Maurizio Sarri: Chelsea yakubali mkataba wa meneja kujiunga na Juventus

Lakini Sarri aliweza kushinda kombe lake la kwanza kabisa kama meneja kwa ushindi wa 4-1 dhidi ya Arsenal mwezi mei katika fainali ya Ligi ya Europa
Maelezo ya picha,

Lakini Sarri aliweza kushinda kombe lake la kwanza kabisa kama meneja kwa ushindi wa 4-1 dhidi ya Arsenal mwezi mei katika fainali ya Ligi ya Europa

Chelsea imekubali mkataba kimsingi unaomruhusi meneja wake Maurizio Sarri kujiunga na upande wa machampioni wa Serie A - Juventus.

Makubaliano hayo yamefikiwa Alhamisi jioni baada ya mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu . Mkataba unaweza kukamilika Ijumaa.

Inafahamika kuwa gharama ya fidia ya ziada ya pauni milioni 5 imekubalika na pande husika.

Sarri aliwasili kutoka Napoli mwezi Julai 2018 na kukiongoza kikosi cha Blues kufikia nafasi ya tatu katika Primia Ligi na kushinda kombe la Ligi ya Europa katika msimu wake mmoja wa uongozi wake.

Licha ya kusaini mkataba wa miaka mitatu mwezi Julai mwaka jana, atakuwa ni meneja wa tisa mwenye mkataba wa muda wote kuondoka chini ya mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich.

Kwa kipindi chote alichofanya kazi katika Stamford Bridge Muitaliano huto mwenye umri wa miaka 60- kumekuwa na tetesi za mara kwa mara kuhusu nafasi kazi yake, huku mashabiki wa Chelsea walielzea kutoridhishwa kwao na mbinu pamoja na namna timu inavyochaguliwa.

Moja ya matukio ambayo yalimshushia hadhi lilitokea mwezi Februari ambapo mlindalango Kepa Arrizabalaga alikaidi maagizo yake kwa kukataa kuondoka uwanjani alipoagizwa apumzike katika mchezo wa fainali ya kombe la Carabao uliochezwa Wembley, muda mfupi kabla ya Chelsea kuchapwa kwa mkwaju wa penati na Manchester City.

Maelezo ya picha,

Maurizio Sarri atakuwa ni meneja wa tisa mwenye mkataba wa muda wote kuondoka chini ya mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich

Lakini Sarri aliweza kushinda kombe lake la kwanza kabisa kama meneja kwa ushindi wa 4-1 dhidi ya Arsenal mwezi mei katika fainali ya Ligi ya Europa, ana baada ya mezi alisema "anastahili'' kubaki katika klabu.

Chelsea kwa sasa hawajaweza kusiani mkataba na mchezaji yeyote baada ya kupigwa marufuku kwa misimu miwili ya uhamisho na Fifa - uamuzi ambao wameupinga na kukata rufaa dhidi yake katika mahakama ya utatuzi wa mizozo ya michezo.

Mzezaji wao nyota Eden Hazard amejiunga na Real Madrid kwa gharama ambayo inaweza kupita pauni milioni 150.

Cha ajabu , Chelsea hawajaomba kuahirishwa kwa marufuku hadi uamuazi wa mwisho utakapofikiwa. Hii inamaanisha kuwa mchezaji mpya atakayewasili kwenye klabu hiyo huenda akawa ni mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic, anayesaini mkataba wa pauni milioni 58 kutoka Borussia Dortmund mwezi Januari.

Juventus hawana meneja baada ya Massimiliano Allegri kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita, baada ya kushinda ligi katika kila moja ya misimu mitano tangu achukue uongozi mwaka 2014.

Mwaka wa Sarri katika Stamford Bridge

Baada ya kusifiwa kwa mbinu zake katika Napoli, alitaka kuanzisha 'mpira wa Sarri ' kwa wachezaji wake wapya wakati Chelsea ilipoanzisha kampeni yake ya Primia Ligi na kucheza gemu 12-bila kuchapwa.

Lakini Blues hawakuwa na taji baada ya kushindwa katika mechi tatu kati ya nne za Primia Ligi kuanzia Januari to February, ikiwemo ilipopigwa 6-0 na waliokuwa washindi Manchester City, jambo lililowafanya waporomoke hadi nafasi ya sita kwenye chati.