Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 31.05.2019: Football gossip: Hazard, Ramos, Neymar, Rabiot, Lukaku, Sane, Sarri

Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard Haki miliki ya picha Getty Images

Real Madrid inaandaa dau jipya la £106m kumnunua mchzaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 28 na raia wa Ubelgiji Eden Hazard. (Telegraph)

Beki wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos, 33, anasema kuwa Hazard ataisaidia sana timu hiyo ya Bernabeu iwapo atahamia klabu hiyo msimu huu. (Star)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 27, anataka kurudi Barcelona msimu huu . (Sport - in Spanish)

Manchester United wanapigiwa upatu kumsaini kiungo wa kati wa PSG na Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 Adrien Rabiot, ambaye atakuwa ajenti huru kuanzia Julai mosi. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester United itamruhusu mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26 Romelu Lukaku kujiunga na Inter Milan msimu huu lakini iwapo klabu hiyo itamnunua kwa dau la £80m. (Times - subscription required)

Manchester City imekataa ombi la klabu ya Bayern Munich la £70m kumnunua winga wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23 Leroy Sane. (Guardian)

City wamewasilisha ombi la £53m kumnunua mchezaji wa Juventus mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ureno Joao Cancelo. (Tuttosport - in Italian)

Juventus wamempatia mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri kandarasi ya £6.2m kwa mwaka. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Itali Andrea Pirlo anasema kuwa alikataa uhamisho wa kuelekea Manchester City 2011, huku Chelsea ikiamua kutomsajili 2009 kwa sababu ya umri wake. (Mail)

Arsenal inamtaka winga wa Bournemouth na Uskochi Ryan Fraser, 25, lakini matumaini yao ya kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, yamedidimia baada ya kushindwa kufuzu katika kombe la mabingwa Ulaya. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 30, beki Shkodran Mustafi, 27, na raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 30, huenda ni miongoni mwa wachezaji watakaopigwa kalamu huku Arsenal ikitafuta fedha za kuimarisha kikosi chake.. (Star)

Mwenyekitiwa Liverpool Tom Werner amesema kuwa ni muhimu kwamba mkufunzi wa klabu hiyo Jurgen Klopp, ambaye amekuwa akiifunza timu hiyo tangu mwezi Oktoba 2015 anasalia katika klabu hiyo kwa muda anaotaka.. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 27, hajaamua kuhamia katika ligi ya Premia hatua itakayowacha klabu za Juventus na Napoli kushindania saini yake. (Marca)

Klabu mpya iliopandishwa daraja ili kushiriki katika mechi za Premia Aston Villa inataka ,kumsaini kiungo wa kati wa Bournemouth Harry Arter, 29, lakini huenda ikakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Fulham na Stoke katika kumsajili mchezaji huyo wa Ireland.. (Irish Independent)

Haki miliki ya picha Getty Images

Aston Villa inataka kumsaini beki wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 Tyrone Mings kwa mkataba wa kudumu kutoka Bournemouth . (Sky Sports)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez ameorodheshwa miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kuifunza klabu ya Itali Roma (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Beki wa Ufaransa na Manchester City Eliaquim Mangala, 28, anatarajiwa kurudi katika klabu ya Porto - miaka mitano baada ya kuondoka ili kuhamia kwa dau la £32m. (O Jogo - in Portuguese)