Tetesi za soka Ulaya Ijumaa tarehe 14.06.2019: Fekir, Pogba, Lukaku, Walker, Rakitic

Liverpool hawana mpango wa kufufua mpango mkataba na mchezaji wa Lyon Nabil Fekir
Maelezo ya picha,

Liverpool hawana mpango wa kufufua mpango mkataba na mchezaji wa Lyon -Nabil Fekir

Liverpool hawana mpango wa kufufua mpango mkataba na mchezaji wa Lyon Nabil Fekir, mwenye umri wa miaka 25, licha ya madai hayo yanayotolewa na Ufaransa. (Independent)

Mkurugenzi wa mchezo wa Juventus Fabio Paratici amesafiri kuelekea katika ofisi za Manchester United mjini London kwa ajili ya mazungumzo ya ana kwa ana juu ya uhamisho wa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26. (Sky Sports Italy via Sky Sports).

Maelezo ya picha,

Mkurugenzi wa Juventus Fabio Paratici amesafiri hadi mjini London kwa ajili ya mazungumzo ya ana kwa ana juu ya uhamisho wa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba

Mshambuliaji wa Manchester United na Ubelgiji Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 26, amekubali mkataba wa kibinafsi na Inter Milan katika mkataba unaoweza kumlipa nyota huyo pauni milioni 6.6 za mafao hadi mwaka 2024. (Gazzetta dello Sport via Metro)

kiungo wa kati-kulia wa Crystal Palace Muingereza Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 21, anapendelea kuhamia Manchester United msimu huu. Palace wanamthamanisha mchezaji huyo wa safu ya ulinzi kwa kiwango cha pauni milioni 70 . (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Manchester City wamekuwa wakisita kukubali thamani pauni milioni 90 ya mchezaji wa safu ya kati-nyuma Harry Maguire

Manchester City wamekuwa wakikataa kukubali thamani pauni milioni 90 ya mchezaji wa safu ya kati-nyuma Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 26 iliyowekwa na Leicester na kusema kuwa pendekezo la uhamisho wake limesitishwa kwa muda. (Daily Mail)

Meneja wa Barcelona Ernesto Valverde atamruhusu kiungo wa kati wa timu hiyo Mcroatia Ivan Rakitic, mwenye umri wa miaka 31, aondoke kwenye klabu hiyo kama timu atapata timu inayomfaa ya kumchukua . (Cadena SER - in Spanish)

Arsenal wanakamilisha mkataba kwa ajili ya mlindalango Mjerumani Markus Schubert, mwenye umri wa miaka 21, kutoka klabu ya Dynamo Dresden. (Independent)

Kiungo wa safu nyuma wa Manchester City -Kyle Walker,mwenye umri wa miaka 29, amekamilisha taratibu za kusaini mkataba mpya baada ya kurejesha mahusino mazuri na meneja Pep Guardiola. (Mirror)

Maelezo ya picha,

Romelu Lukaku, amekubali mkataba wa kibinafsi na Inter Milan katika mkataba unaoweza kumlipa nyota huyo pauni milioni 6.6 za mafao

Borussia Dortmund wanamfuatilia kwa karibu mlinzi wa Arsenal defender Laurent Koscielny, mwenye umri wa miaka 33, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka msimu huu . (Daily Mail)

Everton na Paris Saint-Germain wamo katika harakati za kumsaka mshambuliaji David Neres raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 22 anayechezea klabu ya Ajax. (Esporte - Spanish)

Winga wa Bournemouth -Ryan Fraser, mwenye umri wa miaka 25, amedokeza kuwa ataendelea kubaki katika klabu hiyo kwa mwaka mwingine zaidi licha ya kwamba anngependa kuchezea Arsenal. (mirror)

kiungo wa kati wa Paris Saint-Germain Adrien Rabiot, mwenye umri wa miaka 24, canaweza kuendelea kuwa katika klabu hiyo licha ya kuwekwa benchi kwa kipindi karibu chote cha pili cha msimu uliopita. (ESPN)

Maelezo ya picha,

City -Kyle Walker, amekamilisha taratibu za kusaini mkataba mpya baada ya kurejesha mahusino mazuri na meneja Pep Guardiola

Eden Hazard mwenye umri wa miaka 28, ambaye amesaini mkataba mpya na Real Madrid , amefichua kuwa mlindalango wa zamani wa Chelsea Thibaut Courtois alisaidia kumshawishi ajiunge na Real Madrid. (Football.London)

Kiungo wa kati wa Fulham Cody Drameh, mwenye umri wa miaka 17, anatarajiwa kuwa nyota wa hivi karibuni ikuhamia Bundesliga kufuatia mkataba mpya na Eintracht Frankfurt. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Chelsea anayecheza kwa deni -Tiemoue Bakayoko, mwenye umri wa miaka 24, anasema "hana chaguo " ila kurejea katika klabu hiyo . (L'Equipe - France)

Wolves wamejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na mshambuliaji wa West Brom -Salomon Rondon, mwenye umri wa miaka 29, kutokana na gharama ya mkataba. (Football Insider)

Maelezo ya picha,

Wolves wamejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na mshambuliaji wa West Brom -Salomon Rondon kutokana na gharama ya malipo

Mlindi wa Lazio -Jordan Lukaku yuko tayari kwa mkataba wa kubadilishana nafasi na nahodha wa Newcastle Jamaal Lascelles, mwenye umri wa miaka 25. (Il Messaggero - Italian)

West Ham wameafiki mkataba wenye thamani ya pauni milioni 40 kwa ajili ya mshambuliaji wa safu ya kati wa Villarreal Pablo Fornals,mwenye umri wa miaka 23. (Football Insider)

Tottenham wamejiandaa kuvunja rekodi yao ya uhamisho mara mbili msimu huu ili mradi wasaini mkataba na wachezaji maarufu -Giovani Lo Celso wa Real Betis mwenye umri wa miaka 23 na kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele, mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)