Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 01.06.2019: Sarri De Ligt, Rodri, Gundogan, Ramos, Hazard, Eriksen, Pogba, Mane, Ozil

Haki miliki ya picha Reuters

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri amekubali kuwa mkufunzi mpya wa Juventus na ameitaka Chelsea kumruhusu kuondoka.(Goal)

Sarri alimuelezea Marina Granovskaia kuhusu uamuzi wake katika mkutano siku ya Ijumaa na mkurugenzi huyo wa Chelsea aliahidi kuzungumzia hatma yake na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich. (Sky Italy - in Italian)

Chelsea inasubiri hatua rasmi kutoka kwa mabingwa hao wa Juventus , ambao watalazimika kulipa kandarasi yake ya mwaka mmoja yenye thamani ya £5m. (Guardian)

Uwanja wa Baku Haki miliki ya picha Getty Images

Mamlaka mjini Baku iliagiza kufunguliwa kwa milango katika uwanja huo katika kipindi cha kwanza cha mechi ya fainali ya kombe la ligi ya Europa dhidi ya Arsenal na Chelsea kwa kuwa waliaibishwa na ukosefu wa mashabiki katika uwanja huo.(Times - subscription required)

Beki wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, ataipatia Man United uamuzi wa uwezekano wa kuhamia katika klabu hiyo ya Old Trafford katika siku chache zijazo. (Telegraph)

Beki wa Ajax Matthijs de Ligt

Manchester City inamnyatia kiungo wa kati wa Ufaransa na Lyon mwenye umri wa miaka 22 Tanguy Ndombel epamoja na kiungo wa kati wa Uhispania Marco Llorente, 24, kama mchezaji mbadala iwapo watashindwa kumsajili kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Uhispania Rodri, 22. (Manchester Evening News)

Ilkay Gundogan atasalia katika klabu ya Manchester City msimu ujao hata iwapo kiungo huyo wa Ujerumani ,28, atakuwa ajenti huru wakati ambapo kandarasi yake itakamilika mwisho wa msimu huu.(Mail)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane amezuia kuondoka kwa beki wa Uhispania Sergio Ramos, 33, . (ESPN)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane amezuia kuondoka kwa beki wa Uhispania Sergio Ramos Haki miliki ya picha Getty Images

Real imesitisha harakati zao za kumsaka mshambuliaji wa Benfica mwenye umri wa miaka 19 raia wa Ureno Joao Felix ili kuimarisha juhudi za kuweza ikumsajili mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard. (Marca)

Rial Madrid wanatarajiwa kufanya mazungumzo na Chelsea ili kujadiliana kuhusu usajili wa Eden hazard. (Mail)

kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen

Na Real itamuwania kiungo wa kati wa Ajax na uholanzi Donny van de Beek, 22, ama kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, iwapo itashindwa kumpata kiungo wa kati wa man United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Sun)

Wakati huohuo , Juventus inamlenga kinda wa klabu ya Empoli kutoka Ivory Coast Hamed Traore kama mchezaji mbadala wa Pogba. (Calciomercato)

Arsenal na Leicester wanamchunguza winga kinda wa Valencia Uhispania Ferran Torres,19, ambaye ana thamani ya £25m. (Mail)

Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane

Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 27, anasema alikaribia kujiunga na Man United baada ya kuzungumza na mkufunzi Louis van Gaal, kabla ya simu ya Jurgen klopp kubadili mafikra yake.. (Mirror)

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery yuko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 30, mwisho wa msimu huu (Standard)

The Gunners wamewasiliana na Leicester kuhusu uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa klabu hiyo James Maddison lakini wamedaiwa kutaka kulipwa £60m. (Mail)

James Maddison Haki miliki ya picha Reuters

Barcelona ni miongoni mwa klabu zinazompigania mshambuliaji wa klabu ya Girona raia wa Uruguay 32 Cristhian Stuani, ambaye aliichezea Middlesbrough. (Marca)

Kipa wa Barcelona na Uholanzi Jasper Cillessen, 30, ameikosoa klabu hiyo kwa kuweka dau la £53million huku klabu ya Man United na Benfica zikivutiwa na mchezaji huyo. (Mail)

TETESI ZA IJUMAA

Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard Haki miliki ya picha Getty Images

Real Madrid inaandaa dau jipya la £106m kumnunua mchzaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 28 na raia wa Ubelgiji Eden Hazard. (Telegraph)

Beki wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos, 33, anasema kuwa Hazard ataisaidia sana timu hiyo ya Bernabeu iwapo atahamia klabu hiyo msimu huu. (Star)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 27, anataka kurudi Barcelona msimu huu . (Sport - in Spanish)

Manchester United wanapigiwa upatu kumsaini kiungo wa kati wa PSG na Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 Adrien Rabiot, ambaye atakuwa ajenti huru kuanzia Julai mosi. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester United itamruhusu mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26 Romelu Lukaku kujiunga na Inter Milan msimu huu lakini iwapo klabu hiyo itamnunua kwa dau la £80m. (Times - subscription required)

Manchester City imekataa ombi la klabu ya Bayern Munich la £70m kumnunua winga wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23 Leroy Sane. (Guardian)

City wamewasilisha ombi la £53m kumnunua mchezaji wa Juventus mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ureno Joao Cancelo. (Tuttosport - in Italian)

Juventus wamempatia mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri kandarasi ya £6.2m kwa mwaka. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Itali Andrea Pirlo anasema kuwa alikataa uhamisho wa kuelekea Manchester City 2011, huku Chelsea ikiamua kutomsajili 2009 kwa sababu ya umri wake. (Mail)

Arsenal inamtaka winga wa Bournemouth na Uskochi Ryan Fraser, 25, lakini matumaini yao ya kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, yamedidimia baada ya kushindwa kufuzu katika kombe la mabingwa Ulaya. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 30, beki Shkodran Mustafi, 27, na raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 30, huenda ni miongoni mwa wachezaji watakaopigwa kalamu huku Arsenal ikitafuta fedha za kuimarisha kikosi chake.. (Star)

Mwenyekitiwa Liverpool Tom Werner amesema kuwa ni muhimu kwamba mkufunzi wa klabu hiyo Jurgen Klopp, ambaye amekuwa akiifunza timu hiyo tangu mwezi Oktoba 2015 anasalia katika klabu hiyo kwa muda anaotaka.. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 27, hajaamua kuhamia katika ligi ya Premia hatua itakayowacha klabu za Juventus na Napoli kushindania saini yake. (Marca)

Klabu mpya iliopandishwa daraja ili kushiriki katika mechi za Premia Aston Villa inataka ,kumsaini kiungo wa kati wa Bournemouth Harry Arter, 29, lakini huenda ikakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Fulham na Stoke katika kumsajili mchezaji huyo wa Ireland.. (Irish Independent)

Haki miliki ya picha Getty Images

Aston Villa inataka kumsaini beki wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 Tyrone Mings kwa mkataba wa kudumu kutoka Bournemouth . (Sky Sports)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez ameorodheshwa miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kuifunza klabu ya Itali Roma (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Beki wa Ufaransa na Manchester City Eliaquim Mangala, 28, anatarajiwa kurudi katika klabu ya Porto - miaka mitano baada ya kuondoka ili kuhamia kwa dau la £32m. (O Jogo - in Portuguese)

Mada zinazohusiana