Honduras v El Salvador: Mechi ya mpira iliyoanzisha vita

El Salvador's football team ahead of the deciding match with Honduras in June 1969 Haki miliki ya picha PA
Image caption El Salvador's team ahead of the deciding match against Honduras on 27 June 1969

Mwaka 1969, mataifa ya El Salvador na Honduras yalipigana kwa siku nne na kuacha maelfu wakipoteza maisha na maelfu wengine wakipoteza makazi- umwagaji huo wa damu baado unakumbukwa kama Vita vya Mpira wa Miguu.

Matokeo yalikuwa 2-2 baada ya dakika 90 katika uga wa Azteca jijini Mexico City. Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu baina ya Honduras na El Salvador ndani ya wiki chache; wote wakisaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 1970. Michuano ambayo mataifa hayo mawili walikuwa hawajawahi kushiriki.

Honduras walipata ushindi mwembamba kwenye mechi ya kwanza wa 1-0 katika mji mkuu wao wa Tegucigalpa, kishaEl Salvador wakaandikisha ushindi wa 3-0 nyumbani San Salvador.

Ripoti za vurugu zilitawala mech izote.

Katika mechi ya tatu, dakika 11 ya nyongeza huku matokeo yakiwa 2-2 mchezaji wa El Salvador Mauricio "Pipo" Rodríguez alichomoka kwa kasi katika eneo la penati na kunganisha krosi iliyomshinda kipa wa Honduras Jaime Varela.

"Nilipofunga lile goli, Nilifikiri muda usingetosha kwao kupata tena matokeo ya suluhu dhidi yetu," anakumbuka Rodríguez, miaka 50 baada ya mchezo huo. "Nilikuwa nahakika kuwa kwa goli lile tutashinda."

El Salvador kweli waliibuka na ushindi wa 3-2. Wachezaji wakakumbatiana, wakapeana mikono na kutoka uwanjani.

Baada ya wiki tatu, mataifa hayo yakaingia vitani.

El Salvador - ambayo ni ndogo mara tano kwa eneo la kijiografia kwa Honduras - ilikuwa na idadi ya watu milioni 3 mwaka 1969.

Sehemu kubwa ya ardhi ilikuwa ikimilikiwa na mabwanyenye wachache, huku wakulima maskini wakiachiwa maeneo machache.

Honduras yenyewe licha ya kuwa kubwa kieneo ilikuwa na idadi ya watu miioni 2.3.

Matokeo yake yalikuwa ni, katika kipindi chote cha karne ya 20, raia wa Salvador walikuwa wakihamia Honduras ili kuendeleza ardhi kwa kilimo binafsi na kufanya kazi katika makampuni ya matunda kutoka Marekani.

Kwa mwaka 1969, inakadiriwa watu 300,000 walihama l Salvador na kuingia Honduras.

Mambwanyenye wa El Salvador walikuwa wakiunga kono hama hama hiyo, kutokana na kuwa iliipunguza presha ya watu kutaka kuchukua ardhi yao na kugawana.

Lakini kwa wakulima masikini wa Honsuras hawakulipenda kabisa suala hilo sababu wao pia walikuwa wakitaka mabwanyenye wao.

Kutokana na hali hiyo, Serikali ya Honduran ikaja na mpango wa cha kufanya. Sheria ya ardhi ilipitishwa ili kuondosha suitafahamu hiyo.

Lakini sheria yenyewe haikuyadhibiti mashamba ya Wamarekani bali aardhi iliyotwaliwa na wageni kutoka El Sarvador.

Rais wa Honduras Oswaldo López Arellano akaanza kuwatimua maelfu ya wahamiaji kutoka El Salvador.

Kama hilo halitoshi, kulikuwa na mgogoro juu ya mpaka wa ardhini n majini.

"Kwa kiasi kikubwa vita ilikuwa ni ya kugombea ardhi, watu wengi katika eneo dogo la ardhi, huku mabwanyenye wakikuza mambo kupitia vyombo vya habari," anasimulia Dan Hagedorn, mwandishi wa kitabu cha Vita ya Saa 100, kinachoelezea mgogoro huo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya raia walijikuta mashakani juu ya mzozo huo

Rais wa El SalvadorFidel Sánchez Hernández na serikali yake walikuwa wakihangaika juu ya namna ya kupokea maelfu ya raia wake waliokuwa wakirejea nyumbani, huku mabwanyenye wa nchi hiyo wakitoa msukumo wa jeshi kujibu mapigo.

Taarifa za uchochezi juu ya kuuawa watuna hata tuhuma za ubakaji zikaripotiwa magazetini.

Yote hayo yalipelekea kuongezeka kwa hasira nchi hizo zilipokutana uwanjani.

"Ilikuwa ni zaidi ya mambo ya kisiasa," anaeleza Ricardo Otero, mtangazaji wa michezo raia wa Mexico. "Kukatokea hizo mechi tatu za kufuzu kuelekea kombe la dunia la mwaka 1970. Haikusaidia kutatua mgogoro. Mpira wa miguu huku Amerika Kusini ni mchezo unaopendwa sana - kwa mabaya na mazuri. "

Haki miliki ya picha Bettmann/Getty Images

"Tuliona ni jambo la lazima na uzalendo kwetu kushinda kwa ajili ya nchi yetu El Salvador," Rodríguez anaeleza. " Nafikiri wote tulikuwa na woga wa kupoteza mchezo, kutokana na yale yaliyokuwa yakendelea basi tungekuwa tunaoandamwa na aibu maisha yetu yote."

"Ambacho tulikuwa hatujui ni umuhimu wa ushindi na goli lile la dakika za lala salama - kuwa lingetumika kama lama ya vita."

'Nini kinachoendelea?'

Juni 27, 1969 wakati wachezaji wakijiandaa na mpambano uwanjani, El Salvador ikavunja mahusiano ya kidiplomasia na Honduras.

Waziri wa mambo ya ndani Francisco José Guerrero akasema takribani Wasalvador 12,000 waliondoka Honduras baada ya mechi ya pili huku gazeti la Uingereza la Guardian likiripoti kuwa waziri huyo "alilaumu juu ya mauaji yatokanayo na mechi ya kimataifa ya mpira."

Siku moja baada a mchezo, Shirika la habari la Marekani la UPI liliandika taarifa yenye kichwa cha habari El Salvador yashinda "Vita ya Soka 3-2".

Taarifa hiyo ilidai kuwa polisi 1,700 wa Mexico walitumika kuzuia ghasia huku mashabiki wa Salvador wakiwaita mashabsikili wakiimba "wauaji, wauaji" wakiwalenga Hoduras.

"Watu wa ughaibuni ndio walioanza kusema goli langu limechochea vita," anasema Rodríguez. "Vita ingetokea hata kama goli lisingefungwa."

Haki miliki ya picha AFP/Getty

Baada ya mechi, ghasia za mpakani ziliongezeka.

Julai 14, El Salvador ilitoa amri kwa vikosi vyake kuivamia Honduras, na ndege za kivita zikaingia mawinguni kushambulia nchi jirani.

Mwandishi wa habari raia wa Poland Ryszard Kapuscinski alikuwepo eneo hilo pale vita ilipoanza.

Ameandika kwenye kitabu chake cha mwaka 1978, chenye jina la Vita vya Mpira (The Soccer War) kuwa kulikuwa na michoro ya ukutani zilizosomeka "Hakuna anayeweza kuipiga Honduras" na "Tutalipiza kisasi 3-0".

Pale ambapo nchi za Amerika zilikuwa zimefanikiwa kusuluhisha mgogoro huo Julai 18, tayari watu 3,000 walikuwa washapoteza maisha. Wengi zaidi walikuwa wamepoteza makazi.

Baada ya shinikizo kali la kimataifa El Salvador iliondoa vikosi vyake Honduras mwezi Agosti.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Baadhi ya askari wastaau waliopigana vita hiyo wangali hai

Lakini maumivu hayakuishia hapo. Biashara ikasimama kwa miongo kadhaa baina ya mataifa hayo mawili kufuatiwa kufungwa kwa mpaka.

Dkt Mo Hume, ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Glasgow, anasema matatizo ya ndani kwa El Salvador ambayo yalisababisha Vita ya Soka - idadi ndogo ya mabwanyenye wamiliki ardhi tofauti na idadi kubwa ya aikna pangu pakavu tia mchuzi- yataendelea kuiandama nchi hiyo ya miongo kadhaa ijayo.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Sanamu ya kumbukumbu ya wanajeshi walopigana vita hiyo

Bado kuna uhusiano wa mashaka baina ya mataiafa hayo mawili.

Lakini kwa bwana aliyefunga goli lilozaa vita anasema goli hilo kwake linaendelea kuwa la kujivunia na si vinginevyo.

"Kwangu, goli lile ni chachu ya kujivunia utaifa kupitia michezo," anasema Rodriguez ambaye sasa ana miaka 73.