Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 08.07.2019: Gerrard, Barry, Davies, Pogba, de Gea, Klopp

Pogba Haki miliki ya picha Getty Images

Juventus wanaandaa dau la pauni milioni 120 ili kumnasa kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba, 26. (Times)

Barcelona imeiwapiku Paris St-Germain katika kinyang'anyiro cha kumsaini mshambuliaji kinda wa 16 Louie Barry baada ya nyota huyo kumaliza mkataba wake na klabu ya West Brome. (Sun)

Klabu ya Tottenham ipo katika mazungumzo na beki wa Wales Ben Davies, 26, ili kumpatia mkataba wa muda mrefu. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Steve Gerrard kwa sasa anainoa klabu ya Rangers ya Uskochi

Mmiliki wa Newcastle Mike Ashley amefanya mazungumzo na nyota wa zamani wa Liverpool na kocha wa sasa wa Rangers Steven Gerrard ili kuhamia klabuni hapo. (Mirror)

Beki wa zamani wa Arsenal, Chelsea na England Ashley Cole, 38, anatarajiwa kujiunga na benchi la ufundi la klabu ya Chelsea chini ya kocha mkuu Frank Lampard. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images

Kipa wa Uhispania, David de Gea, 28, anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu ya Manchester United kwa pauni 350,000. (Mirror)

Beki wa pembeni wa klabu ya Celtic na timu ya taifa ya Uskochi, Kieran Tierney 22 anawaniwa na klabu za Arsenal na Napoli. (Telegraph)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anatamani kuifunza timu ya taifa ya Ujerumani siku moja, amesema ajenti wake. (Welt - in German)

Klabu ya Crystal Palace inapanga kumsajili beki kinda wa Chelsea Reece James, 19, ili kuziba pengo Aaron Wan-Bissaka aliyejiunga na Manchester. (Sun)

Nottingham Forest will wanatarajiwa kukamilisha usajili wa kipa wa Manchester City Kosovan Aro Muric, 20,ndani ya siku chache zijazo. (Telegraph)

Mada zinazohusiana