Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 09.06.2019: Mourinho, Bale, Lingard, Ake, Buffon, Koulibaly

Mourinho Haki miliki ya picha Getty Images

Kocha Jose Mourinho amewaambia rafiki zake kuwa anaweza kwenda kuifunza klabu ya Newcastle na yupo tayari kufanya mazungumzo na anayetarajiwa kuinunua klabu hiyo Sheikh Khaled bin Zayed Al Nehayan. (Sunday Mirror)

Kiungo wa England Jesse Lingard, 26, anakaribia kuongeza mkataba na kupata mshahara wa pauni 130,000 kwa wiki katika klabu ya Manchester United. (Sun on Sunday)

Man United bado wana mpango wa kumsajili beki wa Leicester na England Harry Maguire, 26, pia beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30. (Sunday Express)

Manchester United inataka kumsajili kwa mkopo winga wa Real Madrid raia wa Wales Gareth Bale, 29. (Sunday Mirror)

Arsenal wapo karibu kuwasajili wachezaji wawili kutoka klabu ya Sampdoria ya Italia kiungo Mbelgiji Dennis Praet, 25, na beki wa kati raia wa Denmark Joachim Andersen, 23. (Gazzetta dello Sport, via Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Man United wamekuwa wakimuwania Koulibaly kwa muda sasa.

Manchester United wamepeleka dau la pauni milioni 84m kwa klabu ya Napoli wakitaka kumsajili beki raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 27. (Corriere dello Sport, via Mail)

Winga wa Dalian Yifang ya Uchina Mbelgiji Yannick Carrasco, 25, anakaribia kusajiliwa na Arsenal. (Sport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tottenham wanamsaka Ake kwa udi na uvumba

Tottenham wanatarajiwa kutoa dau la pauni milioni 40 ili kumsajili mlinzi wa will Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24. (Sun on Sunday)

Liverpool wapo tayari kumuuza winga wao raia wa Wales Harry Wilson, 22, kwa dau la pauni milioni 21. Winga huyo aliitumikia kwa mkopo klabu ya Derby msimu uliopita. Klabu mbili za Ujerumani Hoffenheim na RB Leipzig zinaripotiwa kumnyemelea winga huyo. (Sunday Mirror)

Golikipa mkongwe wa Italia Gianluigi Buffon, 41, anaweza kurejea kwenye klabu yake ya kwanza Parma baada ya kutangaza kuwa ataachana na klabu ya Paris St-Germain. (La Gazzetta dello Sport, via Goal - in Italian)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gigi Buffon ametangaza kuachana na klabu ya PSG

David Beckham anataka beki wa kulia raia wa Ecuador Antonio Valencia, 33, tajiunge na klabu yake ya Inter Miami ya nchini Marekani. Valencia ameondoka Manchester United mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kumaliza mkataba wake na Mashetani hao Wekundu. (Sun on Sunday)

Rais wa klabu ya Benfica Luis Filipe Vieira amesema namna pekee ya klabu hiyo kumbakiza mshambuliaji wao kinda na nyota Joao Felix, 19, ni kwa kumuuza kisha kumuomba kwa mkopo msimu ujao. Klabu za Manchester United na Manchester City tayari zinamuwinda mchezaji huyo raia wa Ureno. (Sunday Mirror)

Kiungo wa Manchester United na Brazil Andreas Pereira, 23, anakaribia kusaini nyongeza ya mkataba kwa miaka minne na klabu hiyo yenye maskani yake katika uga wa Old Trafford. (Sun on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bakayoko aliitumikia AC Milan kwa mkopo msimu uliopita.

Kiungo wa klabu ya Chelsea na Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, anataka kubaki Chelsea msimu ujao baada ya kutolewa kwa mkopo msimu uliopita katika klabu ya AC Milan. (L'Equipe - in French)

Arsenal hawatarajiwi kufanya usajili golikipa katika dirisha hili la usajili licha ya kipa wao mkongwe raia wa Jamuhuri ya Czech Petr Cech, 37, kustaafu kandanda. (Sunday Mirror)

Tetesi Bora za Jumamosi

Image caption Real Madrid wanafikiria kuacha kumsajili Pogba na badala yake wamnase Eriksen kutoka Tottenham.

Real Madrid itafikiria kumsaini kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, badala ya kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba. (Independent)

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri atatia saini kandarasi ya miaka mitatu ili kuchukua wadhfa wa kuifunza Juventus wiki ijayo (Guardian)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Eric Dier, 25, anafikiriwa na Manchester United kukaza safu ya kati kwenye kikosi cha kwanza cha wachezaji 11. (Times - subscription required)

Image caption Je Eric Dier atakubali kujiunga na Mashetani Wekundu?

Barcelona imekataa ripoti kwamba itamnunua kipa Gianluigi Buffon baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41- kutangaza kwamba ataondoka Paris Saint Germain mwisho wa msimu huu (Mundo Deportivo - in Spanish)

Winga wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe atakataa ombi la kucheza katika ligi ya Uingereza na badala yake kuelekea Bayern Munich. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ananyatiwa na Liverpool na Manchester United. (Sun)

Mada zinazohusiana