Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 08.06.2019: Sarri, Eriksen, Dier, Meunier, Buffon, Rashford, Alonso, Sessegnon

Real Madrid itafikiria kumsaini kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, badala ya kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba. (Independent)

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri atatia saini kandarasi ya miaka mitatu ili kuchukua wadhfa wa kuifunza Juventus wiki ijayo (Guardian)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Eric Dier, 25, anafikiriwa na Manchester United kukaza safu ya kati kwenye kikosi cha kwanza cha wachezaji 11. (Times - subscription required)

Eric Dier

Barcelona imekataa ripoti kwamba itamnunua kipa Gianluigi Buffon baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41- kutangaza kwamba ataondoka Paris Saint Germain mwisho wa msimu huu (Mundo Deportivo - in Spanish)

Marco Alonso

Buffon anataka kustaafu katika soka baada ya kushinda dhahabu katika michezo ya Olimpiki akiichezea Itali katika mashindano hayo yatakayofanyika nchini Japan(Gazzetta dello Sport, via Mail)Barcelona itamwania mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 21, iwapo itashindwa kumsajili Antoine Griezmann au Neymar. (Mail)Atletico Madrid inataka kumsajili beki wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 28, ili kumrudisha nyumbani  (Goal)

Mchezaji wa Fulham na Uingereza Ryan Sessegnon, 19, ameambia klabu hiyo hatosaini kandarasi mpya na kwamba anaelekea Tottenham (Guardian)

Bruno fernandez Haki miliki ya picha AFP

Liverpool itashindana na Tottenham na Manchester United katika kumsaini kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 24 na raia wa Ureno Bruno Fernandes kutoka Sporting Lisbon. (Record, via Mirror)

Winga wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe atakataa ombi la kucheza katika ligi ya Uingereza na badala yake kuelekea Bayern Munich. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ananyatiwa na Liverpool na Manchester United. (Sun)

Dennis Praet Haki miliki ya picha Getty Images

Arsenal wameambiwa watalazimika kuilipa Sampdoria £44m ili kumnunua mchezaji mwenye umri wa miaka 22-beki wa Itali Joachim Andersen na winga wa Ubelgiji Dennis Praet, 25. (Star)West Ham na Arsenal note wanamtaka king wa kati wa  Eibar na Uhispania Joan Jordan, 24. (Marca - in Spanish)

West Ham wanamnyatia mchezaji wa  Newcastle na nyota wa Uingereza 21 Isaac Hayden, 24. (Star)

Everton imejiunga na Arsenal Katia harakati za kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 27 beki wa Togo defender Djene Dakonam kutoka Getafe. (Marca - in Spanish)

TETESI ZA IJUMAA

Joao Cancelo

Beki wa kulia wa Juventus na Ureno, Joao Cancelo, 25, anaweza kuwa njiani kuelekea Manchester City kwa gharama ya pauni milioni 44- ikiwa the blues wanamuuza beki wa pembeni Danilo, 27.(Goal)

Mshambuliaji wa Brazil, Neymar amekataa kuelekea Real Madrid na kuiambia Paris Saint-Germain kuwa anataka kuelekea Barcelona tu . (Express)

Tottenham imepewa ofa ya mchezaji wa kijerumani na mshambuliaji wa Paris St-Germain,Julian Draxler,25, kama mbadala wa Christian Eriksen ikiwa mchezaji huyo, 27, ataondoka. (Star)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Matthijs de Ligt, 19 huenda akachagua kuichezea Paris St-Germain au Barcelona. (Marca)

Mashetani wekundu wanalenga sahihi mbili kubwa mwezi huu.(Sun)

Haki miliki ya picha Reuters

Wakati huohuo, kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans,22, ambaye alitumia msimu uliopita akiichezea Leicester kwa mkopo akitokea Monaco, anahitajika Old Trafford ikiwa Paul Pogba, ataamua kuondoka United.(Independent)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Foxes na Uingereza, Harry Maguire, 26,anajiandaa kuikacha Manchester United, na kuwa na mpango wa kwenda Manchester City. (Mail)

Na kiungo wa kati wa Leicester City, James Maddison anataka kuendelea kubaki King Power, ingawa Manchester United na Tottenham zina nia ya kumchukua. (Mail)

Paris Saint-Germain huenda wakatoa ofa kumnasa kiungo wa kati wa Everton, Idrissa Gueye. (Le 10 Sport)

Everton wameiambia Tottenham wanamtaka beki wa kushoto Danny Rose, 28, ili kumuachia Lucas Digne, 25,aondoke Goodison Park. (Star)

Winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco, 25, karibu atahamia Arsenal kutoka timu ya Dalian Yifang ya uchina.(Mirror)

Mchezaji wa nafasi ya Joachim Andersen,23, huenda akachagua kwenda AC Milan badala ya Arsenal kama meneja wake wa timu anayoichezea sasa Sampdoria, Marco Giampaolo ataamua kuelekea Rossoneri. (Metro)

Schalke wako kwenye kinyang'anyiro cha kupata saini ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi ya Everton Jonjoe Kenny,22, kwa mkopo.(Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon, 29, anajiandaa kuzungumza na Fenerbahce baada ya mipango ya Newcastle kumpata kwa mkopo kutoka West Brom kugonga mwamba. (Sun)

Mada zinazohusiana