Marufuku, apokonywa unahodha na tabia mbaya: Ni nini kinachoendelea katika maisha ya Neymar?

Neymar katika uanja wa mamzoezi

Mambo sio shwari kwa mchezaji huyo aliyeghali zaidi duniani kwa sasa.

Wiki hii kanda ya video iliosambazwa katika mitandao ya kijamii ilimuonyesha mshambuliaji huyo wa PSG mwenye thamani ya £200m , ambaye alikuwa katika mazoezi na Brazil katika maandalizi ya kombe la Copa America mnamo mwezi Juni akichengwa na kinda wa klabu ya Cruzeiro Weverton .

Ni wazi kusema kuwa hakufurahia.

Weverton mwenye umri wa miaka 19 aliorodheshwa katika kikosi cha mkufunzi Tite kupata uzoefu lakini akajipata ameangushwa chini na Nemyar baada ya kupitisha mpira katikati mwa miguu ya mshambuliaji huyo wa PSG.

Hatua hiyo ilijiri baada ya Neymar ambaye alikuwa amewasili katika kambi ya mazoezi ya Brazil na ndege ya aina yake yenye thamani ya £11.5m kupokonywa unahodha wa timu ya taifa baada ya misururu ya matokeo mabaya.

Mchezaji mwenza wa PSG Dani Alvez alipewa uongozi wa timu hiyo badala yake.

Haki miliki ya picha Aurelien Meunier
Image caption Dani Alves alijiunga na PSG 2017 katika drisha sawa la uhamisho na Neymar

Neymar amejipata katika maji moto msimu huu.

Mnamo mwezi Mei , shirikisho la soka nchini Ufaransa lilimpiga marufuku ya mechi tatu mchezaji huyo baada ya kumkemea shabiki wakati timu yake iliposhindwa na Renes katika fainali ya Coupe de France.

Pia anadaiwa kuhusika katika mgogoro na mchezaji mwenza katika chumba cha maandalizi baada ya PSG kushindwa na Montpellier.

Licha ya kuigharimu PSG dau la uhamisho lililovunja rekodi misimu miwili iliopita hatma ya mchezaji huyo katika klabu hiyo imezua mjadala, huku Neymar akihusishwa mara kwa mara na uhamisho wa kurudi Barcelona ama hata kuanza ukurasa mpya na klabu ya Galacticoz ya Real Madrid.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mchezaji wa zamani wa Barca na Brazil Rivaldo amependekeza kwamba Neyamar angerudi katika klabu ya Nou Camp akimtaja kuwa kiungo kilichokosekana katika harakati za mkufunzi Ernesto Vaverde kutaka kushinda kombe la mabingwa Ulaya.

Tangu ashinde kombe hilo na Barca mwaka 2015 , Neymar ameshindwa kujimudu katika michuano hiyo.

Aliondolewa katika awamu ya robo fainali na Barcelona 2016 na tangu alipowasili mjini Paris 2017, PSG imeshindwa mara mbili kuvuka robo fainali-ikishindwa na Real Madrid 2018 na Man United msimu uliopita.

Ushindi huo wa Man United ulimuweka Neymar katika shida licha ya mchezaji huyo kushindwa kushiriki katika mechi hiyo kutokana na jeraha la mguu.

Neymar alimsokoa refa kwa kuipatia Man United penalti iliojaa utata , akiutaja uamuzi huo kuwa wa aibu.

''Watu wanne ambao hawajui chochote kuhusu soka wanatazama penalti hiyo mbele ya runinga'', alisema ktika Instagram.

'Sasa beki wa PSG Presenel alitakiwa kufanya nini na mikono yake ambaye mgogo wake ulikuwa umegeuka'', ?alihoji katika mtandao wake wa Instagram.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Neymar aliwasili kwa kutumia ndege hii yenye thamani ya £11.5m katka uwanja wa mazoezi wa Brazil

Anatarajiwa kufanya nini?

Bado atasalia miongoni mwa wachezaji bora katika michuano ya Copa America mwezi Ujao, lakini mashabiki wa soka wanazidi kupoteza subira yao kutokana na vitendo vyake vya hivi karibuni.

Kuhusu iwapo ni wapi huenda Neymar akacheza soka yake baada ya michuano ya Copa America , haijulikani.

Mada zinazohusiana