Afcon 2019: Tunisia yailaza Ghana kupitia mikwaju ya penalti na kutinga robo fainali huku Ivory Coast ikiilaza Mali

Tunisia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tunisia imefuzu katika robo fainali ya michuano ya Afcon bila kushinda mechi katika dakika 90

Tunisia iliishinda Ghana kupitia mikwaju ya penlati na kutinga robo fainali michuano ya Afcon dhidi ya Madagascar.

Mlinda lango Farouk Ben Mustapha ndiye aliyekuwa shujaa baada ya kuingia na kuokoa mkwaju wa penalti wa Caleb Ekuban.

Tunisia ilikuwa imekaribia kushinda ilipofikia dakika ya 90 kabla ya beki wa ziada Rami Bedoui kujifunga kupitia kichwa dakika za lala salama alipogusa mpira kwa mara ya kwanza.

Wakati huohuo Wilfried Zaha alifunga goli la ushindi na kuisaidia Ivory Coast kuilaza Mali 1-0 ili kutinga robo fainali ya michuano ya Afcon.

Mshambuliaji huyo wa Crystal Palace ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal aliufukuza mpira wa adhabu uliopigwa na Sylvain Gbohouo na kuupata kabla ya kipa Djigui Diarra.

Mali ilikuwa imepoteza nafasi chungu nzima kupitia Moussa Marega na Moussa Djenopo, wote wakikosa nafasi nzuri baada ya pasi safi.

Haki miliki ya picha AFP

Ivory Coast sasa itacheza dhidi ya Algeria katika mechi ya robo fainali siku ya Alhamisi.

Ndovu hao wameibuka washindi wa komnbe hilo mara mbili mwaka 1992 na 2015 lakini walisonga mbele katika raundi ya muondoani wakiwa katika nafasi ya pili baada ya kushindwa 1-0 na Morocco.

Tunisia ilikuwa inaongoza kupitia goli la mshambuliaji wa IsmailiaTaha Yassine Khenissi aliyepata krosi nzuri kutoka kwa Wajdi Kechrida.

Mshambuliaji wa Leeds Ekuban ndiye mchezaji wa pekee aliyekosa mkwaju wake katika penalti hizo huku Ferjan Sassi akifunga goli la ushindi.

Tunisia sasa itakabiliana na Madagascar iliopo katika nafasi ya 108 duniani siku ya Alhamisi licha ya kutoshinda mechi hata moja katika dakika 90.

Mwewe hao walitoka sare mechi zao zote tatu kabla ya mikwaju hiyo ya penalti dhidi ya Ghana.

The Black Stars walitawala kipindi cha mwanzo cha mchezo huku shambulio la kichwa la Nuhu Kassim likigonga mwamba wa goli.

Walipata bao la kwanza lakini likakataliwa . Thomas Partey alimpigia pasi Jordan Ayew ambaye naye alitoa pasi murua kwa nduguye Andre na kufunga kupitia kisigino.

Refa aliamuru kwamba Partey alikuwa ameunawa huku refa wa kutumia Video VAR akitarajiwa katika mechi za robo fainali, lakini kiungo huyo wa Atletico alikuwa ameuzuia mpira huo kwa kifua.

Tunisia ilitawala mechi wakati Wahbi Khazri ambaye alikuwa na jeraha alipoingia kunako dakika ya 68.

Muda mfupi baadaye kona yake iligonga mwamba wa goli kupitia kichwa cha Khenissi.

Hatahivyo bahati ya Tunisia ilisimama wakati Khazri alimpigia pasi ya kisigino Kechrida ambaye krosi yake ilifagiliwa hadi wavuni na Khenissi.

Shambulio la kiungo wa Ghana Mubarak Wakaso lilipanguliwa kabla ya kuchangia katika bao la kusawazisha.

Beki Bedoui aliingia katika nafasi ya Khenissi katika dakika ya mwisho ili kuongeza ulinzi-lakini alifunga mkwaju wa adhabu wa Wakaso hadi wavuni mwa goli la Tunisia.

Pande zote mbili zilikuwa na fursa dakika za lala salama -lakini zilishindwa kuzitumia hivyobasi mechi ikaishia kuamuliwa kupitia mikwaju ya penalti.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii