Jan Oblak wa Atletico Madrid ajiandaa kuhamia Manchester united

Swala la kwamba Oblak ana miaka 26 tu linaweza kuwa kichocheo cha Manchester United kuamua kumchukua Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Swala la kwamba Oblak ana miaka 26 tu linaweza kuwa kichocheo cha Manchester United kuamua kumchukua

Mlindalango wa Atletico Madrid Jan Oblak anajiandaa kuhamia katika timu 'aliyoichezea utotoni' Man Utd

Manchester United inakabiliwa na hali halisi ya kumpoteza mlindalango wao wa muda mrefu David De Gea msimu huu.

Mkataba wa Muhispania huyo unafikio ukingoni 2020 na hajaonyesha dalili zozote za kusaini mkataba mpya na Mashetani wekundu.

De Gea amekuwa ni mchezaji mahiri na kiungo muhimu sana katika klabu ya Manchester United katika enzi ya baada ya Sir Alex Ferguson , lakini alikabiliwa na misukosuko si haba katika msimu wa 2018/19.

Lakini licha ya makosa aliyoyafanya, bado hadhi yake ni kubwa na kuna tetesi kuwa timu ya Ufaransa Paris Saint-Germain iko msari wa mbele miongoni mwa timu ambazo zimeazimia kusaini nae mkataba.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption PSG ya Ufaransa na Juventus zimekwisha onyesha azma kubwa ya kumnunua David De Gea

Kwa hiyo swali ni nani ambaye Manchester United wanamleta kuchukua nafasi ya yake bila matarajio ya Ligi ya Soka ya Championi 2019/20? , anaweza kuwa ni Jan Oblak wa Atletico Madrid.

Meneja Ole Gunnar Solskjaer anacho kibarua kikubwa msimu huu cha kujenga kikosi cha United baada ya kushindwa kwa timu hiyo msimu huu ambapo klabu yake ilishinda michezo miwili tu katika fainali 12.

Tayari raia huyo wa Norway amekwishaanza kazi , huku Daniel James akiwa tayari amesaini mkataba na kikosi hicho kutoka Swansea akitarajiwa kuidhinishwa rasmi wiki hii, lakini bado anayo kazi ya kufanya , na moja ya kibarua kinachomfanya akune kichwa bila shaka ni kumtafuta mlindalango mpya.

Kumpata David De Gea siku za usoni bila shaka ni jambo la mashaka kwani Muhispania huyo anaingia mwaka wake wa mwisho wa mkataba na Manchester United msimu huu na kuna tetesi zilizoshamiri sana zinazomuhusisha kuondoka Old Trafford, huku PSG na Juventus zikisema zinamtaka kwa hamu kubwa.

Image caption Meneja wa manchester United Ole Gunnar Solskjaer anacho kibarua kikubwa msimu huu cha kujenga kikosi cha United ambacho kilifanya vibaya msimu huu

Angependelea kubaki chini ya Ole Gunnar Solskjaer kuliko kwenda PSG.

Swala la kwamba Oblak ana miaka 26 tu linaweza kuwa kichocheo cha Manchester United kuamua kumchukua.

Kama watakubaliana vizuri huenda wanaweza kumpatia mkataba walau wa miaka 10.

Oblakalisaini mkataba na Atleticomwaka huu hadi 2023, wenye kipengele ckinachomuwezesha kuchezea timu nyingine kwa thamani ya Euro milioni €120m, kulingana na gazeti la Mirror.

Hawezi kununuliwa kwa bei ya chee, bali atatumia njia zote kupata kila senti.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Daniel James kutoka Swansea tayari amekwisha saini mkataba na klabu ya Manchester United

Kile ambacho manchester United watahitaji kumkaribisha ni walau kuongeza sura mpya kikosini hususan upande wa safu ya ulinzi - ili kuimarisha ukuta wa safu ya ulinzi mbele yake atakapokuwa golini.

Wanaweza kuanza kwa kumtafuta kiungo mpya wa safu ya nyuma-kati- na nyuma-kulia , kwasababu hata Oblak hawezi kuziba pengo la safu ya ulinzi peke yake.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii