Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 10.06.2019: De Gea, Wan-Bissaka, Meunier, Silva, Sessegnon, Butland

Manchester United itampa David de Gea £20m iwapo kipa huyo ataelekea Paris St-Germain Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United itampa David de Gea £20m iwapo kipa huyo ataelekea Paris St-Germain

Manchester United itampa kipa wa Uhispania David de Gea £20m iwapo mchezaji huyo mwenye miaka 28 ataelekea Paris St-Germain msimu huu wa joto. (Sun)

United imekataliwa ombi lake na Crystal Palace la thamani ya £40m kumsajili mchezaji wa timu ya taifa ya England ya wachezaji wa chini ya miaka 21 Aaron Wan-Bissaka. Timu hiyo ya Eagles inataka takriban £60m. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amefanya mazungumzo na beki wa kulia wa PSG na timu ya taifa ya Ubelgiji Thomas Meunier, mwenye umri wa miaka 27, kuhusu uwezekano wa kuhama msimu huu wa joto.(Express)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City David Silva, mwenye umri wa miaka 33, atashiriki katika mechi ya mtihani uwanjani Etihad Stadium mwakani. Mkataba wa mchezaji huyo wa Uhispania unamalizika mwaka ujao na anataka asitishe kazi yake huko Las Palmas. (Sun)

Tottenham itawasilisha ombi kwa Fulham kumwania winga wa timu ya taifa ya England ya wachezaji wasiozidi miaka 21 Ryan Sessegnon, mwenye umri wa miaka 19, msimu huu wa joto. (Football.London)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkataba wa mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City David Silva unamalizika mwaka ujao

Chelsea imefufua hamu yake ya kutaka kumsajili winga wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Jamaica Leon Bailey, mwenye umri wa miaka 21, lakini ni lazima isubiri kuona iwapo marufuku iliyopewa ya uhamisho wa wachezaji itabatilishwa kabla ya kuwasilisha ombi hilo. (Mail)

Arsenal ina hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Fiorentina Jordan Veretout, mwenye umri wa miaka 26, lakini mchezaji huyo wa zamani wa timu ya tiafa ya Ufaransa ya wachezaji wasiozidi miaka 21 tayari anafanya mazungumzo na Napoli. (L'Equipe)

Newcastle na Southampton zimewasilisha ombi kwa mshambuliaji wa Mainz na timu ya taifa ya Ufaransa ya wachezaji wasiozidi miaka 21 Jean-Philippe Mateta, aliye na miaka 21. (L'Equipe, kupitia Sport Witness)

Arsenal inataka kumsajili mlinzi wa Saint Etienne William Saliba, mwenye miaka 18, lakini timu hiyo ya Ligue 1 inataka kumchukua kwa mkopo msimu ujao wa joto. (Football.London)

Haki miliki ya picha JEAN-PHILIPPE KSIAZEK
Image caption Newcastle na Southampton zimewasilisha ombi kwa mshambuliaji wa Mainz Jean-Philippe Mateta

Stoke inatisha £23m ili kumuuza kipa wa timu ya taifa wa England Jack Butland, mwenye umri wa miaka 26. (Sun)

Mshambuliaji wa Fulham na Serbia Aleksandar Mitrovic, mwenye umri wa miaka 24, analengwa na West Ham. (Mail)

West Ham ipo tayari kushindana na Arsenal na Tottenham kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Atalanta na timu ya taifa ya Ivory Coast Franck Kessie. Mchezaji huyo wa miaka 22 amekuwa akicheza kwa mkopo huko AC Milan tangu 2017. (Express)

Leicester itaendelea na mazungumzo na Luton Town kuhusu kumsajili beki kamili mwenye miaka 21 James Justin. (Mail)

Aliyekuwa kipa wa Manchester United Anders Lindegaard anasema David Moyes kupewa fursa kumpokea Sir Alex Ferguson huko Old Trafford ni kama "kuchaji simu ya iPhone kwa chaja ya Nokia ". (Standard)

Leeds imewasilisha maombi kwa Liverpool kuonyesha hamu ya kutaka kawasajili winga Harry Wilson na Ryan Kent, wote wenye miaka 22. (Football Insider)

Tetesi bora kutoka Jumapili:

Haki miliki ya picha Getty Images

Kocha Jose Mourinho amewaambia rafiki zake kuwa anaweza kwenda kuifunza klabu ya Newcastle na yupo tayari kufanya mazungumzo na anayetarajiwa kuinunua klabu hiyo Sheikh Khaled bin Zayed Al Nehayan. (Sunday Mirror)

Kiungo wa England Jesse Lingard, 26, anakaribia kuongeza mkataba na kupata mshahara wa pauni 130,000 kwa wiki katika klabu ya Manchester United. (Sun on Sunday)

Man United bado wana mpango wa kumsajili beki wa Leicester na England Harry Maguire, 26, pia beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30. (Sunday Express)

Manchester United inataka kumsajili kwa mkopo winga wa Real Madrid raia wa Wales Gareth Bale, 29. (Sunday Mirror)

Arsenal wapo karibu kuwasajili wachezaji wawili kutoka klabu ya Sampdoria ya Italia kiungo Mbelgiji Dennis Praet, 25, na beki wa kati raia wa Denmark Joachim Andersen, 23. (Gazzetta dello Sport, via Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Man United wamekuwa wakimuwania Koulibaly kwa muda sasa.

Manchester United wamepeleka dau la pauni milioni 84m kwa klabu ya Napoli wakitaka kumsajili beki raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 27. (Corriere dello Sport, via Mail)

Winga wa Dalian Yifang ya Uchina Mbelgiji Yannick Carrasco, 25, anakaribia kusajiliwa na Arsenal. (Sport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tottenham wanamsaka Ake kwa udi na uvumba

Tottenham wanatarajiwa kutoa dau la pauni milioni 40 ili kumsajili mlinzi wa will Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24. (Sun on Sunday)

Liverpool wapo tayari kumuuza winga wao raia wa Wales Harry Wilson, 22, kwa dau la pauni milioni 21. Winga huyo aliitumikia kwa mkopo klabu ya Derby msimu uliopita. Klabu mbili za Ujerumani Hoffenheim na RB Leipzig zinaripotiwa kumnyemelea winga huyo. (Sunday Mirror)

Golikipa mkongwe wa Italia Gianluigi Buffon, 41, anaweza kurejea kwenye klabu yake ya kwanza Parma baada ya kutangaza kuwa ataachana na klabu ya Paris St-Germain. (La Gazzetta dello Sport, via Goal - in Italian)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gigi Buffon ametangaza kuachana na klabu ya PSG

David Beckham anataka beki wa kulia raia wa Ecuador Antonio Valencia, 33, tajiunge na klabu yake ya Inter Miami ya nchini Marekani. Valencia ameondoka Manchester United mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kumaliza mkataba wake na Mashetani hao Wekundu. (Sun on Sunday)

Rais wa klabu ya Benfica Luis Filipe Vieira amesema namna pekee ya klabu hiyo kumbakiza mshambuliaji wao kinda na nyota Joao Felix, 19, ni kwa kumuuza kisha kumuomba kwa mkopo msimu ujao. Klabu za Manchester United na Manchester City tayari zinamuwinda mchezaji huyo raia wa Ureno. (Sunday Mirror)

Kiungo wa Manchester United na Brazil Andreas Pereira, 23, anakaribia kusaini nyongeza ya mkataba kwa miaka minne na klabu hiyo yenye maskani yake katika uga wa Old Trafford. (Sun on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bakayoko aliitumikia AC Milan kwa mkopo msimu uliopita.

Kiungo wa klabu ya Chelsea na Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, anataka kubaki Chelsea msimu ujao baada ya kutolewa kwa mkopo msimu uliopita katika klabu ya AC Milan. (L'Equipe - in French)

Arsenal hawatarajiwi kufanya usajili golikipa katika dirisha hili la usajili licha ya kipa wao mkongwe raia wa Jamuhuri ya Czech Petr Cech, 37, kustaafu kandanda. (Sunday Mirror)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii