Kombe la Dunia la Wanawake 2019: Nani kunyanyua ndoo. Mtifuano kuanza leo Ufaransa

Kombe la Dunia la Wanawake linaanza leo, ni muda sasa wa kuongeza uelewa wako juu ya michuano hii.

Kama wewe ni mgeni wa michuano ya wanawake, ama ni shabiki mkubwa unayetafuta habari za ukweli za kuwashirikisha wenzako, basi fatilia kurasa hii na kuwezi kukosea!

Mashindano haya yanafanyika nchini Ufaransa kuanzia tarehe 7 mwezi huu hadi 7 Julai.

Argentina

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: hawa wanapewa nafasi ndogo ya kushinda katika kundi D wakichuana na Uingereza, Scotland na Japan. Hawa wote wameshindwa katika mechi zao sita za kombe la dunia walizocheza.

Takwimu: kama tofauti ya magoli ikizangatiwa basi, walimaliza michuano ya kombe la dunia la 2003 na 2007 na walifunga magoli mengi huku wakiwa na kadi nyekundu mbili.

Uhalisia:wamefuzu kucheza kombe hili huko Ufaransa mbali na kuwa na miaka miwili bila kuwa na michezo yoyote, hawakua na kocha, hawakua katika nafasi ya dunia na walikua na mgogoro na shirikisho la Mpira la nchini kwao juu ya suala la usawa.

Australia

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: wamefikia robo fainali katika kombe la Dunia miaka mitatu iliyopita mfululizo na wana ushawishi wa kushinda michuano hii.

Takwimu: Nahodha na mshambuliaji wao Sam Kerr ni wa kuangaliwa sana. Akiwa na miaka 25, ndio mfungaji bora katika ligi ya Marekani na Australia na pia ni mchezaji wa kike anayepewa thamani kubwa na FIFA.

Uhalisia: Akiwa na miaka 16, Matildas Mary Fowler ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika kombe la Dunia.

Brazil

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Fomiga mwenye miaka 45, amecheza Mombe la Dunia toka mwaka 1995.

Kiwango: Wamewahi kuwa washindi lakini wameshuka kutoka kwenye viwango vya Dunia kutoka nafasi ya 3 hadi nafasi ya 10. Wanashirki kombe la Dunia Wameshindwa mechi nane mfululizo.

Takwimu: Marta ni mchezaji wao wa kutegemewa. Ni mfungaji wa miaka yote katika kombe la dunia, na ametajwa kwa mara 6 kama mchezaji bora mwezi wa tisa.

Uhalisia: Marta na Cristiane wameungana na akifika miaka 41 Formiga atakua mchezaji bora katika michuano saba ya kombe la Dunia.

Kameruni

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Walikua ndio timu ya Afrika pekee kufuzu huko Canada miaka mine iliyopita. Watafanya vizuri katika michuano hii huko Ufaransa,

Takwimu: wameshindwa mechi nne tuu kati ya 14 katika mashindano makubwa.

Uhalisia: Wana jina kubwa zaidi la utani katika michuano hii, ''simba wasioshindwa''

Chile

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Javiera Grez

Kiwango: Baada ya kushindwa kufuzu kombe la dunia lilopita, timu ya wanawake ya Chile hawakucheza siku 981, sasa wamerudi katika michuano hii na wapo katika kundi F lakini wanapigiwa upatu mdogo sana wa kushinda.

Takwimu: Wamemchagua mchezaji wa miaka 17 katika kikosi chao. Elisa Duran amempita Fernanda Pinilla, ambaye pia ni Rais wa shirikisho la Mpira kwa wanawake nchini Chile.

Uhalisia: Kinda Javiera Grez ni mchezaji pekee katika kombe la Dunia akiwa na urefu nchini ya futi tano, ana futi nne.

China

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Ni waandalizi mara mbili wa michuao hiyo na waliwahi kushindwa fainali yam waka 1999, na pia waanzilishi wa soka ya wanawake. China wanatarajiwa kufika awamu ya muondoano lakini pia huenda wakachukua taji.

Takwimu: Wang Shanshan alianza kama mlinzi ,kisha akacheza namba tisa, na sasa anatumika sana katika safu ya ulinzi. Wakati mmoja aliingia uwanjani katika dakika ya 56 kama mchezaji wa ziada na kufunga mabao 9 .

Uhalisia: Jina la utani la Wang Shuang ni 'Lady Messi' kuytokana na ustadi wake kusakata kabumbu, lakini nyota wake anayemuenzi ni Cristiano Ronaldo.

England

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: The Lionesses walimaliza katika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia lililopita, sasa wanaorodheshwa wa tatu duniani na ni miongongoni mwa timu inayopigiwa upatu kushinda taji la dunia mwaka huu.

Takwimu: Karen Carney ni mchezaji wa muda mrefu wa katika kikosi hicho, tangu alipojiunga nao miaka 14 iliyopita. Ameiwakilisha nchi hiyo katika jumla ya mashindano 32 ya kimataifa- Zaidi ya mchezaji mwingine yeyote wa Uingereza, wanaume kwa wanawake..

Uhalisia: Leah Williamson, ni kiungo wa miaka 22 anayecheza safu ya kati,alikuwa anasomea uhasibu naye mlinzi Abbie McManus alikuwa akichezea timu ya Kit ya wanawake kabla Manchester City uwasajili kuwa wachezaji wa kulipwa.

Ufaransa

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Ufaransa haijawahi kupita awamu ya robo fainali katika michuano ya kombe la dunia ya wanawake lakini wenyeji hao wa mashindano hayo wameshindwa mara moja katika kipindi cha miaka miwili, kwa hivyo wanasadikiwa kuwa na uwezo kushinda taji hilo.

Takwimu: Eugenie le Sommer ni mmoja wa wachezaji saba wa Lyon katika kikosi cha Ufaransa. Mshambuliaji huyu amefunga mabao 73 katika michezo 156 na ameshindia klabu mataji sita ya klabu bingwa barani

Uhalisia: Mlinzi Wendie Renard ni mchezaji mrefu Zaidi katika mashindano hayo, futi 6 na ichi 1.

Ujerumani

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Ni washindi mara mbili wa taji la dunia, lakini Ujerumani hawafuzu kwa fainali ya kombe la dunia katika mashindano mawili yaliyopita, lakini wanaingia katika mashindano haya wakiwa hajafungwa katika mechi 13.

Takwimu: Kocha Martina Voss-Tecklenburg ameteua wachezaji 9 kutoka kikosi kilichoshinda dhahabu ya Olympiki katika michezo ya Rio mwaka 2016, ikiwa ni pamoja na Dzsenifer Marozsan, ambaye anasadikiwa kuwa mchezaji bora duniani anayecheza safu ya kati.

Uhalisia: Kikosi chao kilitoa kanda ya video iliyowaonesha historia ya kila mchezaji na pandashuka walizopitia katika soka la wanawake, video hiyo ilipata umaarufu mkubwa katika mitandao ya kijamii na ilipata maoni Zaidi ya milioni tatu.

Italia

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Hii ni mara ya kwanza kikosi hiki kimefuzu kwa kombe la dunia katika kipindi cha mika 20 lakini wengi wanatilia shaka kama watafikia awamu ya muondoano.

Takwimu: Wachezaji wawili wa klabu ya Italia ya AC Milan, Valentina Giacinti na Daniela Sabatini walikuwa wafungaji hodari wakuu katika ligi ya Serie A msimu uliyopita.

Uhalisia: Unaweza kumnunua nahodha Sara Gama kama mwanaserere wa Barbie aliyetunukiwa kama sehemu ya kumuenzi kama 'shujaa' kwa kujitua kimasomaso kuunga mkono hadharani usawa na wa.

Jamaica

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwngo : Jamaica inatajwa kuwa timu iliyoorodheshwa katika kiwango cha chini kwenye michuano ya kombe la dunia la wanawake lakini kocha wake anaamini kuwa kikosi chake kitafika awamu ya muondowano.

Takwimu: Khadija 'Bunny' Shaw, mhitimu kutoka chuo kikuu cha Tennessee, amefunga mabao 19 katika michuano 12 ya kufuzu kwa fainali ya kombe hili

Uhalisia: Timu hii ya kitaifa ilianza tena kushiriki michuano hii mwaka 2014 baada ya mapumziko miaka, pongezi zimuendee balozi na mdhamini Cedella Marley, ambaye nib inti wa mwanamuziki maarufu marehemu Bob Marley.

Japan

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Mabingwa hao wa mwaka 2011 wanasalia kuwa kikosi kilichofuzu kwa fainali ya kombe la dunia ya wanawake mara tatu mfululizo bna bila shaka watashindania taji hilo katika kundi D na England.

Takwimu: Wana timu ya wachezaji chipukizi - 14 kati yao wako chini ya miaka 24 na pia wana matineja wawili

Uhalisia: Wachezaji 10 katika kikosi hicho ni wachezaji wenza katika klabu ya Nippon TV Beleza ya shirika kuu la ndege la Japan.

New Zealand

Haki miliki ya picha Getty Images

Form: New Zealand ilikuwa timu ya mwisho kufuzu kwa kombe la duni na wamefunga jumla ya mabao 43 katika safari yao kuelekea Ufaransa, lakini walimaliza wa mwisho katika awamu ya makundi katika michuano mine ya kombe makombe ya dunia yaliyopita.

Takwimu: Ali Riley na Abby Erceg wameche za kila dakika ya kikosi cha New Zealand katika fainali tisa ya kombe la dunia iliyopita tangu mwaka 2007 lakini hawajawahi kishinda hata moja katika michuano hiyo.

Uhalisia: Wachezaji 12 waliondoka katika kikosi hicho mwaka jana kufuatia madai ya unyanyasaji wa kocha Andreas Heraf. Tayari Tom Sermanni ambaye ni mzaliwa wa Glasgow-amechukua nafasi yake .

Uholanzi

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Mabingwa hao wa Ulaya ni miongoni mwa vikosi vinavyoangaliwa Ufaransa japo walihitaji kujikakamua zaidi kufuzu kwa michuano yay a fainali ya kombe la.

Takwimu: Vivianne Miedema alikuwa mfungaji bora wa mabao katika michuano ya wanawake ya Super League kwa Arsenal na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa PFA. Akiwa na miaka 22 pekee tayari ameishindia nchi yake mataji 75.

Uhalisia: Miedema ni mwandishi wa makala ya uhalisia wa vichekesho.

Nigeria

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Nigeria wamefuzu kwa kila kombe la dunia ya wanawake lakini walipita mara moja tu awamu ya muondoano na mara hii wako kundi moja na Ufaransa

Takwimu: Nigeria wamepoteza jumla ya mechi 16 za kombe la dunia na kufungwa mabao 56. Lakini tarajia mashambulizi makali kutoka kwa wachezaji waliyojumuishwa katika kikosi hiki.

Uhalisia: Mshambuliaji wao wa miaka 19 Rasheedat Ajibade ni bingwa mtindo wa freestyle.

Norway

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Walishinda taji hili mwaka 1995 na wamefuzu katika kila shindano lakini timu hii ya sasa huenda isifanye mabadiliko.

Takwimu: Winga Caroline Graham Hansen aliichezea Norway akiwa na miaka 16 na sasa akiwa na miaka 24, ameshinda zaidi ya mataji 70.

Uhalisia: Miaka miwili baada ya mshindi wa Ballon d'Or Ada Hegerberg anaondoka katika kikosi hicho kutokana na masuala ya usawa katika shirikisho la soka la Norway. Cham cha kitaifa cha wachezaji kilifanikiwa kutia saini makubaliano ya kihistoria ya malipo sawa ambayo iliwawezesha wachezaji wa kike kupata mara mbili ya mshahara waliyokuwa wakilipwa hadi euro 574,540.

Uskochi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Claire Emsile

Kiwango: Uskochi pia itakuwa mara yao ya kwanza kufuzu kwenye michuano hii. Lakini wana kiwango kizuri, hawajafungwa hata mchezo mmoja kwenye mechi tano zilizopita.

Takwimu: Kiungo na nahodha msaidizi, Kim Little ameshinda makombe matatu na vilabu vya mabara matatu tofauti, Seattle Reign ya Marekani, Melbourne City ya Australia na hivi karibuni na Arsenal ya England.

Uhalisia: Mshambuliaji kinara Claire Emslie amechorwa picha kubwa ya kumuenzi katika moja ya mitaa nchini kwao kutokana na kiwango chake.

Sweden

Haki miliki ya picha Sweden National Team

Kiwango: Washindi wa pili katika michuano ya mwaka 2003, wapo kayika nafasi ya tisa kwenye viwango vya ubora japo wameshinda mechi mbili tu katika michuano mikubwa mitatu iliyopita. Hata hivyo wanatarajiwa kufuzu kwenye Kundi F.

Takwimu: Kiungo Caroline Seger amekuwa nahodha wa timu hiyo kwa miaka 10, huku beki Nilla Fischer, ambaye pia ana miaka 34, atacheza michuano yake ya nne ya Kombe la Dunia.

Uhalisia: Jezi za timu hiyo zinajumuisha picha za baadhi ya wanawake mashujaa wa nchi hiyo.

Afrika Kusini

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha Desiree Ellis alikuwa ni moja ya wachezaji wa kwanza wa kikosi cha kwanza cha wanawake cha Afrika Kusini.

Kiwango: Afrika Kusini ni moja ya mataifa manne ambayo yamefuzu kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo. Watakuwa na kibarua kizito watakapokutana na Ujerumani, Uhispania na Uchina katika kundi B.

Stat: Mshambuliaji Thembi Kgatlana alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika 2018 na kushinda Kiatu cha Dhahabu katika michuano ya bara hilo.

Uhalisia: Kocha Desiree Ellis alikuwa ni moja ya wachezaji wa kwanza wa kikosi cha kwanza cha wanawake cha nchi hiyo.

Korea Kusini

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Korea Kusini walifanikiwa kutinga hatua ya mtoano mwaka 2015 lakini wameshinda mechi moja tu katika saba za kufuzu Kombe la Dunia na kupita kwa tofauti ya magoli.

Takwimu: Mshambuliaji Ji So-yun alikuwa ni mchezaji mdogo zaidi wa taifa hilo kufunga goli akiwa na miaka 15 mwaka 2006. Kwa sasa ndiye mfungaji bora zaidi wa kipindi chote na aeshatunukiwa mchezaji bora mara mbili akiwa na klabu ya Chelsea ya England.

Uhalisia: Mahabiki 40,000 walijitokeza kushuhudia mchezo wa Korea Kusini na Korea Kaskazini jijini Pyongyang, amchezo ulioishia kwa sare ya 1-1.

Uhispania

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jorge Vilda ndiye kocha bora wa wanawake kwa 2018

Kiwango: Uhispania hawajafungwa hata mechi moja kwa mwaka 2018 - na wana rekodi ya ushindi 100% wakati wa kufuzu, lakini huwa hawafui dafu mbele ya vigogo kama England na Marekani. Yawezekana wakafuzu kwa mara ya kwanza katika hatua ya mtoano.

Takwimu: Mshambuliaji kinara wa Atletico Madrid Jennifer Hermoso ameshinda kiatu cha dhahabu wakati timu hiyo ikichukua ubingwa wa ligi. Katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia, amefunga magoli saba na kutoa pasi za mwisho tisa.

Uhalisia: Akiwa na miaka 37, kocha wa Uhispania Jorge Vilda ndiye kocha mdogo zaidi katika michuano hiyo. Atatimza 38 siku ya fainali.

Thailand

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiwango: Mwaka 2015 walifungwa goli 4-0 dhidi ya Ujerumani na Norway kwenye hatua ya makundi. Safari hii wanakutana kwanza na mabingwa Marekani. Hawatarajiwi kufika hatua ya mtoano.

Takwimu: Mshambuliaji wao Orathai Srimanee ndiye mchezaji pekee amabye amewahi kufunga goli katika michuano ya Kombe la Dunia.

Uhalisia: Timu hiyo inaitwa kwa jina la utani la Chaba Kaew wakifananishwa na ndovu wa kike mwenye rangi ya pinki kwenye filamu ya wanyama maarufu iitwayo Khan Kluay.

Marekani

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marekani waliwanyuka Japan 5-2 na kunyakua kikombe 2015.

Kiwango: Ndio mabingwa watetezi, timu bora zaidi kwa kiwango duniani, na wanapigiwa upatu kunyakua tena kombe. Wamarekani hawajawahi kumaliza chini ya nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia.

Takwimu: Marekani hawajawahi kufungwa mchezo wowote pale Alex Morgan alipofunga goli. Mchezaji huyo mwenye miaka 30 anayekipiga na Orlando Pride amefunga magoli 101 katika michezo 163.

Uhalisia: Sura za wachezaji wa zimebandikwa kila kona jijini New York na Los Angeles ikiwa ni sehemu ya kampeni ya matangazo ya Nike mwezi uliopita. Ni maarufu kiasi kwamba sura zao zipo kwenye majengo marefu na mabango makubwa.

Mada zinazohusiana