya bao la pili , raia huyo wa Ubelgiji alifunga penalti na kufanya mambo kuwa 3-0.

Alex Iwobi aliipatia Arsenal bao la kufutia machozi mda mchache baada ya kuingia kama mchezaji wa ziada lakini Hazard alifunga krosi nzuri ya Giroud na kufanya mambo kuwa 4-1.

Huku uwanja ukiwa na mashabiki 5000 kutoka pande zote mbili hali haikuwa shwari katika uwanja huo ulioonekana kujaa nusu nchini Azerbaijan.

Mchezaji wa Arsenal wa zamani Olivier Giroud ndie aliyeanza kucheka na wavu baada ya kupata krosi nzuri kutoka kwa Emmerson.

Huku Cech naye pia akikabiliana na timu yake ya zamani na pengine akishiriki katika mechi yake ya mwisho hakuweza kuisaidia Arsenal wakati walipofungwa goli la pili baada ya Pedro kufagilia krosi iliopigwa na Hazard.

Hazard asema kwaheri kwa kuonyesha mchezo mzuri

Haki miliki ya picha Getty Images

Mchezaji huyo wa Ubelgiji baada ya mechi hiyo alisema kuwa huenda ndio kwaheri yake katika klabu hiyo huku akiendelea kuhusishwa na uhamisho wa Real Madrid.

Ushindi huo wa Chelsea uliwapatia taji la tano la Ulaya huku ikiwa ni la kwanza tangu waliposhinda taji la Europa mjini Amsterdam 2013.

Mkufunzi Maurizio Sarri aliyejawa na hisia alisherehekea na wachezaji wake uwanjani, lakini hatma yake bado haijulikani licha ya kumaliza msimu wake wa kwanza Stamford Bridge kwa ushindi.

Kuondoka kwa Hazard kunaonekana kumekamilika na kiwango chake cha mchezo kilihakikisha kuwa mechi hiyo itakumbukwa kwa sababu za kisoka baada ya kukumbwa na siasa mbali na tatizo la tiketi na usafiri.

Mashabiki wa Chelsea ambao walifanikiwa kusafiri kwa treni ,ndege na teksi walizawadiwa na mchezo mzuri wa Chelsea kutoka kwa mchezaji ambaye ameng'ara katika klabu hiyo kwa takriban miaka saba.

Giroud anahitaji pongezi kwa kufunga goli la kwanza ambalo liliichanganya Arsenal. Lakini ni Hazard ambaye alionyesha tofauti mara ka mara msimu huu na miaka iliopita alifaa pongezi zaidi.

Huku Sarri akiweza kumaliza matatizo yake msimu huu kwa tabasamu, Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery alilazimika kutazama kwa mshangao baada ya matumaini yake ya kuipeleka timu yake kushiriki katika klabu bingwa ulaya baada ya kutoshiriki kwa misimu miwili kuangamia katika kipindi cha dakika 16.

Cech aondoka Arsenal kwa kichapo

Haki miliki ya picha PA

Hizo ndizo dakilka ambazo Chelsea walichukua kufunga magoli matatu ahsante kwa safu mbaya ya ulinzi upande wa Arsenal ambayo imeendelea kukosolewa.

Emery alishinda mataji ya Europa akiifunza Sevilla lakini kichapo hicho kina uchungu mwingi kwa kuwa kitaathiri jinsia atakavyofanya matumizi yake kuwasajili wachezaji wapya.

Gunners watarudi katika ligi ya Europa msimu ujao , lakini watacheza bila kipa Cech ambaye anatarajiwa kustaafu akiwa na umri wa miaka 37.

Iwapo atandoka basi ni nani atakayechukua mahala pake?

Mchezaji bora wa mechi-Eden Hazard Chelsea

Haki miliki ya picha Reuters

Mada zinazohusiana