Afon 2019: Nigeria na Senegal zatinga nusu fainali baada ya kuzilaza Afrika Kusini na Benin

Goli la dakika za mwisho la William Troost-Ekong Haki miliki ya picha Getty Images

William Troost-Ekong alifunga goli la dakika za mwisho na kuisaidia Nigeria kutinga nusu fainali ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini.

Samuel Chukwueze alifunga goli la kwanza la Nigeria baada ya kupata krosi nzuri kutoka kwka Alexi Iwobi kabla ya kufunga baada ya jaribio la pili.

Hatahivyo Bongani Zungu alisawazisha kupitia kichwa kilichodaiwa kuwa cha kuotea kabla ya refa wa Video VAR kusema kwamba mpira huo ulikuwa umemgonga mchezaji wa Nigeria kabla ya kumfikia.

Lakini mchezaji wa Udeneese Troost-Ekong alifika katika lango la Afrika Kusini katika muda uliotarajiwa na kuweza kucheka na wavu na hivyobasi kuisadia timu yake kufusu nusu fainali.

Wakati huohuo Senegal nayo ilitinga nusu fainali ya kombe hilo baada ya goli lilofungwa na kiungo wa kati wa Everton Idrissa Gueye kuangamiza matumaini ya Benin katika michuano hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters

Gueye alitamba na mpira na kumpigia pasi nyota wa Liverpool Sadio Mane ambaye hakuwa mchoyo akaamua kumrudishia ambapo mchezaji huyo alicheka na wavu.

Refa wa kutumia kanda ya video VAR amezinduliwa katika awamu ya robo fainli ya michuano hiyo hivyobasi Mane alikuwa na magoli mawili ambayo yalikataliwa kwa kuotea.

Mchezaji wa Benin Olivier Verdon alipigwa kadi nyekundu baada ya kumchezea visivyo Gueye.

Kabla ya goli la Gueye, ambalo ni lake la kwanza nchini Misri , Benini ambayo ilitinga hadi robo fainali bila ya kushinda mechi katika dakika 90 karibu ichukue uongozi baada ya masikhara ya mlinda lango Alfred Gomis.

Kipa huyo alishindwa kudhibiti pasi aliopigiwa na mchezaji mwenzake kabla ya mpira huo kutoka nje.

Na sasa Nigeria itacheza dhidi ya Ivory Coast au Algeria siku ya Jumapili katika nusu fainali ya pili.

Haki miliki ya picha Getty Images

The Super Eagles walipata ushindi wa halali na kuongoza kupitia mchezaji wa Villarreal Chukwueze.

Wangeongeza magoli zaidi wakati Williams alipopangua shambulio la Peter Etebo lililopiga chuma cha goli na kutoka nje.

Goli la Zungu lilikuwa la kwanza katika michuano hiyo ya Afrika kukubalia na refa wa VAR.

Goli hilo lilionekana kuwa la kuotea lakini mwaju wa adhabu wa Percy Tau ulimgonga Odion Ighalo kabla ya kumfikia ambapo Zungu alifunga kwa kutumia kichwa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii